Mikopo ya nchi haiko secured na assets kama mikopo ya kawaida, mingi iko based on trust inayoangalia uchumi na hali ya kisiasa, na siku hizi wanatumia credit ratings companies kama Moody's , Fitch etc , ni wall Street companies na yame rate nchi zote duniani kwa kutumia data zinazoonyesha uwezo wa nchi kulipa na kukopesheka, ukishindwa kulipa mikopo kama nchi hawatachukua kipande cha ardhi au bahari sheria za kimataifa zinakataza, ila utailipa tuu hata baada ya miaka 1000, na uchumi wako unaweza kuanguka overnight na pesa yako ikawa useless, Argentina waliwahi kushindwa kulipa madeni inflation ya nchi ilifikia 275% (compare na yetu less than 10% lakini tunalia)