Mwigulu Nchemba: Maskini Hakopi na Hakopesheki.Tunakopa Kwa sababu Tanzania ni Tajiri.

Mwigulu Nchemba: Maskini Hakopi na Hakopesheki.Tunakopa Kwa sababu Tanzania ni Tajiri.

Nchi zilizoendelea zinakopa lakini zina mifumo mizuri ya kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za mikopo vizuri.
Huwezi kusikia ripoti za CAG zilizosheheni ufisadi kwenye mabunge ya Marekani,China,Ulaya,nk harafu zikafunikwa na kuwekwa kabatini hivi hivi!
 
Anaposema Tanzania ni tajiri hamaanishi raia wote ni matajiri. Elewa maana ya neno "Tanzania ni tajiri"
 
Wewe chawa mwambie huyo boss wako abadilishe kauli.Iko hivi hakuna binadamu ambaye akopesheki.Ata hao maskini wako anaaminiana na wanakopeshana wao kwa wao.Kinachokufanya upate mkopo sio kua tajiri bali dhamana au makubaliano unayoweka kwaajili ya huo mkopo na kiwango cha mkopo.Wanaotukopesha wanaangalia watapata faida gani kutoka kwetu wakishatukopesha.Siku zote wanaokopesha ndio wanaonufaika zaidi kuliko wanaokopa ndo maana kukopa sana sio sifa.kwasababu unakopa kwasababu una upungufu na upungufu unatokana nakushindwa kuzalisha ziada.Ndo maana watu wanahoji matumizi ya hizo pesa zinazokopwa kila mara.
 
Back
Top Bottom