Mwigulu Nchemba atoa siku 14 makampuni ya mawasiliano kutoza kodi zilizokubaliwa

Mwigulu Nchemba atoa siku 14 makampuni ya mawasiliano kutoza kodi zilizokubaliwa

Kumbe walipitisha makato mapya ktk miamala ya fedha ktk simu...

Na wakapitisha Kodi ya laini ya simu...

Hawa wabunge ni wa Taiwan au Tanzania? Mbona ni mzigo mkubwa kwa watumiaji wa simu...
Unapigia majibu mstari?
 
Haya makampuni hayawezi kuwa upande wa wananchi
Kama serikali inatafuta kodi itafute namna nyingine si kwa kupitia wao
 
Hii ni hatari Sana.Are they trying to avoid people's freedom to use social media
 
Mwigulu ni tatizo kwa hizo kodi mara mafuta sijui kutuma hela na hii covid wao hawaoni kuna tatizo la mdororo wa Uchumi duniani wapo na kodi mpya badala ya kuwapa wananchi hauweni...anakera sana Mwigulu
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa watoa huduma wa mitandao ya simu kurekebisha mifumo na kuanza kutoza makato mapya ya Serikali.

Hivi karibuni Bunge lilipitisha tozo kuanzia Sh10 hadi Sh10,000 itakayotozwa kwa kila muamala wa kutuma/kupokea fedha.
Hizi kodi ni muhimu sana. Hii nchi haitajengwa kwa vibanda vya wafanyabiashara wa kariakoo tu. Wote tulipe kodi, ili wabunge wetu wapate mishahara yao kwa wakati
 
Kumbe walipitisha makato mapya ktk miamala ya fedha ktk simu...

Na wakapitisha Kodi ya laini ya simu...

Hawa wabunge ni wa Taiwan au Tanzania? Mbona ni mzigo mkubwa kwa watumiaji wa simu...
Si mlikuwa busy kushangilia
 
Hapa uwezi kuwasikia wale wapumbavu wanajadili kauli ya Mdude. Hapa solution ni kuzidi kukwepa kodi na kuiba tu.
 
Itakuwa ana gani ya kodi by definition?

Kodi ina kanuni zake za kuzingatiwa.

Je zimezingatiwa?
 
Chekecheo kwenye bando linakuja
 
Sawa Serikali ianze kuwalipa watumishi wake telephone allowance maana wengi wao wanatumia simu binafsi kwa kazi za serikali, serikali haiwezi kufaidika mara mbili toka kwa mtumishi huyohuyo
Halafu kuna mtu anakwambia ametoa maagizo ya kikazi kwenye group la wasap la ofisi, yaani mimi nikae kutwa nzima nasoma meseji za wasap kwa kutarajia maagizo ya kikazi kutoka ofisini........hii mitandao mbona imetufanya watu kuwa wajinga sana.....
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa watoa huduma wa mitandao ya simu kurekebisha mifumo na kuanza kutoza makato mapya ya Serikali.

Hivi karibuni Bunge lilipitisha tozo kuanzia Sh10 hadi Sh10,000 itakayotozwa kwa kila muamala wa kutuma/kupokea fedha.
Ningemuona wa maana kama kwanza angetoahizo siku14 kwenye gharama za vifurushi ambazo zimebaki palepale pamoja na kwamba mkuu alitaka TCRA iingilie kati na hata tukaletewa Mkurugenzi mpya wa TCRA lakini hadi sasa hakuna mabadiliko yoyote, kwenye mambo ya msingi kwa wananchi hatuwasikii mkitoa siku 14 kwenye maumivu ndio mko serious!
 
Back
Top Bottom