Mwigulu ajikanyaga Bungeni kuhusu kodi ya Tsh. Trilioni 360 za Makinikia ya Dhahabu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826

Sakata la Makinikia limetinga bungeni baada ya Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhoji kwa nini Serikali ilikubali kupokea Tsh. Bilioni 700 zilizotokana na kesi za malimbikizo ya madeni ya Makinikia badala ya Tsh. Trilioni 360 ambayo ni madai halali kwa Tanzania.

Mpina amehoji swali hilo la nyonge za katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni leo Alhamis, Septemba 22,2022. “Kwa nini Serikali ilikubali kupokea Tsh. Bilioni 700 kutoka katika kesi za malimbikizo ya madeni maarufu kama makinikia badala ya Tsh. Trilioni 360 ambayo ni madai halali katika nchi yetu,”amehoji.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali haijakubali kupokea fedha hizo (Sh700 bilioni) na kuacha Sh360 trilioni, isipokuwa ilipeleka malalamiko kuhusu kampuni za madini. Hata hivyo, kabla ya kumaliza kulijibu swali hilo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alimkatisha na kutaka ufafanuzi wa majibu ya Serikali yaliyotofautiana na swali la msingi lililoulizwa na Mpina.

Akijibu swali hilo, Waziri Mwigulu amesema Serikali haikupokea kimya kimya fedha hizo (Sh700 bilioni) na kuacha Sh360 trilioni bali kilichofanyika ni kwa Serikali kupeleka malalamiko kwenye kampuni za madini. Lakini kabla ya kuendelea kujibu, alikatishwa tena na Dk Tulia akimtaka kwenda kwa mtiririko huku akimtaka Waziri huyo kueleza juu ya tofauti ya fedha zilizoandikwa katika jibu la Serikali na zilizotamkwa na mbunge ili aweze kutoa mwongozo.

Akitoa ufafanuzi, DK Mwigulu amesema Sh360 trilioni anazozungumzia Mpina ni za makinikia wakati katika jibu la swali la msingi, kiasi kinachozungumziwa cha Sh4.21 trilioni ni za mashauri mengine ya kodi. Baada ya maelezo hayo, Dk Tulia aliitaka Serikali kumjibu Mpina tena kwa kadri alivyouliza swali lake la msingi.

Akijibu swali hilo, Dk Mwigulu amesema Sh360 trilioni haipo kwenye Bodi ya Rufani ya Kodi (TRAB) wala Baraza la Usuluhishi la Mapato ya Kodi (TRAT).

Amesema rufaa za kikodi ni mahususi na lilikuwepo kwenye mzozo wa Serikali na Kampuni ya Barick kwahiyo ni kitu tofauti. Katika swali la msingi, Mpina amehoji nini kinachosababisha kesi 1,097 za kodi za muda mrefu zenye thamani ya Sh360 trilioni na Dola za Marekani milioni 181.4 kutoamuliwa hadi sasa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande amesema hadi Agosti 2022, kulikuwa na idadi ya mashauri 854 kwenye hatua mbalimbali za usikilizaji, yenye kodi inayobishaniwa ya jumla ya Sh4.21 trilioni na Dola za Marekani Milioni 3.48 katika taasisi za rufani za kodi ambazo ni TRAB na TRAT.

Amesema hivyo, kwa sasa TRAB na TRAT zinaendelea kusikiliza mashauri hayo pamoja na mashauri mapya yanayoendelea kusajiliwa. Aidha, amesema kwa nyakati tofauti, idadi ya mashauri ya kodi hupungua au kuongezeka kulingana na kasi ya usikilizaji na usajili.
 
..kwa hili wanamuonea Mwigulu.

..pia Luhaga Mpina alikuwepo ktk cabinet wakati serikali ya Magufuli ilipoamua "kuwasamehe" barrick / acacia deni la usd 191 billion.

..wenye majibu ya swali la Luhaga Mpina ni John Pombe Magufuli ambaye amefariki, na Palamagamba Kabudi ambaye bado yuko bungeni.
 
Sakata la Makinikia limetinga bungeni baada ya Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhoji kwa nini Serikali ilikubali kupokea Tsh. Bilioni 700 zilizotokana na kesi za malimbikizo ya madeni ya Makinikia badala ya Tsh. Trilioni 360 ambayo ni madai halali kwa Tanzania.

Mpina amehoji swali hilo la nyonge za katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni leo Alhamis, Septemba 22,2022.

“Kwa nini Serikali ilikubali kupokea Tsh. Bilioni 700 kutoka katika kesi za malimbikizo ya madeni maarufu kama makinikia badala ya Tsh. Trilioni 360 ambayo ni madai halali katika nchi yetu,”amehoji.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali haijakubali kupokea fedha hizo (Sh700 bilioni) na kuacha Sh360 trilioni, isipokuwa ilipeleka malalamiko kuhusu kampuni za madini.

