Atukuzwaye
Senior Member
- Oct 5, 2026
- 191
- 250
Mwezi Novemba tuliokuwa tukiusubiri hatimaye umefika. Macho na masikio ya Watanzania wengi sasa yanaelekezwa Novemba 6, 2026, siku ambayo Mahakama Kuu ya Tanzania inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Antipas Lissu.
Kesi hiyo iliyochukua takribani mwaka mmoja imefikia hatua ya mwisho baada ya upande wa mashtaka na utetezi kukamilisha hoja zao za mwisho mbele ya jopo la majaji watatu.
Upande wa mashtaka umesisitiza kuwa umeweza kuthibitisha shtaka dhidi ya Lissu, huku upande wa utetezi ukipinga madai hayo na kueleza kuwa ushahidi uliowasilishwa haujathibitisha kosa linalomkabili.
Sasa, baada ya kusikiliza pande zote mbili, jukumu limebaki kwa Mahakama kutoa uamuzi wake.
Hukumu hii inatajwa kuwa miongoni mwa maamuzi muhimu yanayofuatiliwa kwa karibu katika historia ya siasa na mfumo wa haki nchini Tanzania.
Je, una matarajio gani kuhusu hukumu hii? Na kwa mtazamo wako, uamuzi wa Mahakama unaweza kuwa na athari gani katika mustakabali wa siasa za Tanzania.