Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo Dkt. Mwigilu Nchemba alisamama kuhitimisha hoja ya mapendekezo ya mpango wa tatu wa maendeleo ya Taifa wa miaka mitano kwa mwaka 2021/22 hadi 2025/26 kwa niaba ya wizara ya fedha na wabunge kujadili kwa takribani siku tano. Pamoja na mambo mengine amefafanua hoja chache ikiwemo mjadala wa tafsiri ya uchumi wa kati, maana yake na kwa mwananchi mmoja mmoja.
Mwigulu Nchemba: Utaratibu wa kuingia uchumi wa kati ni utaratibu ambao unazingatia vigezo, Tanzania kuingia uchumi wa kati haikutuma maombi kwamba tunaomba na sisi tuwe nchi ya kipato cha kati, hatukufanya application na wala Tanzania haikulipia.
Ni jambo linalozingatia vigezo tena vigezo vyenyewe vimezingatiwa na taasisi kubwa zinazoheshimika duniani, World Bank, IMF na wachumi wote ambao wameitangaza Tanzania ni ya uchumi wa kati wala sio washabiki wa CCM, ni taasisi za wasomi waliobobea na hawajaanza kwa kuitangaza Tanzania, zipo nchi ambazo zimewahi kufika kule na zimefika kule kwa kuzingatia vigezo.
Angalia nchi inayoweza kulipia takribani bilioni 700 kulipia watoto kwenye elimu ya juu, tunaita mikopo lakini kimsingi ni bajeti ya serikali kwasababu hawakopi benki hawa, ni bajeti ya serikali. Mambo mengi yamebadilika hata jana tu Simba kushinda kule ni uchumi wa kati ndio maana hawakuwahi kushinda siku zilizopita, viwango vyao vilikuwa vya kiuchumi wa kati.
Wale wapiga ramli wanaosema hatutaweza, niwaambieni tunasonga mbele haturudi nyuma, tunakwenda Kaanani.
======
Kuhusu deni la Taifa, Mwigulu amesema viashiria vyote vinaonesha deni ni himilivu akitoa mfano deni la nje kwa pato la Taifa ukomo wake huwa ni aslimia 55 ilhali Tanzania ipo asilimia 17.3