Siamini kama huyu ni Mwigulu ninayemfahamu, anakuja na hoja nyepesi sana kutetea uozo, nakumbuka mwaka 2015 wakati anatangaza nia ya kugombea urais pale ukumbi wa Chuo Cha Mipango Dodoma nilikuwa mmoja wa Watu waliokuwa wanamuunga mkono na alikuwa na sera zenye mashiko.
Hii Nchi imefika wakati ambao Wasomi wanashindwa kuisaidia Nchi na badala yake wanatetea nafasi zao na matumbo yao tu, hivi leo unategemea kuendesha Nchi kwa kumkamua Mwananchi masikini? Haya Matozo ni zaidi ya Kodi ya kichwa iliyokuwa ikitozwa miaka ya nyuma.
Usimamizi mbovu wa Fedha za umma, matumizi makubwa ya Serikali, ukusanyaji mbovu wa Kodi hasa kwa Makamouni makubwa na kufungua mipaka ya kuuza mazao nje ya Nchi bila kujali akiba iliyopo ndiyo chanzo cha haya magumu tunayopitia katika Serikali hii ya awamu ya sita.
Hivi sisi Watanzania masikini tumeikosea nini hii Serikali ya awamu ya sita? Kuna Bibi kule kijijini ameshindwa kununua Umeme wa LUKU kutokana na hizi Tozo, aliwekewa Umeme wa 5000 alipotembelewa na mjukuu wake tangu mwezi wa kumi mwaka jana, ule Umeme ndiyo umeisha mwezi wa nane mwaka huu, kutokana na gharama za Tozo anatakiwa aweke zaidi ya 10,000 ili kupata huduma hiyo ilihali hata Pesa ya kununua chakula ni tatizo kwake, na nyumba yenyewe anayoishi ni ya udongo, ifike sehemu Rais na Serikali yake wajitathimini kwa haya.