Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli kuna kitu ambacho haukukifanya kitakuangusha tu kwenye Uchaguzi huu

U

Unachosema ni sahihi lakini huwezi kujenga ghorofa wanaowanakufa njaa
 
Sisi wakulima wa Korosho Pamba na mbaazi pia tuongeze hapo kwenye list
 
Poleni sana...
Ngoja tuone hii miaka mitano iliyobaki labda yatalegea...



Cc: mahondaw
 
Wanasiasa wanasema " You win the people through their stomach"
Yesu Kristo aligeuza mikate mitano na samaki wawili na kuwa mikate mingi na samaki wengi wa kutosha watu 5000. Chakula kilibaki kikakusanywa na kupata vikapu 12.
Yusufu , aliyekuwa Wazari mkuu wa Misri wakati wa Mfalme Farao, alikusanya chakula kwa miaka saba ili aje awalishe watu kwa miaka mingine saba ya njaa.
Kwa hiyo hapa Duniani wanaokumbukwa kwa muda mrefu ni wale wanaowapatia watu chakula.
Ukimpatia mtu ajira, umempatia chakula.
Ukiongeza pesa kwenye mzunguko unawapatia watu chakula.
Watu wa Fedha wanasema " Money works" kwa hiyo kama hakuna pesa watu hawafanyi kazi.
Sasa hivi Mabank mengi hayatoi tena mikopo mikubwa ya kibiashara kwa sababu Benki nyingi hazina pesa na watu wengi wanashindwa kufanya biashara kwa hiyo hawahitaji kukopa.
Ardhi, nyumba nk vimeshuka bei kwa asilimia zaidi ya 75. Ardhi kubwa hapa Inchini inashikiliwa na masikini kwa hiyo waathirika wakubwa katika hili ni masikini.
Mwalimu Nyerere alihakikisha kuwa kila anayemaliza shule hata darasa la saba anapata ajira kama atapenda.
Mwalimu Nyerere alianzisha mashirika ya umma mengi ili kumsaidia mkulima na kuongeza ajira.
Uchumi wa Tanzania haukuharibiwa na Mashirika ya UMMA ila uliyumba sana kwa sababu ya Vita ya Uganda na ukame ulioikumba Inchi kwa kipindi kirefu.
 
Wenye akili wanamuheshimu Walter Rodney, mburula kama wewe lazima wawe na mawazo ya kipunguani yanayoshabihiana na muhanga wa risasi 16, kama mnavyodai
mliosoma sllybus za zamani milifundishwa ujinga eti matatizo ya mwafrika chanzo ni mzungu.Kutawaliwa sio kikwazo cha maendeleo kama alivowapoteza walter rodney,fungua ubongo
 
Nakushukuru kwa mawazo yako, siku zote lazima tuanzie uchumi wa Nchi (macro economy) kisha uchumi wa mtu mmoja mmoja (micro economy). Mhe.Rais JPM kaanza na Uchumi wa Nchi na miundombinu ,sasa 2020 -2025 yatafuata hayo. Ndivyo ilivyokuwa awamu zote. Watumishi wa umma tulipata increment moja, tumelipwa malimbikizo ya madeni (salary Arreas), likizo, kupanda madaraja baada ya uhakiki nk, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Wazazi tunasomeshewa darasa la 1 -12, mzigo michango mbalimbali ya elimu imepungua sana, maana ulikuwa unaambiwa ada 10,000/= michango 380,000/=! Ila misheni town, udalali na vitu vya namna hiyo kwa kweli vimepungua sana. Acha tufanye kazi rasmi.
 
mliosoma sllybus za zamani milifundishwa ujinga eti matatizo ya mwafrika chanzo ni mzungu.Kutawaliwa sio kikwazo cha maendeleo kama alivowapoteza walter rodney,fungua ubongo
Mjinga ni ambae hajui kuwa yeye ni mjinga. Kwa sababu hujijui kuwa wewe ni mjinga baki na ujinga wako. Kama ulisoma syllabus moja na wazazi wako, well and good. But kama wazazi wako walikutangulia, basi kwa maneno yako mwenyewe WAZAZI WAKO NA KIZAZI CHAKO KILICHOSOMA ZAMANI NI KIZAZI CHA WAJINGA. Mjinga huzaa mjinga, so wewe ni mjinga kama walivyo wazazi wako
 
Dogo
Akili yako ni ndogo Kama avatar yako! Siyo kila anayetoa maoni humu mwajiriwa na serikali! Tambua Hilo kwanza kabla hujawashambulia wengine waliojiajiri wenyewe!
Usichokijua kitakusumbua daima. Soma Tena nilichoandika juu ya Sera mbili zilizonadiwa na ccm na kukosa usimamizi na mitaji ambazo zingepewa kipaumbele Kama hiki Cha flyover, sgr na bwawa Basi ajira zingekuwa za kumwaga na ingekuwa historia!
Sera za kilimo na viwanda zilihitaji msukumo mkubwa mno kuliko Ile wa she, flyover na bwawa kwani zingeajiri kuanzia wakulima na wewe unayezurura na bahasha ya kaki kwenye ofisi zetu ukisaka kuajiriwa! Usijifariji hapa Bali iambie ccm yako iache Sanaa na kuwatumia wapigakura wake mafukara na maskioni ili uendelee kuwatawala na kinyume chake itekeleze Sera inazoombea kura ili kuleta maendeleo ya kweli! Hutaki, Baki na ujinga wako na elimu yako iliyoshindwa kukusaidia!
 
