ndolelejiUduhe
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,837
- 3,027
Atazawadiwa na Mungu kitakachomfaaWazo la TOZO lilimpaisha Zungu mpaka akawa Naibu Spika.
Watu wa Ilala ndio wa kulaumiwa maana huyu ndiye mbunge waliomchagua wao
😳😳
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Atazawadiwa na Mungu kitakachomfaaWazo la TOZO lilimpaisha Zungu mpaka akawa Naibu Spika.
Watu wa Ilala ndio wa kulaumiwa maana huyu ndiye mbunge waliomchagua wao
Tozo ni ushauri na matakwa ya wananchi, wameyapokea na kuyafanyia kazi. Tunapigwa tozo kweli kweli. Tuseme sawa serikali yetu ni sikivu na inafanyia kazi maoni na matakwa ya wananchi.
Vipi kuhusu kikokotoo?? Je, wananchi pia wanakitaka?? Je siku zote wamekua wakiwasifia kuwa nacho ni kizuri?? Hamsikii kelele za watumishi juu ya kikokotoo?? Mwigulu acha kulisha wananchi maneno, kumbuka kuna kuulizwa kesho kuhusu uchunga wako mbele ya Mola wako.
Hili kundi la.mchwa linatakiwa kupumzishwa haraka sana kuanzia October na kumalizana nao mwakani!! Wametuchoka sana.Kweli sisi wananchi wajinga kama alivyosema kiongozi wa upinzani yaani tumependekeza tozo wenyewe
Halafu tuje tulalamike huu ni ujinga kwekikweli!
Waziri atuambie wananchi wangapi walipendekeza Kati ya wangapi unaweza kuta wananchi wenyewe ni mawaziri na wafuasi tu.
Mambo ya wote tuwe wote, tozo iliyopendekezwa bungeni ni za simu wa siyo za kibenki
sawa lakini hii nchi tumechelewa sana kimaendeleo sasa sijui kulinganisha na nani
Wananchi wa wapi waliokubali hili?Waziri wa Fedha Mh Mwigulu akizungumza na Waandishi wa habari amesema kwamba Wananchi wenyewe ndio walioshauri serikali iweke Tozo ili kupanua wigo wa mapato , na kwamba ilichofanya serikali ni kuufanyia kazi ushauri wa Wananchi.
---
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema wananchi ndio walioshauri Serikali ipanue wigo wa tozo za miamala kwa kujumuisha miamala yote ya kielektroniki, ili wananchi wote wachangie maendeleo. Ameeleza kuwa awali miamala iliyokuwa ikitozwa ni iliyokuwa ikifanyika kwa simu pekee.
Chanzo: SwahiliTimes
Hayo maoni ya wananchi waliyakusanya lini na kwa njia gani?
Aache uongo, hizo tozo zimepitishwa na lile bunge la CCM lisiloweza kuihoji chochote serikali kisha Rais akaweka saini.
Naibu spika Zungu ndiye aliyekuja na hii idea.Waziri wa Fedha Mh Mwigulu akizungumza na Waandishi wa habari amesema kwamba Wananchi wenyewe ndio walioshauri serikali iweke Tozo ili kupanua wigo wa mapato , na kwamba ilichofanya serikali ni kuufanyia kazi ushauri wa Wananchi.