Mwigulu: Maveterani wa Vita vya Kagera kuanza kulipwa Pensheni zao

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema maveterani wa Vita ya Kagera wataanza kulipwa pensheni zao kuanzia mwaka wa fedha 2026/27, baada ya Serikali kukamilisha hatua zote za kisheria na uhakiki wa wanufaika.

1781850019363.png

Akijibu maswali ya wabunge bungeni Juni 18, 2026, Mwigulu alisema Serikali ilitoa Tangazo la Serikali (GN) mwezi Juni 2025 kufuatia marekebisho ya sheria yaliyowatambua rasmi wapiganaji hao kuwa wanastahili mafao na pensheni.

Soma, Pia: Stergomena Tax: Waliopigana vita ya Kagera kuanza kulipwa pensheni kuanzia Julai 2026

Amesema baada ya kutolewa kwa tangazo hilo, Serikali ilikamilisha zoezi la uhakiki wa maveterani waliobaki hai wanaostahili kunufaika, ambapo jumla ya wapiganaji takribani 7,200 walithibitishwa kupitia zoezi hilo.

Mwigulu alieleza kuwa kwa kuwa hakuna tena kikwazo cha kisheria wala cha uhakiki, Serikali itaanza taratibu za kuwalipa pensheni maveterani hao katika mwaka mpya wa fedha, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya kuwapatia stahiki zao.

Mbona wengi walishatangulia mbele ya haki isitoshe waliopo ndoto zao za maisha zilishayeyuka kwa kutokulipwa stahiki zao kwa wakati
 
CCM bhana!!, baadae watakwambia waliogmbania uhuru wote waende kujisajili ili waanze kulipwa viinua mgongo vyao
:AYOOO::AYOOO:
 
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema maveterani wa Vita ya Kagera wataanza kulipwa pensheni zao kuanzia mwaka wa fedha 2026/27, baada ya Serikali kukamilisha hatua zote za kisheria na uhakiki wa wanufaika.

Akijibu maswali ya wabunge bungeni Juni 18, 2026, Mwigulu alisema Serikali ilitoa Tangazo la Serikali (GN) mwezi Juni 2025 kufuatia marekebisho ya sheria yaliyowatambua rasmi wapiganaji hao kuwa wanastahili mafao na pensheni.

Soma, Pia: Stergomena Tax: Waliopigana vita ya Kagera kuanza kulipwa pensheni kuanzia Julai 2026

Amesema baada ya kutolewa kwa tangazo hilo, Serikali ilikamilisha zoezi la uhakiki wa maveterani waliobaki hai wanaostahili kunufaika, ambapo jumla ya wapiganaji takribani 7,200 walithibitishwa kupitia zoezi hilo.

Mwigulu alieleza kuwa kwa kuwa hakuna tena kikwazo cha kisheria wala cha uhakiki, Serikali itaanza taratibu za kuwalipa pensheni maveterani hao katika mwaka mpya wa fedha, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya kuwapatia stahiki zao.

Wenza wa viongozi, haraka sana walianza kulipwa marupurupu ya kupendwa na walioongoza nchi, walioipigania nchi inachukua miaka karibu 40 na bado hawajaanza kulipwa, bado wanaishi wakisubiri mafao yao! Ccm ina wenyewe!
 
Duh Ngoja nimstue mzee,na bi mkubwa maana wote walikuwa huko
nachojuwa waliambulia vyeti na nishani tu

ova
 
Back
Top Bottom