Mwigulu Nchemba: Tozo zina machungu, lakini lazima tuendelee nazo

Mwigulu Nchemba: Tozo zina machungu, lakini lazima tuendelee nazo

Munajenga madarasa yapi na zahanati zipi maana huku mtani tunachangaishwa hela za kujenga vituo vya afya zahanati na madarasa. Sasa nyie munajenga yapi au wapi? zile za UVIKO mulitudanganya tena munajenga madarasa mmh Mwigulu and Samia Must Go
 
Siamini kama huyu ni Mwigulu ninayemfahamu, anakuja na hoja nyepesi sana kutetea uozo, nakumbuka mwaka 2015 wakati anatangaza nia ya kugombea urais pale ukumbi wa Chuo Cha Mipango Dodoma nilikuwa mmoja wa Watu waliokuwa wanamuunga mkono na alikuwa na sera zenye mashiko.

Hii Nchi imefika wakati ambao Wasomi wanashindwa kuisaidia Nchi na badala yake wanatetea nafasi zao na matumbo yao tu, hivi leo unategemea kuendesha Nchi kwa kumkamua Mwananchi masikini? Haya Matozo ni zaidi ya Kodi ya kichwa iliyokuwa ikitozwa miaka ya nyuma.

Usimamizi mbovu wa Fedha za umma, matumizi makubwa ya Serikali, ukusanyaji mbovu wa Kodi hasa kwa Makamouni makubwa na kufungua mipaka ya kuuza mazao nje ya Nchi bila kujali akiba iliyopo ndiyo chanzo cha haya magumu tunayopitia katika Serikali hii ya awamu ya sita.

Hivi sisi Watanzania masikini tumeikosea nini hii Serikali ya awamu ya sita? Kuna Bibi kule kijijini ameshindwa kununua Umeme wa LUKU kutokana na hizi Tozo, aliwekewa Umeme wa 5000 alipotembelewa na mjukuu wake tangu mwezi wa kumi mwaka jana, ule Umeme ndiyo umeisha mwezi wa nane mwaka huu, kutokana na gharama za Tozo anatakiwa aweke zaidi ya 10,000 ili kupata huduma hiyo ilihali hata Pesa ya kununua chakula ni tatizo kwake, na nyumba yenyewe anayoishi ni ya udongo, ifike sehemu Rais na Serikali yake wajitathimini kwa haya.
 
Serikali hii imekosa ubunifu wa vyanzo vya Mapato, hii ni zaidi ya Kodi ya kichwa tulizokuwa tunatozwa miaka ya nyuma, hii haikubaliki hata kidogo.
 
Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema kuwa kiasi kikubwa cha pesa zinazokusanywa kwenye tozo zinarudi kwa wananchi wenyewe kupitia shughuli za uzalishaji mali.

Ametolea mfano wa fedha zinazotolewa kwenye kilimo na wamachinga, pia amesisitiza kuwa pamoja na machungu ya tozo hizi, ni lazima watanzania tujifunge mkanda kuzikabili ili tuuvunje mnyororo wa umaskini.

Kupitia tozo hizi, Serikali inapanga kuongeza vituo vya afya, kujenga zaidi ya madarasa 8000 mwaka huu ili kuziba pengo lililopo kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi nchini.
 
Mwigulu nahisi ana maslahi na hizo Tozo huenda maana kitaifa kwetu ni maumivu makali. Kushabikia Tozo ilihali nje mnakopa kuja kujenga vyoo na madarasa na Tozo nazo mnasema ni za vyoo na madarasa na zahanati.

Kusema makusanyo ni bei gani kwa mwezi hamtaki mnatuzeveza tu. Hii nchi haiwezi endelea kama kila mtu ataruhusiwa kujidokolea hela za umma atakavyo.

Magufuli aliwanyoosha sana yani japo mlimuita mwizi ila ni aheri mtu anaekula na kipofu bila kumshika mkono. Hata kama alidokoa ila mambo ya maendeleo yalifanyika ya kuonekana kwa macho. Awamu hii kumalizia waliyoyakuta yanaendelea tu ni mtihani.
 
Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema kuwa kiasi kikubwa cha pesa zinazokusanywa kwenye tozo zinarudi kwa wananchi wenyewe kupitia shughuli za uzalishaji mali.

Ametolea mfano wa fedha zinazotolewa kwenye kilimo na wamachinga, pia amesisitiza kuwa pamoja na machungu ya tozo hizi, ni lazima watanzania tujifunge mkanda kuzikabili ili tuuvunje mnyororo wa umaskini.

Kupitia tozo hizi, Serikali inapanga kuongeza vituo vya afya, kujenga zaidi ya madarasa 8000 mwaka huu ili kuziba pengo lililopo kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi nchini.

I feel like ungrily skinning this bastard alive [emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]
 
Nikweli, mwigulu katoka mbali,
JamiiForums-1281529247.jpg
 
Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema kuwa kiasi kikubwa cha pesa zinazokusanywa kwenye tozo zinarudi kwa wananchi wenyewe kupitia shughuli za uzalishaji mali.

Ametolea mfano wa fedha zinazotolewa kwenye kilimo na wamachinga, pia amesisitiza kuwa pamoja na machungu ya tozo hizi, ni lazima watanzania tujifunge mkanda kuzikabili ili tuuvunje mnyororo wa umaskini.

Kupitia tozo hizi, Serikali inapanga kuongeza vituo vya afya, kujenga zaidi ya madarasa 8000 mwaka huu ili kuziba pengo lililopo kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi nchini.
Amedhihirisha kuwa yupo gizani anaishi na kufanya kazi kwa kupapasa kama vipofu
 
Back
Top Bottom