Mwigulu Nchemba: Deni la Taifa ni tofauti na fedha ya kwenye ATM. Asema amesaini malipo ya deni lilikopwa kabla hajazaliwa

Mwigulu Nchemba: Deni la Taifa ni tofauti na fedha ya kwenye ATM. Asema amesaini malipo ya deni lilikopwa kabla hajazaliwa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba leo ameongelea deni la Taifa. Amesema deni la Taifa sio kama fedha ya kwenye ATM ambayo unaingiza kadi na kutoa.

Mwigulu anasema anayekopa sio Rais bali Serikali na yeye amesaini kulipa deni lilikopwa awamu ya kwanza wakati hajazaliwa.

Mwigulu amesema kuna mikopo imesainiwa zamani lakini pesa zake zinatoka kwa awamu hivyo kadri inavyopokelewa ndivyo deni linatangazwa upya.

Na wao wanayokopa watalipa ambao hawajazaliwa na bara bara au Reli zikijengwa watapita ambao leo wao wakisaini wao walikua hawajazaliwa..ni kanuni ya maendeleo.
 
Huyu anataka kuhalalisha wizi wa mchana kweupe, yaani wanakopa wanapeleka kwenye miradi hewa mwisho wa siku tunadaiwa watanzania, halafu kesho au keshokutwa mama akitoka madarakani anaanza kusema alikuwa analazimishwa ku sign! Na hali yeye ndiye anaye mwingiza mkenge mama!
 
Halafu serikali ikikopa na kufanya mradi,wanasema wanampongeza na kumshukuru Rais Kwa kutoa fedha za mradi husika!Wanamalizia na kibwagizo,"nani kama ......?"
 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba leo ameongelea deni la Taifa. Amesema deni la Taifa sio kama fedha ya kwenye ATM ambayo unaingiza kadi na kutoa.

Mwigulu anasema anayekopa sio Rais bali Serikali na yeye amesaini kulipa deni lilikopwa awamu ya kwanza wakati hajazaliwa.

Mwigulu amesema kuna mikopo imesainiwa zawani lakini pesa zake zinatoka kwa awamu hivyo kadri inavyopokelewa ndivyo deni linatangazwa upya.

Ni wapuuzi tuu ndio wanahangaika na deni la serikali, halijawahi kuwa shida popote..

Deni la US ni zaidi ya asilimia 200% ya Bajeti ya Nchi..

Sasa Tanzania tuna kideni kidogo ila makelele ya limbukeni ni shida tupu👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220622-221750.png
    Screenshot_20220622-221750.png
    44 KB · Views: 8
Back
Top Bottom