Mwigulu Nchemba: Uchumi wa Tanzania umekua licha ya mlipuko wa COVID-19. Deni la Serikali ni himilivu

Mwigulu Nchemba: Uchumi wa Tanzania umekua licha ya mlipuko wa COVID-19. Deni la Serikali ni himilivu

Wenye kuelewa nondo za uchumi, hivi pato la taifa lina uhusiano gani na uchumi wa taifa?

Maana kasi ya ukuaji wa uchumi inasemwa kuwa imeshuka, lakini pato la taifa hapa latajwa kupanda...

Je, pato la taifa limepanda kwa sababu tumepunguza matumizi au tumeongeza sana kodi au tumeongeza vyanzo vya mapato?
 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema licha ya mlipuko wa COVID19, Tanzania ni miongoni mwa Nchi chache zilizokuwa na ukuaji wa Uchumi chanya kwa mwaka 2020.

Amesema Pato la Taifa la Tanzania lilikua kwa 4.8% na sekta zilizochangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji ni Ujenzi, Habari na Mawasiliano, Uchukuzi na Uhifadhi wa Mizigo, Huduma zinazohusiana na Utawala, Madini na mawe, Afya na huduma za Jamii

DENI LA TAIFA LIMEFIKIA TRILIONI 60.9, NI HIMILIVU

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema hadi Aprili 2021, Deni la Serikali lilikuwa Trilioni 60.9 ambapo kati ya kiasi hicho, Deni la Nje ni Trilioni 43.7 na la Ndani ni Trilioni 17.3. Deni linatokana na kupokelewa Fedha za Mikopo kwa ajili ya kugharamia Miradi ya Maendeleo

Imeelezwa, Deni ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika Kimataifa


Made in Tanzania, engineered by Dr Mwingulu
 
Mbona mnashindwa kumuelewa? You are thinking emotionally!

Amesema ni moja kati ya nchi chache zilizokuwa na ukuaji uchumi chanya 2020. Au kwenye hiyo 4.8% mmeona alama ya negative?

Na ni kweli nchi nyingi duniani uchumi ulikuwa unasoma negative something.

Sent using Jamii Forums mobile app
You are thinking ni kingereza gani braza?

Andika 'You think'
 
R.I.P Magufuli

Ulikataa lock down kwa watanzania licha ya chadema kukimbia bunge na kwenda kukaa lockdown.
Sasa uchumi umekua.
Sasa mkuu tumuamini nani kati ya Rais na Waziri
 
Uchumi wetu haushukagi

Ova
Unashukaga inategemea tunataka nini na tunaongea na nani ?

Mfano, Wanasema uchumi wetu ni imara na unakuwa kwa kasi kwasababu hatujaathirika na CORONA lakini Mabeberu wakitoa package ya mkopo nafuu kwaajili ya nchi zilizoathirika na CORONA na sisi tunataka🤣
 
Unashukaga inategemea tunataka nini na tunaongea na nani ?

Mfano, Wanasema uchumi wetu ni imara na unakuwa kwa kasi kwasababu hatujaathirika na CORONA lakini Mabeberu wakitoa package ya mkopo nafuu kwaajili ya nchi zilizoathirika na CORONA na sisi tunataka🤣
Haha nmekuelewa

Ova
 
Sekta ya mawasiliano iko ICU, kwa kuwaakwapulia mahela katika jina la ukwepaji kodi na kung'ang'aniza ku prove wrong mabeberu.

Beberu waalikubaliana na mtikisiko wa kiuchumi ila kwa sababu ya propaganda za kisiasa Tz za kutangaza makusanyo ya matrilioni. Nchi tajiri my foot!

Haya leo Vodacom taaban, Airtel ndiyo chichemi wanauza minara ili waikodi wapunguze maintenance costs wajaribu kupata faida, mabenki nayo Mungu saidia, sijui tulikula maharage ya wapi wakati tunafanya hayo yote.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Inawezekana kweli uchumi umekuwa ila kasi ya ukuaji ndio imepungua kutoka 7% tuliokuwa tukiambiwa wakati wa Magufuli hadi sasa 4.8%, ila nisichoelewa kabisa ni hili deni, limetoka wapi na tulikuwa tukiambiwa kuwa tunatekeleza miradi ya maendeleo kutokana na fedha zetu wenyewe? hii mikopo ya miradi ya maendeleo iliyokuza hili deni hadi kufikia Trilioni 60, zilikopwa kwa miradi gani?
 
Kuwa na mtazamo tofauti siyo kwamba ndo ni mpinzani mkuu, sema tunaangalia hali za watanzania kwa ujumla je kinachosemwa kinaendana na uhalisia wa maisha yetu?
Tofautisha national income na per capital income.Mwiguru anaongelea national income.Wewe unaongelea per capital income. Umesomea nn we?
 
Back
Top Bottom