Mwigulu Nchemba, Mnalofanya Serikali ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za kodi na mnadhani Watanzania hawaelewi

Waziri wa fedha ambae hajui hata idadi ya Watanzania ambao ni walipa kodi,jana kasema wapo million 55.Yaani amejumuisha hadi watoto!πŸ’πŸ’πŸ’
Hahahah! Sijaisikia hii Mkuu. Yaani First Class degree ya uchumi UDSM, PhD Class, anasema idadi ya walipa kodi Tanzania ni 55 milioni😳😳😳
 
So, what we have to do now?

Nadhani leo Ijumaa tarehe 18/06/2021 ndiyo wanahitimisha mjadala wa bajeti kuu na ni obviously wataipitisha kama ilivyo pamoja na makosa haya...
 
Ili kuepuka labda serikali kufunguliwa mashitaka ya kikatiba juu ya suala la kutoza kodi mara mbili kwa huduma ileile, wakadhani ni akili sana kuiita hii kodi ya pili "Kodi ya Laini ya Simu". Lakini hii si kweli, hii sio kodi ya laini za simu
Basi iite kodi ya uzalendo. Thread closed!
 
Mantiki/maana itabaki kuwa ileile vyovyote vile itakavyosomeka...

Just see;

".....Mnalofanya serikalini ni ukiukwaji wa kanuni za sheria za kodi....."√√√√

na

".....Mnalofanya serikali ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za sheria za kodi....."√√√


Mimi naona all the same..
 
Kuna ile railway levy inayokatwa kwenye kodi ya kuingiza magari miaka nenda rudi sasa, lakini utaambiwa hakuna pesa za kukamilisha mradi wa SGR hadi wanahaha kuitafuta kwenye line za simu......na tayari wameshakopa pesa kibao, huu unakuwa kama ni uzwazwa fulani hivi....
 
Kila mtu ataguswa na hili na ndipo akili zitakaa sawa
 
Nimishamuona mtu anajinasibisha na matai sijui skafu za bendera ya tanzania huwa napoteza imani nae kabisa
 
Dr Mpango ndiye mzee wa field katika maswala ya fedha . Yaani ingewezekana wangebadilishwa huyu awe kule. Lakini kukitokea la kutokea maana yake Mwigulu atashika usukani. Mmh ni kheri yabaki kama yalivyo.
Leo umetoa boko
 
Mwigulu na Zungu sijui wamewaza kwa kutumia kitu gani? yaani laini nilinunua miaka mingi na kodi wakachukua, Leo tena wanataka waanze kuniuzia mali yangu kila siku?
 
Inaumiza sana aiseee halafu pesa karibu nusu yake inaenda kwenye posho zao hali ya kuwa Mishahara yao ni kufuru.
 
Inasikitisha sana MBUNGE anapata MSHAHARA wa Sh.Mil.11 na KIINUA MGONGO cha Sh.Mil.200 na Hakatwi KODI na huo Mshahara na Kiinua Mgongo ni KODI za WANANCHI leo Anasimama MBUNGE na Kudai Wananchi Wakatwe KODI ya UZALENDO .Kama ni UZALENDO anzeni nyinyi WABUNGE wenye MISHAHARA ya MAMILIONI Kukatwa Pesa na Ziende kwenye MIRADI ya MAENDELEO Majimboni Kwenu Huo Utakuwa UZALENDO.Wananchi Wanyonge na Masikini Mnawarundikia UTITIRI wa KODI nyinyi MNASTAREHE kwa MISHAHARA MINONO na MAGARI Mazuri Hebu Waoneeni Huruma Wapiga KURA
 
Hizo kodi ziongezwe mara 20 ili kuwakomoa mataga
Hapo hukomeshi MATAGA maana wao mishahara yao milima na miposho kibao TATIZO ni kwa akina Crimea wenye mishahara ya laki nne.
 
So, what we have to do now?

Nadhani leo Ijumaa tarehe 18/06/2021 ndiyo wanahitimisha mjadala wa bajeti kuu na ni obviously wataipitisha kama ilivyo pamoja na makosa haya...
Kwa sababu wao haiwaathiri kwa sababu ya mishahara yao shida ipo mtaani.
 
Mkuu hayo ndio maisha. Hata wabunge wakisema tulime kwa bidii tuwe na chakula cha kutosha hawajui hata jembe linashikwaje!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…