Mwigulu Nchemba, tafadhali kafute mabango yako barabarani!

Mwigulu Nchemba, tafadhali kafute mabango yako barabarani!

John una vituko sana! Sasa nini sababu ya kum cc Wakudadavuwa? Hujui alishatemwa toka anyang'anywe ofisi na Kange? Usicheze na Wakudadavuwa katika maslahi! Yeye anataka matawi ya juu mwenzake.
Anyway tuache hayo, kwa nini usimshauri ale dili na jasusi ili yale matangazo amuuzie hati miliki wanafuta jina la Mwigulu tuu na kuchomeka Rais 2020 Bernard?
Atajipatia posho ya hatimiliki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaaaaa........ halafu mwandiko ni ule ule kwenye madaraja yote kuanzia Mtwara hadi Bukoba!
 
Labda anayegombea ndio afanye hiyo kazi maana ni rahisi kupata ufadhili au kuingia mfukoni ikiwa unagombea au kama una nia ya kugombea.
Ule ni uchafuzi wa mazingira anaweza kulazimishwa na sheria kuyafuta.

cc: Zungu!
 
Haa
IMG_20200131_104737.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vyema wakaanza kutozwa kodi, iko wazi Tangazo lolote la biashara lazima litozwe kodi.
TRA wapite nchi nzima wapigie hesabu idadi yake na mwisho wasiku wammpe tax bill yake na hesabu ianzie toka 2015 mpaka leo, Akishindwa kulipa afilisiwe na asiruhusiwe kugombea nyadhifa yeyote na kuwa mtumishi wa umma.
 
BARUA YA WAZI KWA MHE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI.

Mhe Rais nakusalimu katika Jina bwana wetu yesu kristo, Jina la bwana lihimidiwa Sana, tumeona ulivyomkiri kristo kuwa bwana na mwokozi wa maisha yetu Katika kipindi hiki kigumu.
Tunaendelea kumwomba atuepushe na hili janga la ugonjwa wa COVID-19.

Mhe Rais watanzania na Dunia tunatambua Kazi kubwa unayoifanya katka Taifa letu ya kuwaletea watanzania maendeleo
Mungu akubariki Sana

Toka mwaka 2015 tulikupa dhamana ya kututumikia Sisi
Na unafanya hivyo

Tumeshuhudia miradi mikubwa ya maendeleo ikitekelezwa
Chini ya uongozi wako

Mhe Rais tunafahamu yakuwa wewe ndiye mkuuu WA nchi, Amiri Jeshi mkuuu.
RAISI wetu mpendwa
Tuliyekuchagua kwa kura zote.

Sasa Kuna Jambo linatuchefua Sana Sisi wananchi wako
Tuliokupa dhamana
Uwe Rais wetu
Toka mwaka 2015.

Kuna huyu kijana, mbunge WA JIMBO la Iramba magharibi
Anaitwa MWIGULU NCHEMBA

Mhe Rais kila tunaposafiri nchini kote
Tunakutana na Mawe njiani yameandikwa
MWIGULU RAIS!!

Mara kwenye madaraja
Mara kwenye miti
Kimsingi hili Jambo limekuwa likitukera Sana Sisi watanzania wazalendo kwa nchi yetu
Kwani tunaye Rais wetu Dr John pombe magufuli
Sasa hii Habari ya Mwigulu Rais inatoka wapi, tunaudhika Sana kuona mambo ya hovyo hovyo kufanywa na huyu kijana.

Huyu kijana ni miongoni mwa viongozi waliokuwepo katika serikali zilizopita
Na Ndio waliotuharibia nchi na magenge Yao
Wamekuwa ni watu WA kudhani kuwa wao ni ZAIDI YA CCM

Mhe Rais ulimpa nafasi katika serikali hii tukufu
Akaishia kufanya mambo ya hovyo hovyo wizarani
Mpka kupelekea kumpumzisha Kazi

Hivi sasa kumeibuka mambo mengi kutokea Jimboni kwake,
Amekuwa akitumia ubunge wake kufanya mambo ya hovyo hovyo
Kudhalilisha viongozi, kuchonganisha serikali na wananchi etc

Ombi letu mhe Rais
Kwa kuwa Alikuwa waziri WA mambo ya ndani ya nchi akashindwa hata kuwaomba Makamanda wote WA Jeshi la police kutumia hata wafungwa kufuta huo uchafu kwenye Mawe yetu
Akaanza kuwapeleka kufyeka bangi huko Arusha Jambo ulilolikemea wazi wazi

Sasa toa maelekezo kwa baraza la mazingira nchini nemc
Wamwandikie barua
Afute Mara moja
HUO uchafu.

Kama aliweza kutumia m30 kuandika nchi nzima
Hawezi kushindwa kutumia m30 kusafisha Mawe yetu
Maana wapiga kura wako tunakereka Sana kuona huo uchafu
Ikiwa tunae Rais wetu kipenzi cha Watanzania

Mwisho, mhe Rais watanzania tunakupenda
Tunakuamini
Tunakuombea

Naitwa Mwaipopo Jeka
Tukuyu mbeya
 

Attachments

  • FB_IMG_15867997808272711.jpg
    FB_IMG_15867997808272711.jpg
    34 KB · Views: 3
Back
Top Bottom