Mwigulu ajikanyaga Bungeni kuhusu kodi ya Tsh. Trilioni 360 za Makinikia ya Dhahabu

Mwigulu ajikanyaga Bungeni kuhusu kodi ya Tsh. Trilioni 360 za Makinikia ya Dhahabu

Nimpongeze Spika kwa namna alivyosimama kuhakikisha serikali, kupitia waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba, anatoa majibu ya kueleweka.

Mwigulu anaonekana hafahamu chochote kuhusu hayo madai, ndio maana anaulizwa habari ya trillion 360, yeye anazungumzia bilion 700, mpaka Spika akaona huyu waziri dishi limeyumba ila hakumwambia.
 
-Watendaji wa Hazina,wamsaidie Waziri na naibu Waziri kuandaa majibu yaliyo sahihi.
-Inasikitisha kuona majibu ya maswali hayaeleweki na shida inakuwa yanapoulizwa maswali ya nyongeza,naibu Waziri anapata shida sana kuyajibu.

Ushauri
-Waziri na naibu Waziri, Fedha na Mipango inabidi wapitie Sana nyaraka na taarifa mbalimbali zinazopelekwa bungeni,ili kumsaidia Mheshimiwa Rais SSH kufanya kazi yake kuwa nyepesi.
-Serikali ifikirie kuanzisha wizara ya Mipango na uwekezaji (Kuondoa Mipango)
-Wizara ya Fedha na Mipango iwe na Naibu Waziri Fedha na Naibu Waziri Mipango.
 
Wengi wa Watanzania hasa wanaoitwa wapinzagiza, ni wajinga na mamburula,

Ni ujinga kusema 700b alizitoa Lisu Kutoka miga!

Jpm anapata kosa lipi hapo na wakati alipokohoa tu 700b zikaingia Kutoka huko Accasia!

Kwa hicho walichotoa, Accasia ni majizii au si majizi?

Mnataka na hiyo kesi ya 360t akaisimamie yeye?

Pumbavu zenu vilaza na wafoji vyeti!
Kwa kifupi ripoti ya MAKINIKIA ilikuwa rubbish yaani takataka.

Baada ya kuwa Rais alitaka ku-prove kuwa ACACIA wanatuibia madini kupitia makinikia, ndipo akaunda tume ya Prof Mruma na Prof Osoro. Kiukweli Tume ya Prof Mruma ilikuta kuwa kontaina la 20ft lina 0.7Kg ya madini ya dhahabu na silver. Na kiasi hicho ndiyo kimekuwa kikilipiwa na ACACIA/ Barrick kodi sahihi kuanzia 1998.

Kwa vile Jiwe alidhani tunaibiwa madini wakati si kweli akaichakachua ripoti ya Prof Mruma na kuandika kuwa kuna 7.0 Kg kwa kila container. Hapa ndiyo ile hoja ya ACACIA kukwepa ushuru wa USD 190 bilioni au Tsh 450 Trillioni ndipo ilipojitokeza. Hiki kitu Tundu Lissu aliita professorial rubbish kwa kuwa ni uzandiki mtupu. Na kweli hatujapata hiyo Tsh 450 Trilion aka Noah moja kwa kila Mtanzania.

Lakini nchi yetu inaongoza kwà kuwa na wapumbavu wengi, maana
 
TRAB = Tax Revenue Appeals Board
TRAT = Tax Revenue Appeals Tribunal
Angalau angeelezea maana yake kwanza ingemsaidia. Hapa kuna mijitu inaanza kumlaum Mwendezake kwa ujinga wa mtu mwingine. Uchache wa taarifa ni tatizo kubwa sana Board hupokea rufaa za kikodi ikiwa kunashauri ambalo mtu anaona sio... kwenye makadirio ya kodi aina zote zinazotozwa na mamlaka za kodi, ikiwa hataridhika na maamuzi ya board atakata rufaa TRAT. Ilianzishwa 2018 kwa mujibu wa sheria. Ukiconnect dot za Mwigulu maana yake utaipata.
Kwa hiyo kama hao jamaa hawajapeleka malalamiko TRAB inamaana wamekubali inabidi wazilipe Mwigulu kachemsha kama alivuosema kwamba hazipo TRAB basi walipe
 
Sakata la Makinikia limetinga bungeni baada ya Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhoji kwa nini Serikali ilikubali kupokea Tsh. Bilioni 700 zilizotokana na kesi za malimbikizo ya madeni ya Makinikia badala ya Tsh. Trilioni 360 ambayo ni madai halali kwa Tanzania.

