Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika Mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba Ni Daktari wa uchumi,Hakubahatisha kupata Firstclass ya uchumi pale UDSM, serikali haikukosea kumpatia kazi pale Benki kuu ya Tanzania yaani BOT, Mheshimiwa Daktari Mzee Jakaya Kikwete hakukosea kumpatia Unaibu waziri wizara ya Fedha, lakini pia Daktari Rais Samia Suluhu Hasssan hawakukosea wala kufanya kosa kumpa Uwaziri wa Fedha huyu Mwamba.
Huyu Mwamba anaujuwa uchumi, uchumi na kunanuni zake zipo kichwani mwake,anajuwa namna ya kueleza na kuelezea uchumi kwa lugha rahisi ya kueleweka hata kwa mtu ambaye hajasoma kabisa masuala ya Uchumi anamuelewa vizuri kabisa.
Akiwa Bungeni huku akishangiliwa na Bunge zima utafikiri Rais ameingia kuzindua Bunge ,ameelezea kwa undani na kwa ufasaha mkubwa sana juu ya Deni la Taifa na kwanini kama Taifa tunakopa na faida za kukopa.
Amesema ya kuwa Tanzania Tunakopa kwa sababu Tunaaminika na tuna uwezo wa kulipa mkopo wote,amesema ya kuwa Maskini hawezi akakopesheka kwa sababu ni ngumu kuaminika linapokuja suala la ulipaji,lakini sisi tunao uwezo wa kulipa na pia Deni letu ni himilivu.
Akasema tunakopa ili kutekeleza miradi mikubwa mikubwa na kimkakati ili kuimaliza ndani ya muda mfupi na kuanza kurejesha marejesho ya mkopo. Akasema mfano mradi wa SGR unaojengwa kutoka Dar mpaka kigoma kama tungesema tutumie makusanyo ya ndani, basi tungeweza kusubiri mpaka miaka 50 ndio tukamilishe jambo ambalo ni gumu sana, lakini ili uharakishe mradi unakwenda unakopa pesa na kumlipa mkandarasi ili akamilishe mradi ndani ya muda mfupi.
Mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba amesisitiza kuwa Nchi haikopi kwa ajili ya matumizi ya kawaida au anasa bali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ile mikubwa.na akasema ya kuwa kwa kadri unavyokuwa na uchumi mkubwa ndio unavyokuwa na Deni kubwa kwa sababu unakuwa na uwezo mkubwa wa kukopa kiasi kikubwa na kuaminika.akatolea mfano Nchi zenye utajiri mkubwa hapa Duniani ndio zenye madeni makubwa sana ukilinganisha na zile masikini.vivyo hivyo kwa mtu mwenye utajiri mkubwa na mabiashara makubwa atakuwa a deni kubwa ukilinganisha na yule mwenye kipato kidogo.
Akatolea mfano kuwa yeye deni lake haliwezi kuwa kubwa ukilinganisha na la Billionea josephu Kasheku Msukuma ambaye ni mfanyabishara mkubwa sana.
Kiukweli namuunga sana Mkono Mheshimiwa Mwigulu kwa NONDO kali Alizo zishusha Bungeni mpaka huku mitaani Watu wakasema kuwa huyu jamaa ni Mwamba kwelikweli wa masuala ya uchumi,na ndio maana uchumi wetu unaendelea kufanya vyema huku miradi mbalimbali ya maendeleo na kimkakati ikiendelea kutekelezwa vyema kabisa. Mheshimiwa Mwigulu kwa hakika wewe ni Mwamba wa uchumi kwelikweli na ndio maana Rais wetu mpendwa Anaendelea kukuamini kushikilia nafasi na wizara hiyo nyeti na moyo wa Taifa.
Angalia; mimi Lucas Hebel Mwashambwa siyo chawa wa mtu wala silipwi na mtu yeyote yule kumuandika humu jukwaani. Maana kumekuwa na katabia ka mtu nikimuandika utasikia mimi ni chawa wake mara nimehamia kwa fulani na kuhama kwa fulani. nilishasema mimi ni mzalendo na kuwaunga mkono wachapa kazi na wazalendo wa Taifa letu.
Niambie pamoja na Mheshimiwa Dkt Mwigulu kuwa katika nafasi nyeti ni lini umewahi kumsikia akihusishwa na scandal za rushwa? Ni wapi umewahi kumsikia akituhumiwa kuiba pesa za umma? Huyu ni msafi ,ni mtu clean kama ambavyo Watanzania wamekuwa wakimuita.ndio maana nimetumia vocha yangu kumuandika na siyo kununuliwa vocha.ukifanya vema mimi nakupa pongezi zako .sinaga wivu wala kinyongo wala chuki na mtu mimi.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.