Mwigulu Nchemba: Mfumuko wa bei utashuka na bidhaa zitashuka. Asema mafuta yalipandisha bei

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba amesema tunakoelekea bidhaa zinaenda kushuka bei kwasababu zilipanda kuitikia kupanda kwa bei ya mafuta. Mwigulu amesema mafuta yamepungua kwa zaidi ya Tshs 400.

Mwigulu anaamini kwa jitihada za Rais Samia kuweka bilioni 100 kila mwezi itazidi kupunguza bei ya mafuta. Ametoa rai kwa watanzania, bidhaa walizoona zimepanda bei zitashuka kwasababu gharama za usafirishaji zitashuka.

Sisi tuliokuwepo wakati wa Vita ya Kagera tunakumbuka ile miezi 18 ambavyo haikuwahi kufika

Wanasiasa siyo wa kuwaamini sana bwashee
Nilikuwa nimemaliza form six and we went to Masaka straight from JKT. Nyerere alisema tufunge mkanda miezi 18, mpaka leo bado tumefunga mikanda. halafu mtu "mwongo" eti anataka kuwa mtakatifu
 
Tumaini la Watanzania lenye first class ya 4.9 na PhD ya uchumi limeongea. Nani atalibishia?

Na atakayelibishia ajiandae kuhamia Burundi maana hakuna namna!
JamiiForums63784684.jpg
 
Swali ni je hiyo bil 100 analipwa nani?

Nia ya kuweka Bl 100 ilikuwa ni kupunguza makali ya Bei kupanda.

Sasa Bei inashuka na bado Bl 100 inalipwa, nani mnufaika?

Au mnawalipa waagizaji mafuta Ili hata Bei zikishuka waendelee kuvuna JASHO letu?
 
Waziri kama yeye hatakiwi kutuambia "anaamini", anatakiwa awape NBS, BoT na UDSM kazi ya kuchata data halafu aje na kauli thabiti ya mfumuko wa bei utashuka kwa kiwango gani kwa muda gani.
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba amesema tunakoelekea bidhaa zinaenda kushuka bei kwasababu zilipanda kuitikia kupanda kwa bei ya mafuta. Mwigulu amesema mafuta yamepungua kwa zaidi ya Tshs 400.

Mwigulu anaamini kwa jitihada za Rais Samia kuweka bilioni 100 kila mwezi itazidi kupunguza bei ya mafuta. Ametoa rai kwa watanzania, bidhaa walizoona zimepanda bei zitashuka kwasababu gharama za usafirishaji zitashuka.

Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba amesema tunakoelekea bidhaa zinaenda kushuka bei kwasababu zilipanda kuitikia kupanda kwa bei ya mafuta. Mwigulu amesema mafuta yamepungua kwa zaidi ya Tshs 400.

Mwigulu anaamini kwa jitihada za Rais Samia kuweka bilioni 100 kila mwezi itazidi kupunguza bei ya mafuta. Ametoa rai kwa watanzania, bidhaa walizoona zimepanda bei zitashuka kwasababu gharama za usafirishaji zitashuka.

Pamoja na U-Turn unazopiga nw,

Bado hutanusurika na SHOKA lililolengwa shingoni mwako kukufurusha ktk kiti ulichokalia.
 
Mwigulu amezaliwa kwenye familia ya kitajiri amekuta kwao maghorofa, magari na supermarket ndiyo maana Hali ngumu za watanzania anaona poa tu.
 
Mwigulu amezaliwa kwenye familia ya kitajiri amekuta kwao maghorofa,magari,na supermarket ndiyo maana Hali ngumu za watanzania anaona poa tu
Mwigu ametokea family maskini ndomana ana DHARAU.

Mbowe ameukuta utajiri na Hana DHARAU, maskini akipata ghafula pesa wengi hurukwa na akili.
 
Back
Top Bottom