Mwezeshe Fidel80 afike kwa Babu

Mwezeshe Fidel80 afike kwa Babu

Kweli utakua unatatizo kubwa ndugu yangu kama wewe ndio huyu kwenye avater yak😵K ngoja tuone jinsi ya kukusaidia
 
Fidel za bia unazo ila za kwenda loliondo tukuchangie mmmmmm jamani!
 
usingenunua vocha au kwenda net kuandika ujumbe huu ungekuwa na zaidi ya hiyo Tsh 500/= unayoiomba hapa
 
Fidel za bia unazo ila za kwenda loliondo tukuchangie mmmmmm jamani!

gaga jamani....kwa nini unamsimanga mwenzio.....mwache apate mchango afike kwa babu....maadamu mzee wa Kiraracha kafika na wengineo...
 
Nina wasiwasi mchango unaweza kuishia kaunta ya bar!
 
Fidel mchango wangu nitakutumia kwa M-pesa, Lakini ujue kabisa, ukishakunywa dawa hakuna kunywa pombe, wala kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Ukifanya hivyo huponi tena, na magonjwa yanakurudia.

Hivi ni kweli haya masharti Babu anayatoa au watu mnajitungia?
 
usingenunua vocha au kwenda net kuandika ujumbe huu ungekuwa na zaidi ya hiyo Tsh 500/= unayoiomba hapa

Tatizo nauli toka Usalule mpaka A town huko kwenda na kurudi si chini ya 300,000 na kila kitu
 
Hujafanikiwa tu kupata nauli bado??

Fanya fasta mie nakusubiri Arusha twende wote ila dahhh Fairway ndo kwaheri
 
Waungwana napenda nifike kwa Babu hapo Loliondo na mm nikanywe Juice ya Babu nimegundua juice ya babu ina husika sana katika kuokoa maisha ya mwanadamu. Babu amekuwa ndo kimbilio la wanyonge na matajiri.
Mimi nashindwa kufika kwa babu kutokana na kipato kunikaba jamani naomba michango yenu ya hali na mali sibagui mchango ili niweze kufika kwa Babu niokoe maisha yangu. Mnao penda kuchangia mtu akitangulia mbele ya haki onyesheni ungwana wenu kipindi hiki ambapo sijatangulia mbele ya haki.
Mchango wako naomba unifikishie mm mwenyewe au hawa wafuatao nina imani nao;-
Mchungaji Masanilo
Babu Asprin,
Carina Ti
Kimey
Kutoa ni moyo wala si utajiri waungwana.
Mkono mtupu haulambwi.
Sura sio roho.

Waambie walete kwangu pia hiyo michango
 
Back
Top Bottom