Mwigizaji mashuhuri wa filamu nchini Rwanda, Micky, ametangaza rasmi kuwa amewasilisha malalamiko ya kisheria katika Bodi ya Upelelezi ya Rwanda (RIB), akituhumu kikundi cha watu kwa kuvuka mipaka na kushambulia familia yake.
Kupitia barua rasmi aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Micky ameeleza kuwa hakuwa na nia ya kufanya mtu yeyote afungwe, lakini amelazimika kuvunja ukimya baada ya vitendo hivyo vya unyanyasaji kuendelea kushamiri kwa muda mrefu.
"Kuanzia mwaka wa 2024 hadi sasa mwaka wa 2026, nimekuwa nikijitahidi kuwa mvumilivu na kuepuka kumuingiza mtu yeyote kwenye matatizo. Sijawahi kutamani kuona mtu anafungwa au maisha yake yanaharibika kwa sababu ya mzozo uliopo kati yetu," alisema Micky katika taarifa yake.
Mwigizaji huyo aliongeza kuwa ni jambo la kawaida kwa watu kutofautiana, kukasirikiana, au hata kuacha kupendana, na kwamba amekuwa akiheshimu hilo. Hata hivyo, alisisitiza kuwa migogoro ya watu wazima haipaswi kuvuka mipaka na kuingiza watoto, familia, au kuhatarisha usalama na maisha binafsi ya mtu.
Licha ya kutoa ufafanuzi huo wa kina, Micky hakutaja wazi majina ya watu au mtu mahususi aliyemfungulia mashtaka hayo. Swala hili limeibua mijadala mikubwa huku mashabiki na umma wakisubiri hatua zitakazochukuliwa na vyombo vya sheria.