Kuwa na lugha ya staha Basi eeh! Wazazi wa wenzako waweke kando na jadili hoja itapendeza kwani hata wewe unao wazazi na usingependa wawe sehemu ya mjadala Tena kwa kuitwa wajinga! Behave yourself please!
 
Akili yako iko uchi.bila Sera madhubuti hayo yote ni hewa.ccm oyeee
 
Mimi ni dotcom thus Sina mawazo ya kijima Kama yako
 
Sasa hao viongozi tunaowachagua wanakazi gani kama si kubadilisha maisha ya mtanzania?
 
From neutral perspective mkuu acha kufananisha ulaya magharibi na Asia (sio yote) na vitu vya ajabu.
Tatizo la serekali yetu inakosa framework ya mipango. Mtu anaweza tu akaamka akasema toa pesa fanya hiki. Chukua bilioni 2 hakikisha hili linaisha in two weeks. Kweli inatakiwa iwe hivyo kikawaida? Kwani hakuna mipango imewekwa mpk tu publisize or rather politicise mambo namna hiyo?
Naamini kinachofanywa kwenye orders kama hizo ni kitu kizuri lakini dah kwani jambo zuri hilo si lilitakiwa liwe na mikakati kabla na fedha zilizotengwa kabla.
Just saying
 
Maisha yako utayabadilisha mwenyewe kwa kuonyesha uthubutu katika kupambana na maisha badala ya kusubiri mwanasiasa akufanyie hivyo. Utasubiri sana kijana.

Si kosa lako, waliokunyima elimu ya Uraia ili usijue umuhimu wa serikali ndio hao wa kuwalahumu. Unapozungumzia Rais unauzungumzia muhimili serikali, serikali ni mwamuzi sawa na refa uwanjani, jukumu lake kubwa ni kuweka sawa mazingira ya ushindani uwanjani pasipo uonevu. Kama ulishawahi lalamika refa Fulani alikuwa mbaya, basi ndio sawa na ukipata Rais mbaya.

Timu inaweza kuwa na uthubutu wa kutosha ila kwa refa mbaya kazi bure.
 
Alichoamua kukifanya JPM na anachoendelea kukifanya sasa, cha kuijenga nchi Kwa miundombinu ndicho kilipaswa kifanywe na awamu ya Kwanza ya pili na tatu,

Kwa kuwa viongozi awamu hizo hawakujikita ktk ujenzi huo, ndio huu ugumu wa maisha tunaouona leo

Kivyovyote ndugu zangu, ili maisha yawe na uahuweni ni lazima mtu awe na kwake, Kwa maana ya kuwa na nyumba aliyoijenga mwenyewe, Kwa kuwa uko tofauti kubwa Kati ya kuishi maisha ya kuanga na maisha yakukaa ktk nyumba unayoimiliki wewe

Lakini, Wakati mtu anajenga nyumba yake! Ni lazima waksti huo awe na maisha magumu,Kwa kuwa itambidi abane matumizi, kama alikuwa na bajeti ya kila wiki ale kuku mara mbili, itamlazimu ale mara moja ikiwezekana Kwa mwezi

Lakini baada ya ujenzi kukamilika, pesa zote za alizokuwa akilia nyumba ya kupanga, nazo atazimiliki yeye

Mf mzuri, Muumbaji wetu, alituwekea miundo Mbinu yote Kwanza, ndipo akatuumba, hii inamana gani

Bila miundo Mbinu, maendeleo hakuna, usafirishaji wa mazao utafanyikaje? Umeme bei nafuu nao utapatikanaje? Usafiri wa anga nao ni mhimu mno Kwa kuwa watu watataka kuja ili nchi ipate pesa za kigeni, mahali pa kutibiwa pakuwa ni karibu vifo visivyo vya lazima vitapungua, mashule yakijenfwa, watoto wengi watapata mahali pa kusoma

Miundo Mbinu ndio Uchumi wenyewee

Ni kweli maisha ni magumu leo, lakini baada ya kuwa tumeimarisha miundo Mbinu yetu, Hali itakuwa Bora zaidi,

Chaguo sahihi la watu wanaoona mbali, Si mwingine, ni JpM pekee,

Anajua kusimamia pesa zetu, hacheki na mzungu Wala nyani
 

We akili hauna hiyo milion mbili inatoka wap🤔

We ni bunju
 

Hongera sana kwa mchango wako, binafsi naachana na mahaba kwa Magufuli hafai kabisa kabisa anatembea anagawa fedha halafu haoni umuhimu wa watu wengine, ngoja ajifunze kulimia meno, upepo wa kisulisuli atauona atalii ahuuu ahuuu,!!!
 
2020 watanzania tutamchagua JPM kwa kura za kutosha.
Mazuri ya JPM ni mengi sana,changamoto huwa zipo tu.hata U.S kuna raia wanalalamikia changamoto za taifa lao.
ilhali tunaambiwa U.S ni kinara wa kila jambo la kimaendeleo.
Wasiojulikana buana!
 

Mtaisoma namba na ngonjera zenu, fyuuu......na mtajamba sana mgombea wenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…