Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Nilisiliza maelezo ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba Bungeni kuhusu mikopo umiza na wanaofanya biashara ya kukopesha bila leseni, na pia nimesoma tangazo la Benk Kuu(BoT) la tarehe 13/05/2024 linalopiga marufuku kufanya biashara ya kukopesha mitandaoni bila kuwa na leseni, nimebaki kushangaa na kujiuliza inawzekana vipi biashara hii inafanywa kupitia menu za makampuni ya simu halafu mamlaka husika zinashindwa kuwabaini hawa wahalifu?
Nilitegemea changamoto iwe ni kusimamia sheria kwenye ku-deal na taasisi na watu binafsi wanaofanya hii biashara kwa kificho huku mitaani lakini sio haya makampuni ya mitandaoni yenye kutumia application zao mitandaoni kutoa mikopo na kulipwa madeni yao kupitia menu za makampuni ya simu tena bila kificho.
Kama kweli Mwigulu na BoT wako serious, basi kwa kushirkiana na Jeshi la Polisi, wangeanza na makampuni ya simu katika kuwabaini wahusika wa hii biashara kwani kupitia menu za mitando ya simu(Mpesa, tigo pesa na Airtel Money), makampuni haya hulipwa na wateja wao na hata app za baadhi ya haya makampuni zimetangaza option mbalimbali za kuwalipa ikiwemo kupitia huduma hizo za Mpesa, tigo pesa na Airtel Money.
Sasa ndio najiuliza, wanashindwaje kuanza na haya makampuni ya simu kuwasaka hawa watu?
Sometimes napata wasiwasi huenda hii biashara ni ya vigogo huko serikalini na ndio maana kuna kigugumizi cha kuchukua hatua.
Tuna safari ndefu sana watanzania katika kuitafuta nchi ya ahadi.