Aliyoyasema Mtaka Wakamwambia Atubu Haraka
Hawana Cha Kupoteza Hata Maisha Yakiwa Juu
 
Mwingulu ni masalio ya mwendazake ilibidi aondolewa mapema na Mama, pia ana ambition ya kua Raisi mwingulu ni sumu kwa Mama.
Aliyekwambia Mwigulu anapanga bajeti peke yake alikudanganya! Kila jambo linalotendeka lina baraka za Mama,
 
Msitegemee CCM kuja kuifikisha hii nchi Kwenye Maziwa na Asali.

Wanasema hii nchi ni Tajiri ina Raslimali za kutosha , alafu leo wanakuja na hoja za hovyo kabisa eti kodi ya Uzalendo kwenye miamala ya Simu,eti ikasaidie ujenzi wa barabara vijijini ..

Zaidi ya miaka 50 ya uhuru bado wanazungumzia barabara hawa hawafai wameishiwa sera.
 
Mwigulu hana anachoharibu,kwasababu hili jambo lilipitishwa na bunge la bajeti kipindi cha bajeti ya serikali,serikali ambayo iko chini ya huyo huyo unayepeleka malalamiko kwake.ata hivyo alishawaambia anataka kukuza uchumi,ndo hivyo wameamua kukuza uchumi kwa kumkamua mwananchi wa chini uku wao wakiendelea kula maisha.
 
... nendeni kwenye mikutano ya kisiasa/kampeni mkasikilize na kuchuja sera na ilani - hatuna nafasi sisi!
... someni sera za vyama na ilani zao mpate mwanga wa jinsi zitakavyosaidia au kuumiza maisha yenu watanzania - hayatuhusu sisi!
... fuatilieni vyombo vya habari mjue yanayojiri nchini na Bungeni kwa manufaa ya maisha yetu na vizazi vyetu - mambo ya wanasiasa hayo!
... sikilizeni hotuba za viongozi wa kisiasa na kuzichambua kwa umakini - fiesta iko mtaani leo!
... kutakuwa na mikutano ya kisiasa kuhusu Katiba Mpya - hayatuhusu, tumpigie kura Diamond ashinde!
... jamani saa mbili usiku wekeni taarifa ya habari kuna jambo zito la kitaifa - kaangalie chumbani kwako na mkeo sisi tunaangalia mchezo!

Siasa ndio kila kitu ndiyo inayoamua maisha yetu ila ndicho kitu kinachopuuzwa zaidi na watanzania! Unapopuuza siasa unapuuza maisha yako hivyo tusilalamike wala kumsingizia mtu; ni matokeo ya upumbavu wetu wenyewe!
 
Mkuu huyu mwigulu anaharibu uchumi badala ya kuupandisha.
Impact ya watu kuacha kutuma miamala kwa njia ya simu sii tu itaathiri watumiaji bali hata makampuni ya simu, hii kitu ina mulplier effects. Makampuni ya simu yatakosa mapato na hivyo corporate tax itashuka hivyo serikali kukosa kodi kama awali iliyokua inatoka kwenye makampuni.

Sjui mugulu amefikiriaje
 
Baada ya huo upigaji wa juzi hapa, kuna gari yake imeingia kimya kimya 0KM, 400M asifikiri hatufahamu!
Inajulikana wazi kuwa mabasi mapya ya ESTER yanayopiga route ya Arusha-Moshi-Dsm ni ya MWIGULU NCHEMBA

Asifikiri hatujui uhuni alioutumia kwa kuyasajili kwa jina la Dada wa kirombo.

Mwigulu ni fisadi
 
Kuna jamaa moja aliwahi kuniambia Tanzania ni nchi ya ajabu sana kuna mambo ambayo dunia nzima hakuna ila Tanzania yapo

Nataka nione huyu muheshiwa waziri akefanya upembivu yakinifu kupitia kitabu gani cha uchumi hadi akaja na wazo la kuweka tozo ya tshs 9400 na ada ya mtandao tshs 8000 jumla inakua tshs 17409 kwa kwananchi wake anae taka kutoa milioni moja yake iliyopo katika pesa mtandao



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mjinga anahanyahanya tu
 
Kama maisha ya uchumi wabkati ndo haya Bora NIRUDI uchumi wa mwanzo TU!!
 
Yajayo yanasikitisha Sana, naona future ya Tanzania ikizidi kuwa Giza zaidi. Hakika tutalimia meno huko tuendako
Tuna imani na mama, au mnasemaje ndugu zangu?
 
Mwigulu ni sehemu ya baraza la mawaziri ni sehemu ya vikao vya maamuzi.

Kuongoza nchi sio sawa na kuongoza jumuiya ya kikristo au kundi fulani la wastaafu wa mtaani.

Kujitegemea kuna gharama zake na ndio hizi, yule mjomba wa nje anayo majukumu yake tena yamemfika shingoni anayo corona na sasa ana majanga ya mvua kubwa zilizoua watu Ujerumani na Ubelgiji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…