Hata hivyo, kabla ya kumaliza kulijibu swali hilo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alimkatisha na kutaka ufafanuzi wa majibu ya Serikali yaliyotofautiana na swali la msingi lililoulizwa na Mpina.

Akijibu swali hilo, Waziri Mwigulu amesema Serikali haikupokea kimya kimya fedha hizo (Sh700 bilioni) na kuacha Sh360 trilioni bali kilichofanyika ni kwa Serikali kupeleka malalamiko kwenye kampuni za madini.

Lakini kabla ya kuendelea kujibu, alikatishwa tena na Dk Tulia akimtaka kwenda kwa mtiririko huku akimtaka Waziri huyo kueleza juu ya tofauti ya fedha zilizoandikwa katika jibu la Serikali na zilizotamkwa na mbunge ili aweze kutoa mwongozo.

Akitoa ufafanuzi, DK Mwigulu amesema Sh360 trilioni anazozungumzia Mpina ni za makinikia wakati katika jibu la swali la msingi, kiasi kinachozungumziwa cha Sh4.21 trilioni ni za mashauri mengine ya kodi.

Baada ya maelezo hayo, Dk Tulia aliitaka Serikali kumjibu Mpina tena kwa kadri alivyouliza swali lake la msingi.

Akijibu swali hilo, Dk Mwigulu amesema Sh360 trilioni haipo kwenye Bodi ya Rufani ya Kodi (TRAB) wala Baraza la Usuluhishi la Mapato ya Kodi (TRAT).

Amesema rufaa za kikodi ni mahususi na lilikuwepo kwenye mzozo wa Serikali na Kampuni ya Barick kwahiyo ni kitu tofauti.

Katika swali la msingi, Mpina amehoji nini kinachosababisha kesi 1,097 za kodi za muda mrefu zenye thamani ya Sh360 trilioni na Dola za Marekani milioni 181.4 kutoamuliwa hadi sasa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande amesema

hadi Agosti 2022, kulikuwa na idadi ya mashauri 854 kwenye hatua mbalimbali za usikilizaji, yenye kodi inayobishaniwa ya jumla ya Sh4.21 trilioni na Dola za Marekani Milioni 3.48 katika taasisi za rufani za kodi ambazo ni TRAB na TRAT.

Amesema hivyo, kwa sasa TRAB na TRAT zinaendelea kusikiliza mashauri hayo pamoja na mashauri mapya yanayoendelea kusajiliwa.

Aidha, amesema kwa nyakati tofauti, idadi ya mashauri ya kodi hupungua au kuongezeka kulingana na kasi ya usikilizaji na usajili.
Lissu aliwahi kusema ripoti ya makinikia ni "Professional Rubbish",akaishia kupigwa risasi
 
Kwahiyo hiyo bil 700 ni ujinga katika kipande kipi cha makinikia, upande wa Lissu au serkali ya awamu 6. Na wajinga waliolipa hiyo 700bil walikuwa wanafanya ujinga kwa wajinga gani?

..Magufuli na Kabudi walitusaliti.

..baada ya CEO wa Barrick kukanyaga IKULU, madai ya usd 191 billion yaliachwa, tukaanza kusikia habari za kishika uchumba cha usd 300 million.

..Na hata hicho kishika uchumba hatukulipwa chote kwa mara moja, tulilipwa kidogo kidogo na haijulikani kama wamemaliza.
 
Sakata la Makinikia limetinga bungeni baada ya Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhoji kwa nini Serikali ilikubali kupokea Tsh. Bilioni 700 zilizotokana na kesi za malimbikizo ya madeni ya Makinikia badala ya Tsh. Trilioni 360 ambayo ni madai halali kwa Tanzania.

Mpina amehoji swali hilo la nyonge za katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni leo Alhamis, Septemba 22,2022.

“Kwa nini Serikali ilikubali kupokea Tsh. Bilioni 700 kutoka katika kesi za malimbikizo ya madeni maarufu kama makinikia badala ya Tsh. Trilioni 360 ambayo ni madai halali katika nchi yetu,”amehoji.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali haijakubali kupokea fedha hizo (Sh700 bilioni) na kuacha Sh360 trilioni, isipokuwa ilipeleka malalamiko kuhusu kampuni za madini.

Hata hivyo, kabla ya kumaliza kulijibu swali hilo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alimkatisha na kutaka ufafanuzi wa majibu ya Serikali yaliyotofautiana na swali la msingi lililoulizwa na Mpina.

Akijibu swali hilo, Waziri Mwigulu amesema Serikali haikupokea kimya kimya fedha hizo (Sh700 bilioni) na kuacha Sh360 trilioni bali kilichofanyika ni kwa Serikali kupeleka malalamiko kwenye kampuni za madini.

