Pre GE2025 Mwigulu aahidi kuwahudumia watoto wawili wa aliyekuwa Mtumishi wa TRA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ameahidi kuwahudumia kimahitaji watoto wawili wa marehemu, Amani Kamguna Simbayao, aliyekuwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Mifupa Muhimbili-Moi- Dar es salaam, aliyefariki dunia kwa kushambuliwa na watu katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, tarehe 6 Disemba, 2024.
View attachment 3172635
Dkt. Nchemba ametoa ahadi hiyo wakati akiongoza waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu katika Viwanja vya Michezo vya TRA, Kurasini Jijini Dar es Salaam.

View attachment 3172637Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba. Amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maanry Mwamba, ambaye aliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Elijah Mwandumbya, katika tukio hilo, na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Yusuf Juma Mwenda, kuhakikisha kuwa kiasi cha shilingi milioni 200 kinatafutwa kwa ajili ya kuanzisha Mfuko Maalum utakao tumika kuwanunulia watoto hao (Najimu Amani Sumbayao (8) na Badria Amani Simbayao (3), pamoja na mama yao, Bi. Arafat Abdalla Ukomo, Hati Fungani za Benki Kuu ya Tanzania, kwa ajili ya uhakika wa kupata huduma stahiki kama vile elimu na mambo mengine.
View attachment 3172638
Maelekezo hayo yanafuatia maombi yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, wakati alitoa salam za Mkoa wake, ambapo alipendekeza uwepo mpango mahsusi wa kuisaidia familia hiyo kimaisha ili iwe motisha kwa familia hiyo iliyopoteza shujaa aliyemwaga damu yake wakati akilitumikia Taifa.
View attachment 3172640
Marehemu Amani Simbayao, alikuwa Afisa Usafirishaji (dereva) wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, ambaye alipigwa na kuumizwa vibaya na watu akiwa kazini na wafanyakazi wenzake wengine wawili katika eneo la Tegeta Kwa Ndevu, Jijini Dar es Salaam. wakati walipokuwa wakilifuatilia gari moja lililokuwa linashukiwa kukiuka masuala ya kiforodha.

Katika tukio hilo la kuuaga mwili wa marehemu, Mhe. Dkt. Nchemba, alilaani vikali tukio hilo la watu kujichukulia Sheria mkononi na kumuua Mtumishi asiye na hatia hata baada ya kujitambulisha kuwa ni Mtumishi wa TRA, na ametoa wito kwa vyombo vya dola kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika na tukio hilo baya ili liwe fundisho Kwa watu wengine.

Pia, Soma:
TRA inatangaza kifo cha mtumishi wao, Amani Simbayao kilichotokea leo 06/12/2024
Jeshi la Polisi linawashikilia watu 4 kwa tuhuma za mauji ya Mtumishi wa TRA Amani Simbayao kutoka tukio la Tegeta

Mwigulu kuongoza waombolezaji kumuaga ofisa wa TRA, Aman Simbayao aliyeuawa kwa kushambuliwa
Maneno ya kisiasa.. MWIGULU NCHEMBA yupogo busy mpaka kwa nduguze sembuse kuwa hudumi hao watoto.

MWIGULU NCHEMBA yupogo very busy labda asumbuliwe na kukumbushwa kumbushwa sanaa

Ni Jambo la muda TU.
 
Msijifanye kifo Cha huyu kinawauma sana.
Msijifanye kusahau familia za wanao tekwa, kuteswa na kuuawa nazo Zina maumivu ya ndugu zao.
Hata mkiwa miungu watu zamu yenu inakuja.
Alisikia mlevi mmoja
Ma CCM huyajui hilo li mugulu limeona jamaa kaacha pisi kali linasingizia watoto. Kwani ndugu hawapo hadi yeye akachukue majukumu yasiyo mhusu?
 
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ameahidi kuwahudumia kimahitaji watoto wawili wa marehemu, Amani Kamguna Simbayao, aliyekuwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Mifupa Muhimbili-Moi- Dar es salaam, aliyefariki dunia kwa kushambuliwa na watu katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, tarehe 6 Disemba, 2024.
View attachment 3172635
Dkt. Nchemba ametoa ahadi hiyo wakati akiongoza waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu katika Viwanja vya Michezo vya TRA, Kurasini Jijini Dar es Salaam.

