Mwezi huu nimekataliwa na warembo 4 kwa sababu ya kuwa na nywele nyekundu

Mwezi huu nimekataliwa na warembo 4 kwa sababu ya kuwa na nywele nyekundu

Pesa unazo za kutosha??
Au ni pesa zile za kulalamika huyu demu anapenda sana sana😏

Mpe vitu anavyotaka uongeze na ambavyo hajasema halafu urudi kutuambia😅😅
Mwanamke kama sio mke wangu na haishi kwangu nitampiga mbupu tuu aende zake, kama hataki akajambe mbele huko.

swala la kumuhudumia aende akaongee na wazazi wake vizuri maana ni wajibu wao huo, mie ntampa asicho pewa na wazazi wake tu ,tusibebeshane majukumu yasiyo yetu.
 
Mwanamke kama sio mke wangu na haishi kwangu nitampiga mbupu tuu aende zake, kama hataki akajambe mbele huko.

swala la kumuhudumia aende akaongee na wazazi wake vizuri maana ni wajibu wao huo, mie ntampa asicho pewa na wazazi wake tu ,tusibebeshane majukumu yasiyo yetu.
Maneno makavu mno haya
 
Jamani hali gani?

Niruke kwenye hoja yangu. Mimi ni mwanaume handsome tu safi, ninajua kuvaa na nina vihela vya kubadili mboga na tugari. Nimekuwa nikipata shida mno kupata mwanamke wa kuingia naye mahusianoni kwa sababu ya shida yangu ya nywele nyekundu.

Nina nywele nyekundu ndiyo, ila si kipili pili yaani zile za kujiviriga viriga na kuwa 'tim tim'. Nikichana zinachanika fresh na zinakuwa level safi tu, shida ni rangi yake nyekundu. Daaah! Yaani naandika huku nacheka na sijui kwa nini!

Simply tu nimegundua warembo wanaangalia mno nywele, na ndiyo maana vijana wengi wa sasa wanawekeza sana kwenye mitindo ya nywele na rangi. Siku hizi hakuna kitu kinachouzika madukani kama super blacks, zamani ilikuwa wateja ni wazee, ila nowadays ni vijana wenzetu ndiyo wateja.

Anyway nimejikubali na kuikubali hali yangu ya nywele, nimekataa kutumia super blacks na taka taka nyingine.

Kutokana na mazingira niliyokutana nao hawa mabinti, ilikuwa si rahisi kunijua kwa ukaribu hivyo hawakujua kuwa nina tuchenji, walianza kunihukumu kwa rangi ya nywele.

NB: Nimekubali yaishe ila nywele kupaka black ni big no. Najikubali, kwanza ukiwa mweupe na ukawa na nywele za kizungu (nyekundu) ni bonge la mvuto, mradi tu ziwe safi.

Ila kwa nyie weusi halafu mkawa na nywele nyekundu kwa kweli ni kituko mno (samahanini kwa kusema hili). Siku hizi kuna rate ya watu wengi weusi kuwa na nywele nyekundu, huo ni uchafu, ni kituko.

I think ukiwa mweusi na ukawa na nywele nyekundu super black itakufaa sana. Unlike kwa mtu mweupe kama mimi.

Mwenye kujua dawa tiririka weusi wapone.
Yaani unatongoza wasichana huko kanisani umewakosa?
 
hamna namna zaidi ya kujikubali mkuu.... unaeza nyoa para na usipendeze

fatilia matunzo ya nywele za aina yako uwe unaziweka vizuri....
Para ndiyo kabisaaa nitatisha[emoji38] hapa ni mwendo wa matunzo tu. Ila rangi itabaki tu nyekundu hivi hivi, kikubwa sina mba wala ukurutu na uchafu mwingine kichwani.

Anyway napambana
 
Back
Top Bottom