Mwigulu Nchemba: Kauli ya kumshukuru Rais kwa kutoa pesa isitugawe Watanzania

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kufahamu kwanini viongozi wanapenda sana kumshukuru Rais kwa kutoa fedha huku watu wanaochanga ni wananchi, Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba amesema sifa hizi hutolewa kwa kuwa Rais ndiye kiongozi mkuu wa nchi.

Amesema kuwa hii haiondoi ukweli kuwa wananchi ndiyo chanzo cha fedha hizo na ndiyo maana yeye mwenyewe kwenye maelezo yake ya leo amewashukuru wananchi kwa kiasi kikubwa.

Kumtaja Rais kusiwagawe Watanzania kwa kuwa yeye ndiye kabeba maono yote. Aidha, kuwa na maono na kutekeleza maono ni vitu viwili tofauti hivyo kwa kuwa Rais anatekeleza maono hayo ni muhimu kumshukuru.
 
Hili jibu lake; "sifa hizi hutolewa kwa kuwa Rais ndie kiongozi mkuu wa nchi" naona halijajitosheleza..

Angetakiwa kumalizia, au labda ametuacha wenyewe tumalizie "kiongozi mkuu wa nchi anayewagawia vyeo"
 
Hapo wanabembeleza vyeo
 
Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kufahamu kwanini viongozi wanapenda sana kumshukuru Rais kwa kutoa fedha huku watu wanaochanga ni wananchi, Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba amesema sifa hizi hutolewa kwa kuwa Rais ndiye kiongozi mkuu wa nchi.

Amesema kuwa hii haiondoi ukweli kuwa wananchi ndiyo chanzo cha fedha hizo na ndiyo maana yeye mwenyewe kwenye maelezo yake ya leo amewashukuru wananchi kwa kiasi kikubwa.

Kumtaja Rais kusiwagawe Watanzania kwa kuwa yeye ndiye kabeba maono yote. Aidha, kuwa na maono na kutekeleza maono ni vitu viwili tofauti hivyo kwa kuwa Rais anatekeleza maono hayo ni muhimu kumshukuru.
Hatutaki kusema mh rais ametowa kiasi fulani ktk mradi fulani mana hatowi mfukoni mwake.Bali tunashukuru serikali.
 
WATANZANIA wanataka mabadiliko kwenye sekta yoyote hapa nchini na taifa kwa ujumla ?
 
Back
Top Bottom