View attachment 3172637Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba. Amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maanry Mwamba, ambaye aliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Elijah Mwandumbya, katika tukio hilo, na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Yusuf Juma Mwenda, kuhakikisha kuwa kiasi cha shilingi milioni 200 kinatafutwa kwa ajili ya kuanzisha Mfuko Maalum utakao tumika kuwanunulia watoto hao (Najimu Amani Sumbayao (8) na Badria Amani Simbayao (3), pamoja na mama yao, Bi. Arafat Abdalla Ukomo, Hati Fungani za Benki Kuu ya Tanzania, kwa ajili ya uhakika wa kupata huduma stahiki kama vile elimu na mambo mengine.
View attachment 3172638
Maelekezo hayo yanafuatia maombi yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, wakati alitoa salam za Mkoa wake, ambapo alipendekeza uwepo mpango mahsusi wa kuisaidia familia hiyo kimaisha ili iwe motisha kwa familia hiyo iliyopoteza shujaa aliyemwaga damu yake wakati akilitumikia Taifa.
View attachment 3172640
Marehemu Amani Simbayao, alikuwa Afisa Usafirishaji (dereva) wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, ambaye alipigwa na kuumizwa vibaya na watu akiwa kazini na wafanyakazi wenzake wengine wawili katika eneo la Tegeta Kwa Ndevu, Jijini Dar es Salaam. wakati walipokuwa wakilifuatilia gari moja lililokuwa linashukiwa kukiuka masuala ya kiforodha.

Katika tukio hilo la kuuaga mwili wa marehemu, Mhe. Dkt. Nchemba, alilaani vikali tukio hilo la watu kujichukulia Sheria mkononi na kumuua Mtumishi asiye na hatia hata baada ya kujitambulisha kuwa ni Mtumishi wa TRA, na ametoa wito kwa vyombo vya dola kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika na tukio hilo baya ili liwe fundisho Kwa watu wengine.

Pia, Soma:

Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

TRA inatangaza kifo cha mtumishi wao, Amani Simbayao kilichotokea leo 06/12/2024

Jeshi la Polisi linawashikilia watu 4 kwa tuhuma za mauji ya Mtumishi wa TRA Amani Simbayao kutoka tukio la Tegeta

Mwigulu kuongoza waombolezaji kumuaga ofisa wa TRA, Aman Simbayao aliyeuawa kwa kushambuliwa
Anawahudumia kwa fedha zake binafsi au kwa Kodi za Watanzania? Watoto wa Marehemu Ali Kibao wanahudumiwa na nani?
 
#HABARI: Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameahidi kuwahudumia kimahitaji watoto wawili wa marehemu, Amani Kamguna Simbayao, aliyekuwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Mifupa Muhimbili-Moi-Dar es Salaam, aliyefariki dunia kwa kushambuliwa na watu katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, tarehe 6 Disemba, 2024.

Dkt. Nchemba ametoa ahadi hiyo wakati akiongoza waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu katika Viwanja vya Michezo vya TRA, Kurasini jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maanry Mwamba, ambaye aliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Elijah Mwandumbya, katika tukio hilo, na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Yusuf Juma Mwenda, kuhakikisha kuwa kiasi cha shilingi milioni 200 kinatafutwa kwa ajili ya kuanzisha Mfuko Maalum utakaotumika kuwanunulia watoto hao (Najimu Amani Sumbayao (8) na Badria Amani Simbayao (3), pamoja na mama yao, Bi. Arafat Abdalla Ukomo, Hati Fungani za Benki Kuu ya Tanzania, kwa ajili ya uhakika wa kupata huduma stahiki kama vile elimu na mambo mengine.

Maelekezo hayo yanafuatia maombi yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, wakati akitoa salamu za Mkoa wake, ambapo alipendekeza uwepo mpango mahsusi wa kuisaidia familia hiyo kimaisha ili iwe motisha kwa familia hiyo iliyopoteza shujaa aliyemwaga damu yake wakati akilitumikia Taifa.

Marehemu Amani Simbayao, alikuwa Afisa Usafirishaji (dereva) wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, ambaye alipigwa na kuumizwa vibaya na watu akiwa kazini na wafanyakazi wenzake wengine wawili katika eneo la Tegeta Kwa Ndevu, Jijini Dar es Salaam wakati walipokuwa wakilifuatilia gari moja lililokuwa linashukiwa kukiuka masuala ya kiforodha.
 
Skitumbiliwa itakua je na wenyewe wataishia hapo? Kwanini asiwaingize kwenye mfumo wa TRA ndo igharamikie masomo na malezi kuajumla, wanasiasa wetu wsfikie mahara waache cheap politics
 
Wale wahanga waliofariki kwenye ajali ya kuporomokewa na ghorofa kule kariakoo ambazo kimsingi ni walipa Kodi na ni wadau wa tra na kiuhalisia wameacha watoto na familia zao Mwigulu na chalamila walichukua hatua Kama hizo?
Kama hawajafanya hivyo, tusemeje basi, zaidi ya kuuita ubaguzi uliopita viwango?
 
Back
Top Bottom