Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
DODOMA: Serikali imeahidi kuendelea kuweka uwekezaji mkubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa (BMH) ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za kibingwa na kibingwa bobezi nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, amepongeza hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa na hospitali hiyo na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwa bega kwa bega nao katika kuboresha sekta ya afya.
Dkt. Mwigulu amebainisha kuwa Rais Samia ametoa maelekezo ya makusudi kuhakikisha hospitali hiyo inapata ushirikiano na uwekezaji wa kutosha ili kuendeleza nia njema ya kuokoa maisha ya wananchi.
"Sisi ndani ya serikali tutaendelea kuwaunga mkono, na Mheshimiwa Rais alinituma nihakikishe hiyo; kwamba serikali itaendelea kuwa bega kwa bega nanyi. Kuweza kuhakikisha kama ambavyo tunaweka uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya, basi tutaendelea kuweka uwekezaji mkubwa katika hospitali yetu," alisema Dkt. Mwigulu.