Mwigulu Nchemba: Kuwa na uwezo wa Kukopesheka ni sifa nzuri kwa Taifa

Mwigulu Nchemba: Kuwa na uwezo wa Kukopesheka ni sifa nzuri kwa Taifa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Waziri wa Fedha na mipango Dr. Mwigulu Nchemba akizungumza na Clouds 360 asubuhi hii kuhusu Deni la Taifa amesema Tanzania ni nchi iliyo na sifa nzuri kimataifa, ikiwemo kuwa na uwezo wa kukopesheka pasipo vikwazo.

Akijibu swali la Mwandishi wa habari aliyetaka kujua kwanini anajisifu kuwa na uwezo wa kukopa huku deni la Taifa likizidi kukua, Dr. Nchemba amesema kuwa kukopesheka ni sifa nzuri tofauti na watu wanavyodhani.

“Kimsingi watu wengi wanadhaniaga siyo sifa, wanadhani labda siyo sifa. Kimsingi, kiuchumi, kiutaalam, kama nchi inaweza kukopesheka ni sifa moja kubwa kuliko nchi isiyoweza kukopesheka”

Amesisitiza kuwa ukiona nchi haikopesheki jua kuwa Nchi hiyo haina Serikali au imekopa hadi imefilisika hivyo haiwezi tena kukopesheka.

Ameongeza, “hata hapa Afrika Mashariki, mwekezaji yeyote sasa hivi, ndio maana mikutano mikubwa ikifanyika nje, Rais mmoja anayesumbuliwa sana duniani kugombewa appointments mpaka zinajaa ni Rais wa Tanzania kwa sababu nchi yake ipo properly maganed kwenye maswala ya uchumi. Mtu anaweza kuwekeza, hata sekta binafsi kukopeshwa kwake ni lazima nchi iwe na hizi sifa”

.............

Kuongezeka kwa deni la taifa kwa kiasi cha Shilingi 21 trilioni ndani ya miezi 6 kumezua tafrani na mijadala mikali kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari nchini Tanzania.

Taarifa ya uchumi ya mwezi Novemba 2022 iliyotolewa hivi karibuni na Benki Kuu ya Tanzania inaonyesha kuwa hadi kufikia mwezi Oktoba 2022 deni la taifa lilikuwa limefikia Shilingi 90.35 trilioni.

Alipokuwa akisoma Bajeti ya Serikali mwezi Juni, Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba alisema hadi mwezi Aprili 2022 deni la taifa lilikuwa limefikia Shilingi 69.4 trilioni

Hii inaonyesha wazi kuwa deni la taifa limeongezeka kwa kiasi cha Shilingi 20.91 trilioni kati ya Mwezi Aprili na Oktoba mwaka huu.
 
Sawa Dr. Luteni, Kanari Generali Field Marsha kiongozi mkuu Ndugu Mwigulu Lameck Nchemba PhD Mchumi Daraja la Kwanza.
 
Lakini mi nashangaa, watu wanachukulia poa lakini kuna wakati hata kupata hizi info ilikua mbinde
 
Nina mashaka kama sifa ya "kukopesheka" pekee iwe sababu ya kubebesha wananchi na vizazi vijavyo mzigo mzito wa madeni. Wiki hii tu Raisi wa Kenya ameonya kuhusu uzito wa mzigo wa deni la taifa lao. Wananchi wa Ugiriki na Argentina wameteseka sana kutokana na Deni la taifa. Wataalamu wa uchumi humu jf tafadhali watujuze zaidi.
 
Nina mashaka kama sifa ya "kukopesheka" pekee iwe sababu ya kubebesha wananchi na vizazi vijavyo mzigo mzito wa madeni. Wiki hii tu Raisi wa Kenya ameonya kuhusu uzito wa mzigo wa deni la taifa lao. Wananchi wa Ugiriki na Argentina wameteseka sana kutokana na Deni la taifa. Wataalamu wa uchumi humu jf tafadhali watujuze zaidi.
Hata Zimbabwe inakopesheka, tatizo la Tanzania ina viongozi wabovu sn
 
Mwigulu awe serious kwenye suala la deni la Taifa, ni suala la usalama wa nchi pia.
 
Back
Top Bottom