Mwenyezi Mungu, nifanye lipi ili ujibu ombi langu, niwe vipi ili unitue mzigo huu? Mbona ni kama umenifumbia macho hunioni

Mwenyezi Mungu, nifanye lipi ili ujibu ombi langu, niwe vipi ili unitue mzigo huu? Mbona ni kama umenifumbia macho hunioni

Mimi sio bora kuliko wengine ila napambana kwa namna ilio haki, kwa namna ilio ya juhudi huku namtanguliza alioiumba dunia hii.

Kila nachogusa ni kama kiko allergic na mikono yangu, hakiwi ridhiki, hakikaii, watoto watakula nini, nimtamtunza vp huyu mrembo ambae Mungu alinijalia.

Mimi ni mpumbavu kuliko wote? Mimi ni mdhambi kuzidi wadhambi wengine?

Je, natwanga maji kwenye kuni? Je nasukuma ukuta? Maana baba jitihada yangu kukufikia hailingani na muelekeo nilio nao.

Mama anataabika, mimi nitaabika, mdogo wangu anataabika,

Nimemuona mama yangu akikuliliia miaka nenda miaka rudi ila bado amekuwa rafiki wa tabu na mateso,.

Je, baba yangu ni laana umeiruhusu katika nzao yake, je ni basi tu hatupo katika mipango ya baraka zako?

Nashuhudia tu makuu ya hii dunia, hata walio na dhambi wakifurahia kiasi, ila mimi nimekuwa cas study ya tabu

Mbona saul alikuwa muuaji ila ulimpa ukuu wa milele, mimi ni wa aina gani hadi niwe mtumwa wa dhiki kiasi hiki

Baba, nimekufanyia makubwa, nimekulilia, hata kama nilikosea ila ilikuwa ni kwa jina lako.

Kwanini utake kuruhusu nifanye maamuzi utafikiri mlugha mlugha ambae hajawi kukutumainia?
Kumbuka Jairo, alienda kwa Yesu akaomba Yesu aende nyumbani kwake, aweke mkono wake juu ya kichwa cha mtoto wake apone. Yesu akasema tunakwenda, ila wakachelewa njiani.

Mara wasaidizi wa Jairo wakafika toka nyumbani na kilio wakimwambia Jairo, wala usimsimbue Yesu, mtoto amekufa. Jairo hakulalamika kwa Yesu kwanini amechelewa kusikia na kutekeleza ombi lake. Na Yesu alimwambia Amini tu. Yaani AAMINI mtoto atapona. Jairo aliamini.

Ndugu, mwamini Mungu usimtilie mashaka kuwa hajibu. Ukiacha kuamini na kuweka mashaka anakupa kulingana na mashaka yako, yaani picha inayoiona kwenye mashaka yako ndiyo utaiona kwenye maisha yako. Ukiamini, unakuwa na picha ya kile kizuri unachokitarajia na utakipata. Anza kuamini
 
Mkuu naona una manguniko !a lawama , hii sio njia nzuri.

Anza kushukuru na kujua kanuni za Mungu ndipo mema yatakujia.
Iko siri katikavkushukuru, kuomba na kuamnini
Tuache unafki, wewe unaweza kushukuru kulala njaa? Una madeni kila kona, watoto wamefukuzwa shule huna pesa ya kulipa ada utashukuru tu?
 
Mleta mada punguza matarajio makubwa au ya aina fulani, punguza matazamio ya aina fulani, kuna sisi wenzako huku mfumo wa maisha yetu tukiucompare na wako wewe una weza kua na heri mara nyingi lakini hatuvunjiki moyo au kukata tamaa, maana nilipo mimi kwa sasa hivi sina hakika ya kesho nitakula nini lakini niko na amani maana kuna ambaye yeye hawezi kujilinganisha na mimi nimempita mara nyingi lakini nae ana amani na tumaini pia yupo na furaha, naongea hivi kwa ushuhuda kabisa.
Lisilo kuua linakuimarisha.
Umemaliza mkuu.
Kama ni kweli hiyo hali aliyoandika ipo hivyo; basi afanye kumwomba Mungu msamaha kwani inavyoonekana ni amekata tamaa, anamtaka Mungu afanye kitu kama yalivyo matarajio yake i.e. Anampangia Mungu cha kufanya. Hataki Mungu afanye kadri ya mapenzi yake na kwa wakati unaofaa. Laiti angelikopi na kupesti hiyo komenti yako hapo👆👆 na awe anaisoma kila siku, nadhani ingemsaidia sana badala ya Kumkufuru Mungu kwamba eti huenda Mungu ameshindwa au hataki kwa makusudi kukisikiliza kilio au kuyasikia maombi yake. Huyu mleta mada hata hatambui kwamba tayari amesha pokea zawadi na baraka Uhai, Afya njema na Akili timamu Maisha mema ya Amani hadi ameweza kuja kuandika hapa:KEKBye:
 
Tuache unafki, wewe unaweza kushukuru kulala njaa? Una madeni kila kona, watoto wamefukuzwa shule huna pesa ya kulipa ada utashukuru tu?
Ndiyo tena kwa adabu na Heshima kubwa. Sababu ni hizi hapa:
1. Umelala njaa ok. Lakini si upo Hai?
2. Madeni uliyo nayo ni mengi na ya uzito gani kiasi kwamba huoni hata wenzio nao wanamadeni. Nchi zinakopa (Madeni)sembuse iwe mtu mmoja mmoja?. Madeni ni sehemu ya maendeleo.
3. Watoto wamefukuzwa shule - Kwani wameuawa?? Umeambiwa kwamba utoaji wa Elimu umesitishwa? -Watoto wataenda shule utakapopata hela. Pambana upate fedha hata ya mkopo.
Unatakiwa kushukuru tena mno kwani wapo wenzako ambao habari ya "leo watakula" au watakuwa Hai dk. inayofuata haipo e.g. huko Gaza na Lebanon n.k.n.k. yan tumaini la kuendelea kuwepo halipo.
 
Back
Top Bottom