MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Mh Mwigulu ni kweli wewe ni msomi wa hali ya juu na hilo halina ubishi. Kutoka Ilboru hadi UDSM sio jambo la masikhara. Wewe ni mwanasiasa msomi. Pia ni mwanasiasa mwenye haiba ya uongozi na unafaa hata kuwa Rais wa nchi hii. Binafsi namshukuru Mungu kwa mabadiliko uliyoyaonyesha kuanzia mwishoni mwa uongozi wa JK. Enzi zako za ujana kuna picha zilienea ukimvalisha mbuzi tshirt ya CHADEMA kitu ambacho hakikuwa sawa. Bahati nzuri ulishtuka na ukaachana na siasa za aina ile. Hata zile siasa za kuandika mawe barabarani sidhani kama utaendelea nazo. Kwa ufupi Mwigulu unafaa kuwa Rais. Haiba na elimu unayo huku ukiwa na uzoefu wa uongozi kuanzia UVCCM.
Kwenye awamu hii ya sita pia ulianza vizuri ingawa kuna mambo ulikuwa unafanya mwanzoni yalikuwa ya kisiasa. Kwa mfano wewe waziri kuweka mikutano ya hadhara kwa kisingizio cha kuongea na wananchi ilikuwa ni kampeni za siri. Bahati nzuri pia umeachana na hiyo style. Kwa sisi tunaokumbuka harakati zako za kutaka uwe rais tulishakusoma.
Mimi kama mtu ninayevutiwa na aina yako ya siasa ninakusihi achana na haya mambo ya kupendekeza mambo yanayowaumiza watanzania. Hizi ishu za tozo zinakuharibia mno. Hatuwezi kumlaumu mtu mwingine zaidi yako wewe waziri mwenye dhamana. Inawezekana wataalamu wanakuletea hizi ideas kwa lengo la kukuharibia nia yako. CCM haitabiriki kabisa hasa nyakati za uchaguzi. Zile nyakati waweza shangaa ukapigwa chini hata tano bora usifike ili CCM isijiharibie kwa wananchi. Nakushauri peleka muswada wa dharura bungeni hii sheria inayohusiana na tozo irekebishwe.