Mwigulu aliacha lini kuutaka Urais?

Ndio kwanza kumepambazuka.. Kama ni balehe ya kigoli ndio kwanza hata kuchezwa bado na kifua bado kigumu vile vijipu
 
Na safari hii ndio anajiandaa haswa..

Ni kama vile amejua huko chamani kwao bila mfuko mnene wa kutosha mgombea hatoboi mbele ya wajumbe..

Sasa anachotufanyia kwenye hizi tozo uuh ajue tu Mungu anamuona.
 
Hiyo voices from within yako ya mama kumkabidhi mgombea toka Zanzibar 2025 nakubaliana nawe 100%
 
Naona, basi wewe ni Mwanamalundi wa zama zetu umekuja, katika umbo la Mwanamayalla.
Karibu mitaa hii "Ombeni Mtapewa", Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je Wajua Kauli Huumba? Angalia Kauli Hizi Ziliumba Nini!. Laiti Zingesikizwa...!.
P
Acha ujinga wewe jamaa! Hatujawahi kuwa na zamu eti this time muisiramu au this time ni mkristo!
Tufanye ni ilijitokea tuu bila kupangwa Nyerere akawa Mkristu akapokelewa na Mwinyi Muislamu, akapokelewa na Ben, Mkristu, akapokelewa na JK Muislamu, then JPM Mkristu na sasa Samia, Muislamu.
Ilijitokelezea tuu!. Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Mustakabali wa 'Urais' wa JMT?
Au this time Tanzania bara au this time Tanzania visiwani! Jakaya alitoka bara
Baada ya Ben, ilikuwa iwe ni zamu ya Zanzibar mgombea alikuwa awe Dr. Omar Ali Juma!. Naomba nisikuambie what happened... Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano, 2015 Si Zamu ya Zanzibar?
,Nilikua nakuheshimu sana humu jukwaani, kumbe na wewe ni hovyo kabisa
Duh...!. Haya asante!.
D
 
Bado nakupinga tu! Nyerere kua Bara,then Mwinyi Zanzibar,akaja Ben, Jakaya, Magu na asa hivi Samia! Sio kwamba ni sheria! Ungesema kwamba Rasi akiwa Bara,Basi Makamu awe Zanzibar hapo ningesema sawa!

Baada ya Ben,ilikua lazima Jakaya awe Rais,hata 1995, Jakaya ndiyo aliongoza kura za urais! Kifo cha Dr Omary Juma,sijui nini kilitokea! Kama unajua tujuze,hata kama Dr Omary Juma alifariki,ina maana hapakua na watu wengine wenye power zaidi ya Dr Omary Juma?? Mbona walikuwepo kina Dr Gharib Bilal! Na wengine wengi?? Je kama Magu asingefariki,unadhani Rais angekua nani?? Najua utasema Hussein Mwinyi! Lakini wote hatujui na kama ndiyo Hussein Mwinyi angekua Rais wa JMT!
 
2030 Ni zamu ya mkristo mkatoliki si lazima awe mwanamke Ila lazima awe mkatoliki. Mwigulu sio mkatoliki sioni nafasi yake kwenye urais hatokuja kuwa rais wa kusadikika hata kwa ndoto. Ila uwaziri mkuu labda
 
Vipi haya mabango kuendelea kuwepo wakati wagombea wengine walisha vunja makundi?

Penye Tozo pana njia.
Mtia nia wa Urais aliyetumia mawe kama mabango
 
Kifo cha Dr Omary Juma,sijui nini kilitokea! Kama unajua tujuze,
Kuna vitu vingine afadhali usijue kuliko ukijua!. No news is good news!. Maadam hujui kilichotokea ni afadhali ukae hivyo hivyo usijue kuliko ukijua!.
P
 
In short Mwigulu will never be a President of this country. Case closed.
Marais wa nchi hupangwa na Mungu, hivyo kwa vile wewe sio Mungu, you can't be certain sure kuwa fulani hawezi kuwa rais!, unless mpangaji ni wewe!.
Kwani unadhani hata Samia alijua kuwa atakuwa rais?, hakujua!.
P
 
Marais wa nchi hupangwa na Mungu, hivyo kwa vile wewe sio Mungu, you can't be certain sure kuwa fulani hawezi kuwa rais!, unless mpangaji ni wewe!.
Kwani unadhani hata Samia alijua kuwa atakuwa rais?, hakujua!.
P
Alijua...! Duniani KOTE TISS ndiyo wapangaji WA Marais nchini mwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…