Swadakta Mhe. Waziri, kuna watu wameumbiwa kulalamika tuuuu! Kama unajua wajibu wako TASK FORCE itadunda kwakua Kila watakapoweka mitego watakuta uko vizuri.
Ila wale wafanyabiashara janja janja, unanunua Mali ya milioni 30 unaandikiwa Risiti ya milioni Moja wacha wafungiwe tu maana namna hakuna.
Nimewahi kuleteana Sana shida na Cashier wa duka Moja mtaa wa Tandamti ameniuzia kiatu cha elfu 90 halafu namdai risiti ananiambia mashine mbovu. Nikamwambia basi nirudishie fedha yangu... Ghafla mashine ikapona na nikapewa Risiti.
Hawa ndio watu Nape anawatetea yaani bureee kabisa. Mabarabara, Mishahara, Madawa vitanunuliwa kwa fedha toka wapi Sasa?