Mwigulu awaomba viongozi wa Yanga wapotezee suala la Kagoma ili aweze kucheza Simba

Mwigulu awaomba viongozi wa Yanga wapotezee suala la Kagoma ili aweze kucheza Simba

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Nafahamu undani wa Suala la Yusuf Kagoma, ni kweli Kagoma alisaini mkataba Yanga, na baadae akasaini Simba.

Najua kutokwenda kwake Yanga na badala yake kusaini Simba hata sio Masuala ya Fedha. Tutatumia muda sana tukitaka kuchimba haya.

Kagoma ni mtoto wetu, Yanga ni Club kubwa sana na ina mambo muhimu ya kuyawekea nguvu kuyafanikisha kuliko kuweka nguvu Kagoma aisicheze licha ya ukweli kwamba alistahili achezee Yanga.

NIMEWAOMBA VIONGOZI WA YANGA WASAMEНЕ YOTE, WAONDOE SHAURI DHIDI YA KAGOMA, WAMWACHE AWE HURU AKAITUMIKIE SIMBA KWA MASLAHI MAPANA YA MPIRA WA TANZANIA NA KWA FAIDA YA MCHEZAJI MWENYEWE.

Waziri wa Fedha.

20240824_175414.jpg
 
anatafuta umaarufu tu, maana anashauri jambo ambalo limeishamalizika. Hata kabla hajasema hivyo, tayari Kagoma ameshaidhinishwa Simba na alikuwa ni mmoja wa wachezaji wa akiba katika mechi dhidi ya Tabora
 
Nawashauri Yanga washikilie hapohapo, unamuachiaje silaha adui ili akudhuru!
 
Shida ya wachezaji wa Bongo ni kupenda kwao kuendekeza siasa za Simba na Yanga. Na sishangai kuona wengi wao hawatoki nje ya mipaka yaTanzania.
 
Shida ni kwamba wanadhani Singida FG bado ni Utopolo B.
 
Huyu bwana ni mmoja wa vivuruge wakuu wa mpira wa Tanzania
 
Nafahamu undani wa Suala la Yusuf Kagoma, ni kweli Kagoma alisaini mkataba Yanga, na baadae akasaini Simba.

Najua kutokwenda kwake Yanga na badala yake kusaini Simba hata sio Masuala ya Fedha. Tutatumia muda sana tukitaka kuchimba haya.

Kagoma ni mtoto wetu, Yanga ni Club kubwa sana na ina mambo muhimu ya kuyawekea nguvu kuyafanikisha kuliko kuweka nguvu Kagoma aisicheze licha ya ukweli kwamba alistahili achezee Yanga.

NIMEWAOMBA VIONGOZI WA YANGA WASAMEНЕ YOTE, WAONDOE SHAURI DHIDI YA KAGOMA, WAMWACHE AWE HURU AKAITUMIKIE SIMBA KWA MASLAHI MAPANA YA MPIRA WA TANZANIA NA KWA FAIDA YA MCHEZAJI MWENYEWE.

Waziri wa Fedha.

View attachment 3078170
Wanasiasa wa bongo wanapenda kwenda na upepo ili watrend mara VAR,mara usajili wa Kagoma ila mambo yao ya msingi hawa yafanyi, dola inakimbia kila siku mda si mrefu itakuwa buku tatu kwa dola moja.
 
Back
Top Bottom