Mpina amehoji swali hilo la nyonge za katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni leo Alhamis, Septemba 22,2022.

“Kwa nini Serikali ilikubali kupokea Tsh. Bilioni 700 kutoka katika kesi za malimbikizo ya madeni maarufu kama makinikia badala ya Tsh. Trilioni 360 ambayo ni madai halali katika nchi yetu,”amehoji.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali haijakubali kupokea fedha hizo (Sh700 bilioni) na kuacha Sh360 trilioni, isipokuwa ilipeleka malalamiko kuhusu kampuni za madini.

Hata hivyo, kabla ya kumaliza kulijibu swali hilo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alimkatisha na kutaka ufafanuzi wa majibu ya Serikali yaliyotofautiana na swali la msingi lililoulizwa na Mpina.

Akijibu swali hilo, Waziri Mwigulu amesema Serikali haikupokea kimya kimya fedha hizo (Sh700 bilioni) na kuacha Sh360 trilioni bali kilichofanyika ni kwa Serikali kupeleka malalamiko kwenye kampuni za madini.

Lakini kabla ya kuendelea kujibu, alikatishwa tena na Dk Tulia akimtaka kwenda kwa mtiririko huku akimtaka Waziri huyo kueleza juu ya tofauti ya fedha zilizoandikwa katika jibu la Serikali na zilizotamkwa na mbunge ili aweze kutoa mwongozo.

Akitoa ufafanuzi, DK Mwigulu amesema Sh360 trilioni anazozungumzia Mpina ni za makinikia wakati katika jibu la swali la msingi, kiasi kinachozungumziwa cha Sh4.21 trilioni ni za mashauri mengine ya kodi.

Baada ya maelezo hayo, Dk Tulia aliitaka Serikali kumjibu Mpina tena kwa kadri alivyouliza swali lake la msingi.

Akijibu swali hilo, Dk Mwigulu amesema Sh360 trilioni haipo kwenye Bodi ya Rufani ya Kodi (TRAB) wala Baraza la Usuluhishi la Mapato ya Kodi (TRAT).

Amesema rufaa za kikodi ni mahususi na lilikuwepo kwenye mzozo wa Serikali na Kampuni ya Barick kwahiyo ni kitu tofauti.

Katika swali la msingi, Mpina amehoji nini kinachosababisha kesi 1,097 za kodi za muda mrefu zenye thamani ya Sh360 trilioni na Dola za Marekani milioni 181.4 kutoamuliwa hadi sasa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande amesema

hadi Agosti 2022, kulikuwa na idadi ya mashauri 854 kwenye hatua mbalimbali za usikilizaji, yenye kodi inayobishaniwa ya jumla ya Sh4.21 trilioni na Dola za Marekani Milioni 3.48 katika taasisi za rufani za kodi ambazo ni TRAB na TRAT.

Amesema hivyo, kwa sasa TRAB na TRAT zinaendelea kusikiliza mashauri hayo pamoja na mashauri mapya yanayoendelea kusajiliwa.

Aidha, amesema kwa nyakati tofauti, idadi ya mashauri ya kodi hupungua au kuongezeka kulingana na kasi ya usikilizaji na usajili.
Another Charles Kitwanga 😅😅😅
 
Kwa kifupi ripoti ya MAKINIKIA ilikuwa rubbish yaani takataka.

Baada ya kuwa Rais alitaka ku-prove kuwa ACACIA wanatuibia madini kupitia makinikia, ndipo akaunda tume ya Prof Mruma na Prof Osoro. Kiukweli Tume ya Prof Mruma ilikuta kuwa kontaina la 20ft lina 0.7Kg ya madini ya dhahabu na silver. Na kiasi hicho ndiyo kimekuwa kikilipiwa na ACACIA/ Barrick kodi sahihi kuanzia 1998.

Kwa vile Jiwe alidhani tunaibiwa madini wakati si kweli akaichakachua ripoti ya Prof Mruma na kuandika kuwa kuna 7.0 Kg kwa kila container. Hapa ndiyo ile hoja ya ACACIA kukwepa ushuru wa USD 190 bilioni au Tsh 450 Trillioni ndipo ilipojitokeza. Hiki kitu Tundu Lissu aliita professorial rubbish kwa kuwa ni uzandiki mtupu. Na kweli hatujapata hiyo Tsh 450 Trilion aka Noah moja kwa kila Mtanzania.

