Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Thread starter
- #41
Mwambie kwa Kiingereza Mkuu ili asikasirike; intellectually disabledHii ni dalili No.3 ya mtu aliyefilisika kimawazo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwambie kwa Kiingereza Mkuu ili asikasirike; intellectually disabledHii ni dalili No.3 ya mtu aliyefilisika kimawazo.
Hahaha, Mkuu itabidi tumuulize Mzee Mwinyi.Mantiki/maana itabaki kuwa ileile vyovyote vile itakavyosomeka...
Just see;
".....Mnalofanya serikalini ni ukiukwaji wa kanuni za sheria za kodi....."√√√√
na
".....Mnalofanya serikali ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za sheria za kodi....."√√√
Mimi naona all the same..
Usiwe unakurupuka wewe mbuzi,kodi ya kila line ni 10-200 na unayoisemea wewe ni kodi ya miamala ya kifedhaMwigulu Nchemba, ambaye siku zote ametueleza kwamba yeye ni mchumi mbobezi aliefaulu degree yake ya uchumi pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa daraja la kwanza, anakuja kutufafanulia Watanzania kwamba serikali imefanya ufikirio saa katika suala la kodi ya laini ya simu ili isiwaumize Watanzania. Kimsingi huo si ukweli.
Kama Mwigulu alifanya vizuri kama anavyodai katika degree yake ya uchumi, basi atakumbuka kwamba kanuni moja ya msingi katika kodi ni kwamba huwezi kumtoza kodi mnunuzi mara mbili kwa huduma au bidhaa ileile. Huo ni unyanyasaji au wizi wa kiserikali.
Sasa Mwigulu na serikali kwa makusudi kabisa, wameamua kututoza watanzania kodi ya kununua airtime au data katika huduma za simu mara mbili, halafu wanaona ni sawa. Kumbuka kwamba kila unaponunua airtime, lazima ulipe VAT - ambayo ni kodi. Na sasa juu ya hii VAT, Mwigulu na serikali wanakuja na kodi nyingine, kati ya Shs 10 hadi shs10,000. Hii ni kodi, na wamekiri hivyo.
Ili kuepuka labda serikali kufunguliwa mashitaka ya kikatiba juu ya suala la kutoza kodi mara mbili kwa huduma ileile, wakadhani ni akili sana kuiita hii kodi ya pili "Kodi ya Laini ya Simu". Lakini hii si kweli, hii sio kodi ya laini za simu. Ingekuwa hivyo ingepaswa kukatwa pale unaponunua line ya simu. Huko ni kutumia technicalities kupotosha ukweli. Hii kodi ni juu ya kitu kile kile ambacho kinatozwa kodi kama VAT - kununua airtime au data, in essence doubl taxation, na ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za kodi. Na kama ingekuwa ni "line service charge" isingepaswa kubadilika kutegemea kiasi cha airtime au data unachonunua, ingebaki palepale, fixed amount.
Najua huenda walifikiria kuiita hii kodi "levy" badala ya "kodi". Lakini sasa, Mwigulu na serikali walijua wazi kwamba ikiwa wangeiita levy, basi matumizi ya mapato ya hiyo levy yangepaswa kuwa ndani ya sekta ya mawasiliano - yaani ring-fenced. Kanuni za levy zinataka ukitoza levy basi mapato yake yaende kuboresha huduma ndani ya sekta hiyo levy inapokatwa. Mfano, huwezi kukata levy ya road maintanance kwenye mafuta, halafu uchukue fedha kuzipeleka kulipa mishahara ya serikali ya bara na visiwani.
Na kama ingekuwa "line service charge" serikali ilijua wazi basi ingepaswa kunufaisha pia kampuni za simu, sio kwenda serikalini. Hilo serikali iliona kabisa haiwezekani.
Na sijui kwa nini waliona aibu kusema ni levy badala ya kodi ya laini ya simu, kwa kuwa serikali haijawahi kuwa na aibu ya kutumia makato ya levy kwa kitu kisichokusudiwa. Angalia kwa kila lita ya petroli na dizeli kuan levy ya road mainatance, mabilioni ya shilingi kila siku, lakini serikali bila aibu inachukua hizo fedha na kuzipeleka kwenye matumizi yasiyohusika kabisa na barabara, na kutojali kwamba barabarani kuna mashimo ambayo yanasababisha ajali zinazoharibu magari na hata kuleta vifo. Hawajali. Mashimo yanabaki barabarani hata mwaka mzima, wakati fedha za angalau kuyafukia tumeshalipa!
Kuna levy pia kwenye vitu kama bill za umeme, kwa ajili ya kuwapa REA kusambaza umeme vijijini. Lakini mtu akikuambia hiyo levy imetumika kwenye gharama za uchaguzi wala usishangae.
Kwa hiyo Mwiguli Nchemba, tunawaambia wazi. Mnachofanya ni ukiukwaji wa taratibu za kodi na msidhani kwamba hatuoni. Mnaiita kodi ya laini ya simu lakini ni kodi inayokatwa kwa kununua airtime au data ambazo tayari zina kodi - VAT. Na tunajua kwa nini mmeogopa kuiita levy, kwa kuwa kama ni levy basi haipaswi kutumika kulipia mishahara na posho nyingi za wabunge, na mlishindwa kabisa kuuelewa kama mkiita levy mtasema ni levy kwa ajili ya nini na ingewabana kikatiba kuingiza hizo fedha kwenye matuizi yenu yasiyo na tija na suala la mawasiliano.
