Mwigulu aliacha lini kuutaka Urais?

Mwigulu aliacha lini kuutaka Urais?

Mwigulu Lameck Nchemba Madelu alijitokeza kwenye kinyang'anyiro cha 2015.

View attachment 2343267

Kwa kweli siyo siri kuwa huyu ndugu alikuwa na kiu kubwa ya kuitumia haki yake hiyo ya kikatiba. Basi tu wajumbe hawakuzithamini potentials zake nyingi anazozijua mwenyewe.

"Pana maswali ya kujiuliza kwa yeyote anayeikodolea macho fursa ya 2025."

Je, kiu ya ndugu Madelu kama ilikwisha, ilimalizwa na nini?

Je ni uchochoro upi wa kupitia angali nao Madelu kuweza kuipata nafasi hiyo adhimu japo hata kwa kuwa candidate tu?

Vipi hii Singida United imechipuka chipuka kama uyoga tu?

Vipi haya mabango kuendelea kuwepo wakati wagombea wengine walisha vunja makundi?

Penye Tozo pana njia.
Ndio kwanza kumepambazuka.. Kama ni balehe ya kigoli ndio kwanza hata kuchezwa bado na kifua bado kigumu vile vijipu
FB_IMG_1662078835884.jpg
 
Na safari hii ndio anajiandaa haswa..

Ni kama vile amejua huko chamani kwao bila mfuko mnene wa kutosha mgombea hatoboi mbele ya wajumbe..

Sasa anachotufanyia kwenye hizi tozo uuh ajue tu Mungu anamuona.
 
Kiukweli mimi ni mtu wa mizaha sana!. Hata hapa ile 2014, nilikuwa nafanya mzaha tuu Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Hivyo mzaha wangu huu Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, Sauti Imeshauri Mama Amkabidhi Kwanza Dr. Mwinyi, Urais wa JMT, Ndipo Aje Mwanamke!
Uweke tuu kwenye kumbukumbu zako, 2025 ikifika nitakukumbusha.
P
Hiyo voices from within yako ya mama kumkabidhi mgombea toka Zanzibar 2025 nakubaliana nawe 100%
 
Naona, basi wewe ni Mwanamalundi wa zama zetu umekuja, katika umbo la Mwanamayalla.
Karibu mitaa hii "Ombeni Mtapewa", Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je Wajua Kauli Huumba? Angalia Kauli Hizi Ziliumba Nini!. Laiti Zingesikizwa...!.
P
Acha ujinga wewe jamaa! Hatujawahi kuwa na zamu eti this time muisiramu au this time ni mkristo!
Tufanye ni ilijitokea tuu bila kupangwa Nyerere akawa Mkristu akapokelewa na Mwinyi Muislamu, akapokelewa na Ben, Mkristu, akapokelewa na JK Muislamu, then JPM Mkristu na sasa Samia, Muislamu.
Ilijitokelezea tuu!. Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Mustakabali wa 'Urais' wa JMT?
Au this time Tanzania bara au this time Tanzania visiwani! Jakaya alitoka bara
Baada ya Ben, ilikuwa iwe ni zamu ya Zanzibar mgombea alikuwa awe Dr. Omar Ali Juma!. Naomba nisikuambie what happened... Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano, 2015 Si Zamu ya Zanzibar?
,Nilikua nakuheshimu sana humu jukwaani, kumbe na wewe ni hovyo kabisa
Duh...!. Haya asante!.
D
 
Karibu mitaa hii "Ombeni Mtapewa", Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je Wajua Kauli Huumba? Angalia Kauli Hizi Ziliumba Nini!. Laiti Zingesikizwa...!.
P

Tufanye ni ilijitokea tuu bila kupangwa Nyerere akawa Mkristu akapokelewa na Mwinyi Muislamu, akapokelewa na Ben, Mkristu, akapokelewa na JK Muislamu, then JPM Mkristu na sasa Samia, Muislamu.
Ilijitokelezea tuu!. Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Mustakabali wa 'Urais' wa JMT?

Baada ya Ben, ilikuwa iwe ni zamu ya Zanzibar mgombea alikuwa awe Dr. Omar Ali Juma!. Naomba nisikuambie what happened... Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano, 2015 Si Zamu ya Zanzibar?

Duh...!. Haya asante!.
D
Bado nakupinga tu! Nyerere kua Bara,then Mwinyi Zanzibar,akaja Ben, Jakaya, Magu na asa hivi Samia! Sio kwamba ni sheria! Ungesema kwamba Rasi akiwa Bara,Basi Makamu awe Zanzibar hapo ningesema sawa!

Baada ya Ben,ilikua lazima Jakaya awe Rais,hata 1995, Jakaya ndiyo aliongoza kura za urais! Kifo cha Dr Omary Juma,sijui nini kilitokea! Kama unajua tujuze,hata kama Dr Omary Juma alifariki,ina maana hapakua na watu wengine wenye power zaidi ya Dr Omary Juma?? Mbona walikuwepo kina Dr Gharib Bilal! Na wengine wengi?? Je kama Magu asingefariki,unadhani Rais angekua nani?? Najua utasema Hussein Mwinyi! Lakini wote hatujui na kama ndiyo Hussein Mwinyi angekua Rais wa JMT!
 
Japo mimi namsuport Mwingulu kwenye urais kwa sababu hii Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa! lakini 2025 ni awamu ya pili ya Samia ambayo ataitoa zawadi kwa Zanzibar for one term kumalizia term yake, hivyo 2030 ni zamu ya mgombea mwanamke Mkristu probably Dr. Tulia!. 2040 ni zamu ya Muislamu. Sasa Mwigulu atapitia wapi?.
P
2030 Ni zamu ya mkristo mkatoliki si lazima awe mwanamke Ila lazima awe mkatoliki. Mwigulu sio mkatoliki sioni nafasi yake kwenye urais hatokuja kuwa rais wa kusadikika hata kwa ndoto. Ila uwaziri mkuu labda
 
Kifo cha Dr Omary Juma,sijui nini kilitokea! Kama unajua tujuze,
Kuna vitu vingine afadhali usijue kuliko ukijua!. No news is good news!. Maadam hujui kilichotokea ni afadhali ukae hivyo hivyo usijue kuliko ukijua!.
P
 
In short Mwigulu will never be a President of this country. Case closed.
Marais wa nchi hupangwa na Mungu, hivyo kwa vile wewe sio Mungu, you can't be certain sure kuwa fulani hawezi kuwa rais!, unless mpangaji ni wewe!.
Kwani unadhani hata Samia alijua kuwa atakuwa rais?, hakujua!.

Alijua...! Duniani KOTE TISS ndiyo wapangaji WA Marais nchini mwao
 
Back
Top Bottom