Mwenzenu Napita kipindi kigumu sana

Mwenzenu Napita kipindi kigumu sana

ngoshwe

mkuu kama vipimo vyote ni negative na bado unaumwa basii utakua unastress zina kusumbua na zimekusababishia condition inaitwa psychosomatic disoder, ni jinsi ubongo unaposhindwa kukabiliana na stress za mda mrefu kwahio inaamishia kwenye viungo...yaani unasikia kama unaumwa lakini ukipima majibu ni negative.

ushauri wangu ni kwamba nenda kawaone wataalamu wa akili, njoo hapa muhimbili kuna department ya psychitry watakusaidia
 
Last edited by a moderator:
ngoshwe

Lazima utakuwa umerogwa, ni pm nitakupa contact ya mganga atakusaidia sana

Ubarikiwe!

Sasa kwa kuwa wewe yalikukuta na ukatibiwa huko ndio uje useme kuwa mungu kakusaidia? au unataka kuleta kufuru tu? wewe ulienda huko na unaweza kumshauri aende au asiende lakini msaada wa huko mungu hausiki, ni nguvu za giza tu, na ndio hao hao wanaosababisha albino wanakatwa mikono na miguu.
Kuna tabu gani kutibiwa kwa mganga wa kienyeji, kwako lazima ziwe nguvu za giza kwa kuwa hujui tiba inafanyikaje na ni kazi ya kitaalamu. Kuhusu albino kukatwa miguu huwezi kulaumu wahandisi wa barabara kuwa wanasababisha ajali.
ngoshwe

Ndugu yangu usupoteze muda huko mahospitali, yashanikuta hayo
Nenda kwa watalaam wa kiswahili aisee mungu atakufanyia wepesi.pole sana
Nashukuru kwa ushauri wako wa wazi, sema neno 'wataalamu wa Kiswahili' lina ukakasi. Mweleze kwa uwazi kuwa aende kwa mganga wa kienyeji na Mungu atamfanyia wepesi pasi na shaka!

Mh pole sana mkuu, hapo inawezekana hata mambo ya 'kiswahili' yanahusika, hebu kama ww ni mkiristo nenda kafanyiwe maombi kanisani!
Kufanya maombi ni kamari na kupoteza muda. Maombi yangekuwa na msaada hao waombaji wangetembelea mahospitali, hasa kwa kuwa ni kazi ya Mungu.

================
================

ngoshwe,

Mwiba hutokea mahali ulipoingilia. Kama tatizo lako lina kila dalili kuwa ni la kurogwa usipoteze muda kwenda hospitali, huko huwa hawakosi sababu ya kukwambia na hata siku ukifa vipimo vya post-mortem havitakosa cha kusema.

Sema tatizo lako kwa uwazi ili usije kutapeliwa na wanaojifanya waganga hali ikawa mbaya. Ukishafikia uamuzi wa kupata tiba sahihi wasiliana nami nikuelekeze mahali pa kwenda!
 
Last edited by a moderator:
ngoshwe

mkuu kama vipimo vyote ni negative na bado unaumwa basii utakua unastress zina kusumbua na zimekusababishia condition inaitwa psychosomatic disoder, ni jinsi ubongo unaposhindwa kukabiliana na stress za mda mrefu kwahio inaamishia kwenye viungo...yaani unasikia kama unaumwa lakini ukipima majibu ni negative.

ushauri wangu ni kwamba nenda kawaone wataalamu wa akili, njoo hapa muhimbili kuna department ya psychitry watakusaidia

Kaka mi wlinipeleka huko waka niintaview na kunianzishia cjui clinic nikaenda kama mara 3 hamna k2 wakaamuaa kunifuta tu, hayo matatizo yapo ni viumbe vingine hvyo havitibiki bila watalaam asili aisee.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana , makushauri kwa hayo uliyoeleza nenda kwenye maombi kwa florian katunzi pale viwanja vya mwalimu nyerere sabasaba ukaombewe hizo ni nguvu tu za giza na shida hiyo itakwisha kabisa
 
Ushauri wangu, mkuu nenda kwa matabibu wa asili utapata msaada huko!
Ikumbukwe kuwa tabibu ni sababu tu ya kupona ila mponyaji hasaa ni Mwenyezimungu mtukufu!!!!
Kwa hiyo unapoenda kwa tabibu tegemea kupona kwa uweza wa mwenyezimungu!!!
Na maombi tu bila kutafuta sababu ya kupona ni kazi bure na hawezi kutokea hivyo!!!!!
 
Acheni na imani potofu, mara maombi mara kwa waganga wa kiswahili, nenda hospitali tu, achana na matapeli , fuata tiba za kisayansi utapona
 
hayo ni mapepo/ majini yamekuingia, na wewe ndie chanzo ama kwa tabia zako au kuna mtu amekutupia. cha kufanya amini kwamba yesu anaweza kila jambo hakuna gumu la kumshinda kata shauri mpokee bwana yesu, amini anaweza kukuponya na hiyo hali na nyinginezo kisha tafuta kanisa lenye nguvu ya mungu (sio kila kanisa wana nguvu ya mungu) nenda uombewe na ujifunze kujiombea mwenyewe.
 
tatizo lako si kubwa. bado una vodonda vya tumbo na hujagundua. epuka vyakula hatarishi nawe utakuwa salama, japo hutapona vidonda
 
hayo ni mapepo/ majini yamekuingia, na wewe ndie chanzo ama kwa tabia zako au kuna mtu amekutupia. cha kufanya amini kwamba yesu anaweza kila jambo hakuna gumu la kumshinda kata shauri mpokee bwana yesu, amini anaweza kukuponya na hiyo hali na nyinginezo kisha tafuta kanisa lenye nguvu ya mungu (sio kila kanisa wana nguvu ya mungu) nenda uombewe na ujifunze kujiombea mwenyewe.

shukran mkuu
 
Back
Top Bottom