Mwenyekiti wa zamani wa benki ya China ahukumiwa kifo

Mwenyekiti wa zamani wa benki ya China ahukumiwa kifo

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Mwenyekiti wa zamani wa Benki ya China, Liu Liange amehukumiwa kifo kwa kupokea hongo ya dola milioni 16.8 (TZS bilioni 44.4) pamoja na makosa mengine ya ufisadi na utoaji wa mikopo kinyume cha sheria.

Mahakama ya China imeamuru mali zote binafsi za Liu zitaifishwe na mapato yake yote yanapaswa kurejeshwa na kuwasilishwa kwenye hazina ya serikali.
 
CCM igeni Sheria mzuri Namba hii kutoka Uchina
 
Mao alishasema hakuna shida mtu mmoja kufa katika population ya watu billion.

Hakuna jipya China inanyonga sana viongozi wa kiserikali
 
Huo utaratibu ukija huku kwetu karibia viongozi wote watafilisiwa na kunyongwa mpaka viongozi wa jumuiya.
 
hii sheria ingekua ni bongo, hawa viongozi wa viyoyozi wote wangekuwa makaburini.
Mkuu,hata wasiokua viongozi,wapo ambao nao wanaiba kwenye maeneo yao ya kazi,wanachukua rushwa kwenye maeneo yao ya kazi,

Wizi ni wizi tu,
wizi mdogo hupelekea kua wizi mkubwa,
Wala rushwa wapo kila sehemu,

China wapo serious na maisha,hawacheki na mtu.
 
Back
Top Bottom