GE2025 Mwigulu: Mkinipatia ridhaa nitapasua barabara na nitashusha shule mpya

GE2025 Mwigulu: Mkinipatia ridhaa nitapasua barabara na nitashusha shule mpya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mgombea ubunge jimbo la Iramba Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa endapo akipata ridhaa ya kuwa Mbunge kwa awamu nyingine ataongeza na kuboresha miundombinu ya Elimu, Afya, Barabara pamoja na Maji ili wananchi Wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida waendelee kupata huduma bora, salama na ya Haraka

Ameyasema hayo wakati akifungua kampeni ya kunadi Sera zake katika Kijiji cha Makunda kata ya Kyengege ili kupata ridhaa ya kuendelea kuwa Mbunge Wa jimbo la Iramba Mashariki

Mwwnyeki Wa Ccm mkoa Wa Singida Martha Mlata alishuhudia uzinduzi huo huku akiwataka wananchi Wa Iramba Mashariki kuendelea kumuamini Dkt Mwigulu na Mgombea Urais kupitia Ccm Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapigia kura za ndio Oktoba 29 na kupata ushindi wa Kishindo

Aidha Katibu Wa Ccm wilaya ya Iramba Filbert Mdaki amesema kuwa uchaguzi Wa mwaka huu watafanikiwa kupata ushindi kwa asilimia kubwa kutokana na kufanikiwa kuvunja makundi baada ya kupita kwa uchaguzi wa ndani




Chanzo: Crown Digital
 
Back
Top Bottom