Lakini kabla ya kuendelea kujibu, alikatishwa tena na Dk Tulia akimtaka kwenda kwa mtiririko huku akimtaka Waziri huyo kueleza juu ya tofauti ya fedha zilizoandikwa katika jibu la Serikali na zilizotamkwa na mbunge ili aweze kutoa mwongozo.

Akitoa ufafanuzi, DK Mwigulu amesema Sh360 trilioni anazozungumzia Mpina ni za makinikia wakati katika jibu la swali la msingi, kiasi kinachozungumziwa cha Sh4.21 trilioni ni za mashauri mengine ya kodi.

Baada ya maelezo hayo, Dk Tulia aliitaka Serikali kumjibu Mpina tena kwa kadri alivyouliza swali lake la msingi.

Akijibu swali hilo, Dk Mwigulu amesema Sh360 trilioni haipo kwenye Bodi ya Rufani ya Kodi (TRAB) wala Baraza la Usuluhishi la Mapato ya Kodi (TRAT).

Amesema rufaa za kikodi ni mahususi na lilikuwepo kwenye mzozo wa Serikali na Kampuni ya Barick kwahiyo ni kitu tofauti.

Katika swali la msingi, Mpina amehoji nini kinachosababisha kesi 1,097 za kodi za muda mrefu zenye thamani ya Sh360 trilioni na Dola za Marekani milioni 181.4 kutoamuliwa hadi sasa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande amesema

hadi Agosti 2022, kulikuwa na idadi ya mashauri 854 kwenye hatua mbalimbali za usikilizaji, yenye kodi inayobishaniwa ya jumla ya Sh4.21 trilioni na Dola za Marekani Milioni 3.48 katika taasisi za rufani za kodi ambazo ni TRAB na TRAT.

Amesema hivyo, kwa sasa TRAB na TRAT zinaendelea kusikiliza mashauri hayo pamoja na mashauri mapya yanayoendelea kusajiliwa.

Aidha, amesema kwa nyakati tofauti, idadi ya mashauri ya kodi hupungua au kuongezeka kulingana na kasi ya usikilizaji na usajili.
Hizo pesa hazipo zilikuwa ni hadithi za Jiwe na kundi lake la Sukuma gang..

Tzn iwe na Trilioni 360 izitoe wapi hasa?
 
TRAB = Tax Revenue Appeals Board
TRAT = Tax Revenue Appeals Tribunal
Angalau angeelezea maana yake kwanza ingemsaidia. Hapa kuna mijitu inaanza kumlaum Mwendezake kwa ujinga wa mtu mwingine. Uchache wa taarifa ni tatizo kubwa sana Board hupokea rufaa za kikodi ikiwa kunashauri ambalo mtu anaona sio... kwenye makadirio ya kodi aina zote zinazotozwa na mamlaka za kodi, ikiwa hataridhika na maamuzi ya board atakata rufaa TRAT. Ilianzishwa 2018 kwa mujibu wa sheria. Ukiconnect dot za Mwigulu maana yake utaipata.
 
Mimi nilijua trilioni 360 ilikuwa ni mbinu ya kupata Bilioni 700.

Huo mkakati ulikuwa mkali Sana, nawapongeza wore waliomshauri hayati hiyo mbinu.

Alikuza mgogoro ili tupate power ya kubargain.

Tukaishia kupata hayo mabilioni na ushiriki wetu katika kuendesha migodi.
 
Wengi wa Watanzania hasa wanaoitwa wapinzagiza, ni wajinga na mamburula,

Ni ujinga kusema 700b alizitoa Lisu Kutoka miga!

Jpm anapata kosa lipi hapo na wakati alipokohoa tu 700b zikaingia Kutoka huko Accasia!

Kwa hicho walichotoa, Accasia ni majizii au si majizi?

Mnataka na hiyo kesi ya 360t akaisimamie yeye?

Pumbavu zenu vilaza na wafoji vyeti!
 
Unajua 700B terms zake zilikuwaje au unaongelea tu final outcomes?

Wale jamaa hawakuwa so stupid kukubali ku-sign wakati walikuwa wana uwezo wa ku-trigger dispute mechanism London endapo terms zingekuwa unfavourable kwao, in long term kwendana na wachambuzi wa uchumi- Hakuna cha maana tulicho-gain.
 
Wengi wa Watanzania hasa wanaoitwa wapinzagiza, ni wajinga na mamburula,

Ni ujinga kusema 700b alizitoa Lisu Kutoka miga!

Jpm anapata kosa lipi hapo na wakati alipokohoa tu 700b zikaingia Kutoka huko Accasia!

Kwa hicho walichotoa, Accasia ni majizii au si majizi?

Mnataka na hiyo kesi ya 360t akaisimamie yeye?

Pumbavu zenu vilaza na wafoji vyeti!
Naona ume-raise issue ya 700B,

Hizo 700B serikali ilizipokea lini na wapi? Ili isije tukawa tunajenga hoja kwa fikra za kufikirika.
 
Back
Top Bottom