McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex jijini Dodoma, Marico Magale, amesema wamachinga wa soko hilo wamepokea na kuunga mkono uamuzi wa Serikali wa kusitisha mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, wakieleza kuwa hatua hiyo inalenga kulinda amani na usalama wa nchi.
Magale amesema wafanyabiashara hao wanaelewa mantiki ya maelekezo yaliyotolewa bungeni Juni 26, 2026, akibainisha kuwa baadhi ya kauli za kisiasa zinaweza kuchochea hisia na kusababisha taharuki miongoni mwa wananchi.
Ameongeza kuwa wakirejea matukio ya Oktoba 29 yaliyowahi kuathiri shughuli za biashara, wamachinga wa Machinga Complex walipata hasara kubwa, hali iliyowapa funzo kuhusu umuhimu wa kudumisha utulivu wakati wote.
“Maisha yetu sisi wamachinga yanategemea biashara za kila siku. Hatuwezi kupata kipato bila kutoka kufanya biashara. Kwa hiyo tunafahamu kuwa bila utulivu, hata shughuli za kiuchumi zinaathirika,”
Soma Pia: Mwenyekiti wa Wamachinga Arusha: Wamachinga hawakuhusika na maandamano Oktoba 29, wanaiheshimu sana serikali