Mwigulu ajikanyaga Bungeni kuhusu kodi ya Tsh. Trilioni 360 za Makinikia ya Dhahabu

Nimpongeze Spika kwa namna alivyosimama kuhakikisha serikali, kupitia waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba, anatoa majibu ya kueleweka.

Mwigulu anaonekana hafahamu chochote kuhusu hayo madai, ndio maana anaulizwa habari ya trillion 360, yeye anazungumzia bilion 700, mpaka Spika akaona huyu waziri dishi limeyumba ila hakumwambia.
 
-Watendaji wa Hazina,wamsaidie Waziri na naibu Waziri kuandaa majibu yaliyo sahihi.
-Inasikitisha kuona majibu ya maswali hayaeleweki na shida inakuwa yanapoulizwa maswali ya nyongeza,naibu Waziri anapata shida sana kuyajibu.

Ushauri
-Waziri na naibu Waziri, Fedha na Mipango inabidi wapitie Sana nyaraka na taarifa mbalimbali zinazopelekwa bungeni,ili kumsaidia Mheshimiwa Rais SSH kufanya kazi yake kuwa nyepesi.
-Serikali ifikirie kuanzisha wizara ya Mipango na uwekezaji (Kuondoa Mipango)
-Wizara ya Fedha na Mipango iwe na Naibu Waziri Fedha na Naibu Waziri Mipango.
 
Kwa kifupi ripoti ya MAKINIKIA ilikuwa rubbish yaani takataka.

Baada ya kuwa Rais alitaka ku-prove kuwa ACACIA wanatuibia madini kupitia makinikia, ndipo akaunda tume ya Prof Mruma na Prof Osoro. Kiukweli Tume ya Prof Mruma ilikuta kuwa kontaina la 20ft lina 0.7Kg ya madini ya dhahabu na silver. Na kiasi hicho ndiyo kimekuwa kikilipiwa na ACACIA/ Barrick kodi sahihi kuanzia 1998.

Kwa vile Jiwe alidhani tunaibiwa madini wakati si kweli akaichakachua ripoti ya Prof Mruma na kuandika kuwa kuna 7.0 Kg kwa kila container. Hapa ndiyo ile hoja ya ACACIA kukwepa ushuru wa USD 190 bilioni au Tsh 450 Trillioni ndipo ilipojitokeza. Hiki kitu Tundu Lissu aliita professorial rubbish kwa kuwa ni uzandiki mtupu. Na kweli hatujapata hiyo Tsh 450 Trilion aka Noah moja kwa kila Mtanzania.

Lakini nchi yetu inaongoza kwà kuwa na wapumbavu wengi, maana
 
Kwa hiyo kama hao jamaa hawajapeleka malalamiko TRAB inamaana wamekubali inabidi wazilipe Mwigulu kachemsha kama alivuosema kwamba hazipo TRAB basi walipe
 
Another Charles Kitwanga 😅😅😅
 
Tundu Lissu alishayaona haya tangu mwanzo.

Bravo TL
 
Professerial Rubiish

TL best Person of all time.

Alichosema kuhusu Mgogoro wa Barrick na Tz ndio kilichotokea na kinaendelea kuwatafuna.

Mwigulu amejaribu kuficha aibu ya Mwendazake ya Tril 360.

Swali la Mpina japo yeye mpina ni mnafiki lakini linaibua aibu kubwa kwa awamu ya tano.

Mwigulu akabaki kijikanyaga tu.
 
Zile b 700 Lisu alizitoa Miga?

Embu utuambie, Kama Accasia hawakuwa majizi, iweje watoe hizo pesa hata kama ni kidogo!

Acha uzuzu Dogo!
 
Acha utumwa wa kijinga mkuu! Ilikuwaje Accasia watoe hizo b 700?

Na unaposema ile ripot ilikuwa kinyume cha 7.0, unaushahidi upi wa hiki usemacho kwamba JPM aliichakachua?

Na ikiwa aliichakachua, basi ni vema pia, maana, Taifa lilinufaika na uchakachuzi ule hadi tukapata hizo 700b za kujenga vituo viwili vya afya, na hiyo sio Kwa faida Kwa mchakachuzi, Bali ni Kwa watoto wa kitanzania na watoto wako wakiwemo
 
Nyie watu kenge kweli kweli.
Wewe ndio kenge zee kabisa..

Ule uchafu na uzushi wa makinikia ya Mwendazake kupitia Ossoro ndio unataka Serikali ifanye Kazi?

Kwa nini waliotunga huo upuuzi hawaku claim hizo pesa? Unaelewa maana ya Trilioni 360 kwanza?

Kama zipo kazichukue basi.
 
Ina maana Mpina aliamini zile hadithi za marehemu? Zile zilikuwa ni story za kunogesha baraza kwa wasio na akili, wenye akili wote walijua kuwa ni uwongo.
Siyo kuamini... Kama ni uongo basi waje wazi ili tujue kuwa akina Propesa Ossoro walipresent Professorial Rubbish. Pia watu wawajibishwe kwa huo uongo.... Ili next time tusifanywe mazuzu tena.
 
Zile b 700 Lisu alizitoa Miga?

Embu utuambie, Kama Accasia hawakuwa majizi, iweje watoe hizo pesa hata kama ni kidogo!

Acha uzuzu Dogo!
Haya ngoja tuone kama Swali la Mbunge kuna mtu wa kumjibu.

Hizo bil 700 zenyewe ziko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…