Mwenyezi Mungu, nifanye lipi ili ujibu ombi langu, niwe vipi ili unitue mzigo huu? Mbona ni kama umenifumbia macho hunioni

Mwenyezi Mungu, nifanye lipi ili ujibu ombi langu, niwe vipi ili unitue mzigo huu? Mbona ni kama umenifumbia macho hunioni

Mimi sio bora kuliko wengine ila napambana kwa namna ilio haki, kwa namna ilio ya juhudi huku namtanguliza alioiumba dunia hii.

Kila nachogusa ni kama kiko allergic na mikono yangu, hakiwi ridhiki, hakikaii, watoto watakula nini, nimtamtunza vp huyu mrembo ambae Mungu alinijalia.

Mimi ni mpumbavu kuliko wote? Mimi ni mdhambi kuzidi wadhambi wengine?

Je, natwanga maji kwenye kuni? Je nasukuma ukuta? Maana baba jitihada yangu kukufikia hailingani na muelekeo nilio nao.

Mama anataabika, mimi nitaabika, mdogo wangu anataabika,

Nimemuona mama yangu akikuliliia miaka nenda miaka rudi ila bado amekuwa rafiki wa tabu na mateso,.

Je, baba yangu ni laana umeiruhusu katika nzao yake, je ni basi tu hatupo katika mipango ya baraka zako?

Nashuhudia tu makuu ya hii dunia, hata walio na dhambi wakifurahia kiasi, ila mimi nimekuwa cas study ya tabu

Mbona saul alikuwa muuaji ila ulimpa ukuu wa milele, mimi ni wa aina gani hadi niwe mtumwa wa dhiki kiasi hiki

Baba, nimekufanyia makubwa, nimekulilia, hata kama nilikosea ila ilikuwa ni kwa jina lako.

Kwanini utake kuruhusu nifanye maamuzi utafikiri mlugha mlugha ambae hajawi kukutumainia?
Mhubiri 9:11
Nikarudi na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo, lakini wakati na bahati huwapata wote.
 
ammeeeeeen
 
Usikate tamaa, Endelea kumtumainia Mungu, Kadri Giza linavyozidi kuwa nene, Ndivyo Pambazuko linakaribia. Kumbuka Mungu hachelewi wala hawahi kujibu maombi yetu, Bali hujibu kwa wakati na majira yanayofaa! Huenda anazo sababu zake ambazo sisi hatuzioni wala hatuwezi kuzielewa, Huenda tukaomba gari ila akakawia kujibu ombi akikuepusha na ajali mbaya ambayo ingekupata na hilo gari! Endelea kumuamini Mungu, Yupo, anajua, na atakujibu!
Isaya 41:10 “usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu”.
Amen
 
Achana na Mungu mchovu na mdhaifu.

Hakuna Mungu anayejibu maombi.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Kwanza lazima ujue, No one is coming to save you.

You are responsible to save your own life, Pambana kaza mpaka kieleweke.

This world is not for the weak and lazy people. You either go hard, go home or you die.

Acha kulia lia.

Find ways to make money because nobody cares about your sufferings.
 
Hakuna asiye na shida wewe, au unadhani uko peke yako? Na watoto wanaokufa njaa nao wamlilie nani? Maisha sio fair, fanya unachoweza au kaa chini upoteze muda kulaumu na kulalamikia imaginations.

Honestly hutakiwi kuonewa huruma wala kufarijiwa hata kidogo kama wafanyavyo hawa members.
Roho mbaya tu wewe
 
Angalia nidhamu yako binafsini, Tabia zako zinapatana na malengo?

Mungu, Kuomba , Maombi, havihusiani na mafanikio.

Kuna watu ni matajiri kupitia kuumiza watu, hawa Mungu hawaoni ili awaadhibu au?
 
Shirki hiyo, unamshirikisha Mungu kwenye huo ulozi wa chumvi?
Chumvi ni ya kuweka kwenye chakula siyo kujipata ili Mungu akusikie.
Huna akili wewe mbwa kabisa.

2 Wafalme 2:21​

Elisha akaenda kwenye chemchemi ya maji, akatupa chumvi hiyo ndani na kusema, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimeyafanya maji haya kuwa yenye kufaa; tangu sasa hayatasababisha vifo au kutoa mimba.”
 
Mimi sio bora kuliko wengine ila napambana kwa namna ilio haki, kwa namna ilio ya juhudi huku namtanguliza alioiumba dunia hii.

Kila nachogusa ni kama kiko allergic na mikono yangu, hakiwi ridhiki, hakikaii, watoto watakula nini, nimtamtunza vp huyu mrembo ambae Mungu alinijalia.

Mimi ni mpumbavu kuliko wote? Mimi ni mdhambi kuzidi wadhambi wengine?

Je, natwanga maji kwenye kuni? Je nasukuma ukuta? Maana baba jitihada yangu kukufikia hailingani na muelekeo nilio nao.

Mama anataabika, mimi nitaabika, mdogo wangu anataabika,

Nimemuona mama yangu akikuliliia miaka nenda miaka rudi ila bado amekuwa rafiki wa tabu na mateso,.

Je, baba yangu ni laana umeiruhusu katika nzao yake, je ni basi tu hatupo katika mipango ya baraka zako?

Nashuhudia tu makuu ya hii dunia, hata walio na dhambi wakifurahia kiasi, ila mimi nimekuwa cas study ya tabu

Mbona saul alikuwa muuaji ila ulimpa ukuu wa milele, mimi ni wa aina gani hadi niwe mtumwa wa dhiki kiasi hiki

Baba, nimekufanyia makubwa, nimekulilia, hata kama nilikosea ila ilikuwa ni kwa jina lako.

Kwanini utake kuruhusu nifanye maamuzi utafikiri mlugha mlugha ambae hajawi kukutumainia?
Usimpangie Mungu namna ya kukubariki. Bado kidogo utaenda kwa waganga.
 
Back
Top Bottom