You can fool some people sometimes, but not all the people all the times.
Weka vyanzo vyako hapaNasubiri kuona kama hizi tozo zao zitadumu mpaka 2025! Kwa aina hizi za tozo, ni wazi serikali yetu imeishiwa vyanzo vipya na rafiki vya kukusanya mapato.
Kinachokera ni kwa upande wao kuto onesha kabisa dalili za kupunguza matumizi yao ya kila siku! Wabunge bado wanajilipa mabilioni ya shilingi kila mwezi kama posho na mishahara, serikali bado inachezea tu fedha za walipa kodi kwa kulipia vyeo visivyo na tija kama vile vya Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Ma Ras, Ma Das, nk! Ma V8 bado yanaendelea kununuliwa kila siku!
Achana na hao mbuzi ni bora itozwe na ikafanye malengo yake,ukisikiliza kila kenge hutofanikisha lolote.Inafaa itaongeza barabara zitakazojengwa na majimbo kupata mil 600. Najaribu kujiuliza mil 600 zitaleta balaa gani huko mitaani kwa wana siasa
Weka cha maana alichofanya kama sio kutegemea mikopo na kupora watu fedha.Dr Mpango ndiye mzee wa field katika maswala ya fedha . Yaani ingewezekana wangebadilishwa huyu awe kule. Lakini kukitokea la kutokea maana yake Mwigulu atashika usukani. Mmh ni kheri yabaki kama yalivyo.
Halafu na zile posho nene mlizolipana wakati mnaandaa hizo tozo zenu, utanigawia?Weka vyanzo vyako hapa
Hujui kitu nchi sio familia yako ambayo unawaza kula kulaa kunya basiKuna ile railway levy inayokatwa kwenye kodi ya kuingiza magari miaka nenda rudi sasa, lakini utaambiwa hakuna pesa za kukamilisha mradi wa SGR hadi wanahaha kuitafuta kwenye line za simu......na tayari wameshakopa pesa kibao, huu unakuwa kama ni uzwazwa fulani hivi....
Acha unyumbu wako hujui hata unaongea nini zaid ya kuropokaInaumiza sana aiseee halafu pesa karibu nusu yake inaenda kwenye posho zao hali ya kuwa Mishahara yao ni kufuru.
Hoja sio kuondoa hiyo kodi bali hoja ni kudai hao wabunge nao walipe kodiInasikitisha sana MBUNGE anapata MSHAHARA wa Sh.Mil.11 na KIINUA MGONGO cha Sh.Mil.200 na Hakatwi KODI na huo Mshahara na Kiinua Mgongo ni KODI za WANANCHI leo Anasimama MBUNGE na Kudai Wananchi Wakatwe KODI ya UZALENDO .Kama ni UZALENDO anzeni nyinyi WABUNGE wenye MISHAHARA ya MAMILIONI Kukatwa Pesa na Ziende kwenye MIRADI ya MAENDELEO Majimboni Kwenu Huo Utakuwa UZALENDO.Wananchi Wanyonge na Masikini Mnawarundikia UTITIRI wa KODI nyinyi MNASTAREHE kwa MISHAHARA MINONO na MAGARI Mazuri Hebu Waoneeni Huruma Wapiga KURA
Afu utekaji utatamalaki upyaa🙄Dr Mpango ndiye mzee wa field katika maswala ya fedha . Yaani ingewezekana wangebadilishwa huyu awe kule. Lakini kukitokea la kutokea maana yake Mwigulu atashika usukani. Mmh ni kheri yabaki kama yalivyo.
I say kuna watu wajinga na hawajui kuwa ni wajinga. Ndio kwanza umeamka? Unajua maana ya miamala ya kifedha?Usiwe unakurupuka wewe mbuzi,kodi ya kila line ni 10-200 na unayoisemea wewe ni kodi ya miamala ya kifedha
Hivi unachanganya bangi unayovuta na kitu gani, mavi ya nguruwe?Acha unyumbu wako hujui hata unaongea nini zaid ya kuropoka
Usiwe unakurupuka wewe mbuzi,kodi ya kila line ni 10-200 na unayoisemea wewe ni kodi ya miamala ya kifedha
Imeongezwa kama walivyoongeza 100 kwenye mafutaKama ni kodi ya line ingekatwa wakati wa kununua line... Ukisema tulipe Kodi ya matumizi ya line hiyo ipo na inakatwa kupitia vat ktk kununua vocha..
Kila mtu ataguswa na hili na ndipo akili zitakaa sawa
Sasa kama Waziri mwenyewe tu wa hiyo Wizara amekaa kipigaji pigaji tu! Unategemea nini!!! Zitapigwa tu.Hii Kodi ni wizi kuwaaibia wananchi pesa na kwenda kutumia ktk matumizi yasiyokuwa ya msingi...