Lakini nchi yetu inaongoza kwà kuwa na wapumbavu wengi, maana
Tundu Lissu alishayaona haya tangu mwanzo.

Bravo TL
 
Wengi wa Watanzania hasa wanaoitwa wapinzagiza, ni wajinga na mamburula,

Ni ujinga kusema 700b alizitoa Lisu Kutoka miga!

Jpm anapata kosa lipi hapo na wakati alipokohoa tu 700b zikaingia Kutoka huko Accasia!

Kwa hicho walichotoa, Accasia ni majizii au si majizi?

Mnataka na hiyo kesi ya 360t akaisimamie yeye?

Pumbavu zenu vilaza na wafoji vyeti!
Professerial Rubiish

TL best Person of all time.

Alichosema kuhusu Mgogoro wa Barrick na Tz ndio kilichotokea na kinaendelea kuwatafuna.

Mwigulu amejaribu kuficha aibu ya Mwendazake ya Tril 360.

Swali la Mpina japo yeye mpina ni mnafiki lakini linaibua aibu kubwa kwa awamu ya tano.

Mwigulu akabaki kijikanyaga tu.
 
Zile b 700 Lisu alizitoa Miga?

Embu utuambie, Kama Accasia hawakuwa majizi, iweje watoe hizo pesa hata kama ni kidogo!

Acha uzuzu Dogo!
 
Kwa kifupi ripoti ya MAKINIKIA ilikuwa rubbish yaani takataka.

Baada ya kuwa Rais alitaka ku-prove kuwa ACACIA wanatuibia madini kupitia makinikia, ndipo akaunda tume ya Prof Mruma na Prof Osoro. Kiukweli Tume ya Prof Mruma ilikuta kuwa kontaina la 20ft lina 0.7Kg ya madini ya dhahabu na silver. Na kiasi hicho ndiyo kimekuwa kikilipiwa na ACACIA/ Barrick kodi sahihi kuanzia 1998.

Kwa vile Jiwe alidhani tunaibiwa madini wakati si kweli akaichakachua ripoti ya Prof Mruma na kuandika kuwa kuna 7.0 Kg kwa kila container. Hapa ndiyo ile hoja ya ACACIA kukwepa ushuru wa USD 190 bilioni au Tsh 450 Trillioni ndipo ilipojitokeza. Hiki kitu Tundu Lissu aliita professorial rubbish kwa kuwa ni uzandiki mtupu. Na kweli hatujapata hiyo Tsh 450 Trilion aka Noah moja kwa kila Mtanzania.

Lakini nchi yetu inaongoza kwà kuwa na wapumbavu wengi, maana
Acha utumwa wa kijinga mkuu! Ilikuwaje Accasia watoe hizo b 700?

Na unaposema ile ripot ilikuwa kinyume cha 7.0, unaushahidi upi wa hiki usemacho kwamba JPM aliichakachua?

Na ikiwa aliichakachua, basi ni vema pia, maana, Taifa lilinufaika na uchakachuzi ule hadi tukapata hizo 700b za kujenga vituo viwili vya afya, na hiyo sio Kwa faida Kwa mchakachuzi, Bali ni Kwa watoto wa kitanzania na watoto wako wakiwemo
 
Ina maana Mpina aliamini zile hadithi za marehemu? Zile zilikuwa ni story za kunogesha baraza kwa wasio na akili, wenye akili wote walijua kuwa ni uwongo.
Siyo kuamini... Kama ni uongo basi waje wazi ili tujue kuwa akina Propesa Ossoro walipresent Professorial Rubbish. Pia watu wawajibishwe kwa huo uongo.... Ili next time tusifanywe mazuzu tena.
 
Zile b 700 Lisu alizitoa Miga?

Embu utuambie, Kama Accasia hawakuwa majizi, iweje watoe hizo pesa hata kama ni kidogo!

Acha uzuzu Dogo!
Haya ngoja tuone kama Swali la Mbunge kuna mtu wa kumjibu.

Hizo bil 700 zenyewe ziko wapi?
 
Back
Top Bottom