Mwigulu Nchemba: TRA inatimiza wajibu wake vizuri, wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi ipasavyo!

Mwigulu Nchemba: TRA inatimiza wajibu wake vizuri, wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi ipasavyo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa katiba na sheria Dr Mwigullu Nchemba amewajibu wabunge wa CCM wanaoilalamikia TRA kwamba taasisi hiyo inatimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Mwigullu Nchemba amesema katika serikali iliyopita wakati akiwa Naibu waziri wa fedha uchumi wetu uliendeshwa kwa kodi za watumishi wa umma kwani wafanyabiashara hasa wakubwa walikuwa hawalipi kodi kabisa. Wafanyabiashara walikuwa wanakimbilia bodi ya rufani za kodi kujificha lakini awamu hii mambo ya konakona hayapo tena, amesema Mwigullu.

Ikumbukwe kuwa wabunge wa CCM wakiongozwa na Nape Nnauye na Joseph Musukuma walidai kuwa TRA inawaonea wafanyabiashara kwa kutumia task force badala ya wataalamu wa kodi.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!
 
Swadakta Mhe. Waziri, kuna watu wameumbiwa kulalamika tuuuu! Kama unajua wajibu wako TASK FORCE itadunda kwakua Kila watakapoweka mitego watakuta uko vizuri.

Ila wale wafanyabiashara janja janja, unanunua Mali ya milioni 30 unaandikiwa Risiti ya milioni Moja wacha wafungiwe tu maana namna hakuna.

Nimewahi kuleteana Sana shida na Cashier wa duka Moja mtaa wa Tandamti ameniuzia kiatu cha elfu 90 halafu namdai risiti ananiambia mashine mbovu. Nikamwambia basi nirudishie fedha yangu. Ghafla mashine ikapona na nikapewa Risiti.

Hawa ndio watu Nape anawatetea yaani bureee kabisa. Mabarabara, Mishahara, Madawa vitanunuliwa kwa fedha toka wapi Sasa?
 
Nisaidieni kuniulizia Mwigulu Nchemba kama ameshawahi kufanya biashara yeyote Tanzania hii ya awamu ya tano.

Siku hizi TRA hawana simile kabisa. Kama ulikuwa unadaiwa nao then mzigo ukaonekana kwenye akaunti yako faster wanaukata juu kwa juu 😭😭
 
Kwa ninyi wajinga wajinga hamumuoni leo Mkuu wa Mkoa wa DSM akilalamika kuwa Dubai ya East Africa, Kariakoo imepotea.
Wateja wake toka Malawi, Zamia, Congo na mikoani wamekimbia kutokana na harrassment ya TRA.

Mpato ya kodi ya matrilioni yamepotea
Hayo yachukueni kama mafanikio.
 
ngoja nifanye fitna
Mwaga mtama ili nae tumharishie vizuri madudu yake.

Hayo mabus yanapita njia ya kati "Dar - Singida - Mwanza/Geita". Kesho nenda katume hata bahasha empty halafu uone kama unapewa risiti EFD, au nenda kakate ticket ya bus uone kama unapewa risiti za elektronik.

Unapewa risiti kama gazeti la udaku. Nchi hii utalipa kodi wewe na mimi kajambanane maisha mguu upande mguu sawa geuka kushoto, ila vigogo wa CCM bado wanakujuana ndani ya mikoa yao.
 
Kuna watu watapotea mapema mno baada ya JPM kuondoka madarakani mmojawapo ni huyu Mwigulu
Mwigulu anajua kucheza na saikolojia ya viongozi wa juu yake mpaka mda huo utakapofika ipo hoja ataitoa kwa wakati huo ambayo itakufurahisha sanana utakuja kuona hakika huyu ndiye mtu sahihi haswa A game of playing with human brain
 
Mimi naamini ipo siku moja Watanzania wote kwa kauli moja tutaafikiana kuna mahali tumekosea, TRA indeleeni kufanya munayofanya ila naamini nanyi pia mupo kwenye hii boti.
 
Unajua practical is better than theory..., aache kazi huko aingie mtaani afanye biashara ili alipe hio Kodi ipasavyo....

Hii serikali bana..., imejitoa kwenye ajira, imejitoa kwenye kila msaada kwa raia wake..., hao hao wanaoajiri wananchi zaidi (anasema ndio hawalipi kodi wana kona kona).., okay sio mbaya hao wanaokusanya kodi watuonyeshe zinafanya nini na sio long term projects but short term...

Watu wanataka uhakika wa malazi, mavazi na uhakika wa chakula..., jambo ambalo percent kubwa hawana..., tunadanganyana elimu bure wakati watu hata guarantee ya kupata mkopo (sio grant) wa kwenda chuo hawana na wakimaliza hakuna guarantee ya ajira (ukiwauliza wanakwambia jitafutie mwenyewe)..., sasa sijui wanafanya nini huko..., wote watoke huko tuje kitaa tutafute wenyewe na kila mtu ale kodi zake anazojitafutia...., na hayo madini, utalii n.k. tugawane pasu pasu bila kusahau kizazi kijacho.....

Hii nchi ya imejaa Wasanii...., nashangaa kwanini Bongo Movie sio kama Hollywood....
 
Back
Top Bottom