Mwigulu kuwa makini. Tozo zitakuharibia malengo ya kuwa Rais

Mwigulu kuwa makini. Tozo zitakuharibia malengo ya kuwa Rais

Mh Mwigulu ni kweli wewe ni msomi wa hali ya juu na hilo halina ubishi. Kutoka Ilboru hadi UDSM sio jambo la masikhara. Wewe ni mwanasiasa msomi. Pia ni mwanasiasa mwenye haiba ya uongozi na unafaa hata kuwa Rais wa nchi hii. Binafsi namshukuru Mungu kwa mabadiliko uliyoyaonyesha kuanzia mwishoni mwa uongozi wa JK. Enzi zako za ujana kuna picha zilienea ukimvalisha mbuzi tshirt ya CHADEMA kitu ambacho hakikuwa sawa. Bahati nzuri ulishtuka na ukaachana na siasa za aina ile. Hata zile siasa za kuandika mawe barabarani sidhani kama utaendelea nazo. Kwa ufupi Mwigulu unafaa kuwa Rais. Haiba na elimu unayo huku ukiwa na uzoefu wa uongozi kuanzia UVCCM.

Kwenye awamu hii ya sita pia ulianza vizuri ingawa kuna mambo ulikuwa unafanya mwanzoni yalikuwa ya kisiasa. Kwa mfano wewe waziri kuweka mikutano ya hadhara kwa kisingizio cha kuongea na wananchi ilikuwa ni kampeni za siri. Bahati nzuri pia umeachana na hiyo style. Kwa sisi tunaokumbuka harakati zako za kutaka uwe rais tulishakusoma.

Mimi kama mtu ninayevutiwa na aina yako ya siasa ninakusihi achana na haya mambo ya kupendekeza mambo yanayowaumiza watanzania. Hizi ishu za tozo zinakuharibia mno. Hatuwezi kumlaumu mtu mwingine zaidi yako wewe waziri mwenye dhamana. Inawezekana wataalamu wanakuletea hizi ideas kwa lengo la kukuharibia nia yako. CCM haitabiriki kabisa hasa nyakati za uchaguzi. Zile nyakati waweza shangaa ukapigwa chini hata tano bora usifike ili CCM isijiharibie kwa wananchi. Nakushauri peleka muswada wa dharura bungeni hii sheria inayohusiana na tozo irekebishwe.
Sikubaliani vitu vitatu kwenye hii mafa yako;

1. Mwigulu siyo msomi wa hali ya juu kwa kuwa hata PhD yake ni ya kuandikiwa tu baada ya kutoa pesa. Siyo rahisi kupata PhD ukiwa Waziri ambaye uko kazini kila wakati. Hizi PhD za akina Magufuli, Mwigulu, Doto Biteko na Selemani Jafo, wanatoa fedha na kuandikiwa na maprofesa wa vyuoni.

2. Mwigulu hawezi kuwa Rais wa Tanzania kamwe. Ataishia kuwa na ndoto tu. Mwigulu ana baadhi ya tabia za ki-Makonda au Ki-Magufuli za kuua wapinzani. Nchi hii haiwezi kurudi kwa mijitu mikatili tena
 
Da kaona kodi haitoshi,mikopo haiyoshi,sasa tozo nazo pia wanaona hazitoshi,waataamia kodi ya kichwa kila utembeapo lipia 1000.
 
Mkuu WAZO2010, ulaya ni ulaya na Afrika ni Afrika

Shuhudia Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!

Shuhudia January Makamba, very intelligent, humble, down-to-earth! Can make the best President

Naomba fafanua upuuzi kivipi?

Fafanua mihemko kivipi?.

Wizi gani?

Sifa gani, Umalaya gani?.
P
Sasa kama Ulaya ni Ulaya na Africa ni Africa. Kuna technologia gani Africa tunaweza jivunia Africa? Chanjo zote Ulaya. Hii Democrasia tume Copy wapi? Why tusi copy na umri wa ma Rais wa Ulaya? 60s+ . Au tuna copy chenye ku favour baadhi ya watu tu ila visivyo wa favour mna tupa kapuni?
 
Back
Top Bottom