Ndugu zangu wanachadema, naomba tuache kuwa na ulevi wa ushindi wa uchaguzi hasa kwa timu Lisu, sis raia tulitarajia baada ya uchaguzi chadema ingebaki kitu kimoja, lakini kwa bahati mbaya naona jambo hili limekuwa gumu na hasa kwa Viongozi kulitengenezea utaratibu ili wanachama kubaki wamoja. Nitaongelea maswala kadhaa ili kuleta uelewa msingi wa kinachoendelea:
- Naomba ifahamike kwamba kuongoza chama kikubwa kama Chadema siyo jambo jepesi kama watu wengi wanavyodhani , hivyo wale wanaozalisha hila na tuhuma kuhusu m/kiti wa zamani nashauri waache, kwani wanayofanya sasa hivi hawamsaidii TAL wala timu yake.
- Toka wakati wa kampeni tulishuhudia nguvu kubwa ya kampeni ya Timu Lisu ambapo hata walikuwa wakitishia kujitoa kwanye Chama iwapo Mh TAL hatoshinda na kwamba ilianza kutengeneza hila kuwa Mh Mbowe angelazimisha ushindi wa mizengwe dhidi ya mshindani wake. (Kumbe TImu Lisu walikuja kwenye uchaguzi kwaajili ya ushindi wa mtu na siyo chama.)
- Ushindi wa Mh Lisu dhidi ya Mh Mbowe ulikuwa na margin ndogo sana, na ukizingatia style ya kampain iliyotumika wakati uchaguzi haikuwa ya kistaarabu (yaani ililenga kukipasua chama), hivyo Mh TAL alitakiwa baada tu ya kutangazwa mshindi awe muangalifu sana kwenye kauli anazotoa ten kwani kama M/kiti mpya angeonyesha kama anamuhitaji kila mmoja hata wale ambao hawajamchagua kwaajili ya mstakabali mwema wa chama kitu ambacho, yeye na wapambe wake walitumia muda huo vibaya kwa kujipongeza as if walikuwa wanashindana dhidi CCM.
- Nitoe angalizo kuna wafuasi wa TAL and Heche ambao wengine wala siyo wanachama na waliyo wanachama ni wing ya Vijana, ambao unaona wapo tayari kuendeleza ile vita ya wakati wa kampeni hadi sasa hivi ambapo kimsingi kwa kujua au kutokujua inapelekea chama kukosa nguvu ya ushawishi.
- CCM na vyombo vyake wameanza kuwatest kwa tukio lile la Mwanza la kutekwa kwa kiongozi na watu wasiojulikana, ukilinganisha na namna mlivyokuwa mnaonyesha uchungu wakati wa kampeni na Mbowe kuwa ameshindwa usubutu wa kufanya jambo , naona majibu wameshayapata kuwa hata hii timu mpya hawana kitu kipya juu ya kupambana na upoteaji wa watu hivyo kuna uwezekano haya mabo yakaendelea
- Jambo la jingine ni kwamba, mwaka jana Mh. Lisu na Timu yake walitumia muda mwingi sana kukipasua chama na kutengeneza mazingira kuwa Mh Mbowe amepoteza ushawishi , kumbe wao ndiyo waliyokuwa hawampi ushirikiano (hujumu) m/k wa zamani ili kufanikisha agenda yao ya kiuchaguzi. sasa siyo muda wa kulialia na Mbowe tena jengeni chama na kama kuna watu mnahisi mmewatendea sivyo basi tafuta watu wenye busara ili kuyamaliza (Inawezekana wewe ndiyo unawhitaji zaidi kuliko waowanavyokuhitaji(Kule CCM watu huwa wanajishusha kwaajili ya maslahi yaoya kiuchumi na nafasi za kisiasa))
- Na jambo la mwisho n1 kwamba. Mh Mbowe ana hadhi yake ndani ya Chadema na nje ya chama hata kama yupo pembeni, japo tupo katika zama za Demokrasia lakini siyo kila mtu ndani chama anaweza weza kumbagaza na kumtungiatungia tuhuma kama hao mahasimu wanavyotaka, kwani kwa kufanya hivyo wanakiumiza chama na si vinevyo.
- Na mwisho kabisa kama haya yote yanafanyika kwa makusidi ili kurecruit wanacham wapya that well and good lakini chama kitachukua muda mrefu kurudi kwenye peak