Nimesoma toka kwenye blog inaitwa Wanawakenisisi mama aliyekaa kwenye ndoa yake zaidi ya miaka 20 akizungumzia siri ya mafanikio yao, moja ikiwa kupeana break kwenye suala la sex. Nadhani ina make sense; kila siku kila siku si mtachokana jamani. Someni wenyewe msiseme NK nimetunga:
[h=2]Sunday, April 15, 2012[/h][h=3]
From One Woman - To Another....[/h]
"Mimi ni mwanamke niliyeolewa, nina watoto wawili na na nipo ndani ya ndoa miaka 20 sasa hivi. Hua inaniuma sana sana kuona jinsi ndoa za siku hizi hazidumu. Yaani watu munatuchangisha, baada ya miezi miwili ndoa ishasambaratika! Je, kosa ni la nani? Mimi kama mimi ningependa kuelezea machache lakini muhimu yaliyoniwezesha kufika hapa..
La kwanza na la muhimu - Sigusi kamwe kamwe simu ya mume wangu! Staki presha.. Yaani hata kama kalewa kalala na simu yake inaita au imeingia sms naigeuza naiweka chini ya mto wake, nalala zangu.
Pili, sometimes kama mwanamke inabidi ua manipulative kidogo. Hua namruhusu mume wangu kwenda out na washkaji zake at least mara moja kila wiki. Ila nikiona inakua too much na anarudi late sana, hua namuagiza vitu tofauti aniletee. Mfano - mishkaki ya nundu (hii lazma iliwe ikiwa ya moto), ice cream na vitu ambavyo akishanunua lazima aviwahishe nyumbani visije haribika.. Akishafika nyumbani hatoweza tena kutoka.
Tatu - At least mara moja kwa mwezi tunakwenda oout for a date, mie na mume wangu tu. Tunakwenda for dinner tukimaliza tunakwenda dancing kidogo kwenye live band. Inakua nakumbukia wakatui uuulleee alipokua ananitongoza. It's a great feeling.
Nne - Sio kua napata kipato kikubwa sanaaa but mie na my mume tulifungua account ya malengo. Hii tunakua tunaingiza hela tu, hatutoi kamwe. Hela hizi hutuwezesha sisi kwenda vacation na family yetu mara moja kila mwaka. Hua tunachagua sehemu ya kwenda kulingana na amount ya hela iliyopo kwenye account hiyo kwa wakati huo.
Tano -
Kuna wakati tuna abstain kufamya tendo la ndoa kwa muda. Inaweza ikawa mwezi mmoja hadi mitatu. Hii inasaidia kuongea ladha ya mapenzi wakati tunaporudi katika maisha ya kawaida.
Sita - Hua namnunulia vijizawadi vidogo vidogo. Naweza nikamnunulia cuff links, socks, viatu, tai, after shave, vest, mara simu, au laptop.. This way anajua kua namuwaza kila wakati.
Saba - Family time - hii hua tunafanya kila jumapili. Tunaweza kuamua tukampa dada off siku hiyo. Sisi kama family tutafagia, kufua, kupika - kisha tutakaa pamoja na kula na baada ya hapo tukakaa nje kwenye garden na kupiga story with drinks. Mara nyingine tunakwenda Bagamoyo au Kigamboni na kufurahi tu na family. Kuna namna nyingi to spend time na family. Hua nazibadilisha badilisha ili wasiboreke.
Anyway haya ni machache tu...
Nakutakia siku njema.."
Mrs K