Yeye naona haimuhusu aiseeee, kwa kuwa ni mnufaika.... masuala ya msingi ya kitaifa, wengine wanaendelea kuleta ushabiki wa vyama......Tz safari bado ni ndefu.
Kwa hiyo wewe haikuhusu,inahusu chadema sivyo?
 
Tanzania kuna bunge!!???
 
Vitu vingine SSH anayataka mwenyewe , mtu alie wai kua wizara ya fedha na wenzake au watangulizi wake wakaona hapamtoshi, akapewa wizara ya Mambo ya ndani bado wakaona hapamtoshi then katiba na sheria, leo wamrudisha kule , huyu Mwingulu , hamna kitu ,natamani nafasi yake angepewa tu Mbunge Kishimba ,ana vyeti tu ,ila hamna lolote,
 
mkuu unasema mpango kakaa kimya wakati alitweet anasema "wananchi wote vumilieni tu mtazoea"
yaani hapa mwigulu anafanya alichojadili na mamlaka zake za uteuzi akiwemo mpango, kiukwli awam hii tumepigwa aisee.

kiukwel mm huwa inafika kipindi nawaza bora ata tusingekuwa na hili bunge, hawa wabunge hamna kitu wamesababisha hasara kubwa sana ktk hili taifa, wanajilipa miposho mikubwa ambayo haikatwi kodi na marupurupu mengine juu, mbunge pekee aliyejaribu kuiomba serikali ipunguze posho za wabunge ni Zitto Z Kabwe. nakumbuka alishambuliwa vikali sana kuanzia bungeni mpaka kwenye mitanao, na waliokuwa wakimshambulia ni wabunge wenzake wakiwemo waupinzani huku mwigulu akiongoza mashambulizi.

kiukweli tumpigwa tema pakubwa mno.
 
Mawazo ya mfu. Ukiwa hai huwezi kuwa na mawazo haya. Unaogopa kinyago ulichochonga mwenyewe?
ata tukiongea haita saidia. wakishaamua wameamua. ata baada ya mwezi wakipandisha tena mtapiga tu kelele kwenye mitandao mwisho wa siku makato yataendelea kama kawaida.
 
Hivi kama hatutaki kukatwa kodi ili tuendeleze nchi yetu,nchi yetu itaendelezwa vipi?

Mtoa mada wewe kama ungekuwa Waziri wa Wizara husika ungefanya nini ili kuongeza mapato ya Serikali ili irudishe maendeleo kwa wananchi??

Wakati tunalalamika tuwe tunatoa na suluhisho ili mhusika apate kulichukua na ikiwezekana kulifanyia kazi
 
Kati ya mawaziri wa hovyo huyu ni namba moja, watu wanaofanya miamala ya Simu wengi ni wenye maisha ya chini, mabenki yana makato madogo kuliko hata makampuni ya simu.

Miamala ya simu inafanywa na watu wengi vijijini walio mbali na mabenki kurahisisha mambo.

Huyu waziri amekuwa wa hovyo kabisa eti kodi ya mshikamano, unaleta kodi ya mshikamano wakati wao wabunge hawatumiwi mishahara kwa mpesa. Huyu waziri anatakiwa ajiuzulu maana ana akili mgando.

Kuna wazazi watoto wao wanasoma shule za bweni mbali, wanatuma hela za matumizi ambazo ni kuuza kuku au mbuzi, mzazi anatuma 50,000 ya matumizi halafu hela ya kutolea ni jogoo wawili.

Mzazi analipa hela ya chakula cha mtoto shuleni hela ya kutolea anauza mbuzi mzima.

Hivi uchumi gani huu wa kijinga halafu Mwingulu na Rais wote ni wasomi wa Uchumi.
 
Mbona mnatuhumu Mwigulu tu? Hivi unafikiri Rais alikuwa hajui mwaka wa fedha 2021/2022 wataingiza Tsh ngapi na kupitia vyanzo vipi vya mapato? Walianza kujadili wenyewe huko yakapitishwa kwenye vikao mpaka vya baraza la mawaziri ndo wakatuletea sisi uku.

Mtu ameteua mpaka mshauri wake wa masuala ya uchumi yupo anakuja kusaini iyo bill as if alikuwa hajui kusoma!

 
Kodi zetu za Kizalendo zinaweza kupita na kichwa cha mtu

Kodi na tozo zisizo na mashiko ni hatare sana kwa president anaesikiliza wananchi kama Madam SSH

The minister could be the champion on the previous regime but not this One

Time will tell
 
Sheria iliyopitishwa na bunge yaweza kuwa nzuri shida kwa hawa wasimamizi wa utungaji wa kanuni. Na ndiyo hasa shida vinginevyo ungesikia statement zao sheria irejewe bungeni na sio kanuni. Kwakuwa kanuni wametengeza wao ndiyo wameamua kwenda kuzirejea. Kwahiyo wafukuzwe kabisa. La tungesema baraza la mawaziri livunjwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…