Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Mheshimiwa kwanza nikupongeze, you are smart, but the problem is you are 'evil smart' sometimes.
Katika historia yako ya utumishi, umegundua siri ya namna ya kuwatumia watawala wakupe unachokitaka nitakupa mifano.
Kipindi cha Jakaya uligundua CCM ya wakati huo ni legevu, haina watu wa kwenda toe to toe na wapinzani, ukachagua njia ya kuwa militant, njia ya kuonesha makeke makeke ya kijeshi, ukichanganya na uwezo wako wa kuzungumza na kwa kuwa naturally akili unazo, tena nyingi tu, jicho la JK na wakubwa wenzie wakakuona, wakakufanya Naibu Ktibu Mkuu, na baadae Naibu Waziri wa Fedha, baadae alipoingia JPM akakupa uwaziri. Good!
Ila kuna tatizo moja lazima uelewe, kuna mambo kadhaa umefanya ama ukiendelea kufanya historia itakuweka upande mmoja mbaya sana na huenda mwisho wako ukawa mbaya mno nitakueleza.
1. Mwigulu usiwe tayari kusimama upande wa kuumiza watu ili mradi upande huo una nguvu za kukupa cheo.
a) Ulimsingizia Alfred Rwakatare Ugaidi, ukamsumbua sana, akapata tabu sana, hii yote kwa nini, kuwafurahisha wenye cheo kuwa una uwezo wa kuwakomesha wapinzani ili wenye uwezo wa kutoa vyeo wakuone? Sasa eventually ukishapata vyeo kwa mtindo huo, hiyo inasaidiaje kujenga siasa safi katika nchi, kitu ambacho ni muhimu kwa ajili ya amani, mshikamano wa kitaifa na maendeleo ya nchi?
2. Kauli yako ya kumtukana Abdu Nondo na kumlinganisha na Kinyago
Ni mfano mwingine tu namna unavyodhani kuwa kwa kupambana na watu wanaotia doa matendo ya watawala wanaokupa vyeo, basi utajikurubisha kwao, na kwamba watazidi kukuona na kwamba watakupa au kukuhakikishia usalama wa cheo chako. Hivi Abdu Nondo kumtetea na kumlilia Akwilina na kutaka haki juu ya kuuliwa kwake pasipo na haki ndo amegeuka Kinyago? As I said, you are very smart lakini you can be evilish smart na hilo halina mwisho mwema.
3. Kutetea watoto wanaopata Mimba mashuleni wafukuzwe shule
Kwa rekodi ulisikika bungeni ukitaka watoto waliopata ujauzito waachishwe masomo, ukasema wazi mambo ya uzazi na kusoma haviendi sawa, Ulisema hivyo bila kujali mustakbali wa watoto maelfu wasio na hatia ambao wanahitaji Elimu ili wajikomboe na umasikini, lakini wewe kwa kuwahukumu kupitia wao kubeba viumbe wa Mungu matumboni mwao, kubeba watanzania watarajiwa matumboni mwao unaona kuwa hawa watu hawastahiki kupata elimu!.
Yaani unataka kumuadhibu mtoto kwa kuleta uhai duniani kwa kumhukumia adhabu ya Ujinga. Sasa umepewa Wizara ambayo ina dhamana ya kusimamia sheria za nchi na haki za kikatiba za watu, nina wasiwasi kuwa kwanza utawezaje kulinda haki za watu kwa mtindo huu wakati unaamini kabisa watoto kuwa na mimba ni kosa kubwa sana la kustahiki wanyimwe Elimu kisa tu wana viumbe ambao ni Watanzania wenzako watarajiwa matumboni mwao. But naamini, haya uliyafanya ili uwe katika mtizamo sawa na wanaogawa vyeo bila kujali athari nzima za maelfu ya watu. You care about yourself and you can sacrifice anyone for the sake of power!
4. Ishu ya Korona
Katika kitu ambacho jamii inaweza ikakuhumu mno mno ni hili suala la kuamua kuexploit incompentency ya mamlaka kwenye kuhandle hili tatizo la Korona ili wewe uweze kupanda tena kwenye ngazi ya mamlaka. Kama nilivyokueleza, you are smart, lakini hata shetani naye ni smart sana. Uligundua Sauti ya utetezi juu ya Mgawa vyeo anavyoendesha mapambano dhidi ya Ugonjwa wa mauaji ya halaiki ya watu wa Korona kuwa ni hafifu ndani na nje ya chama chenu, ukaona huu ni wasaa wa kupaza sauti usikike na uonekane, hukujali maisha ya watanzania, hukujali kuwa ugonjwa huu ni existential threat ya wananchi, Unajua wazi kuwa hali ni mbaya mbaya sana, lakini ufanyeje ukaona haya yooote siyo kitu, ila kilicho cha msingi ni kusimama na anayeweza kugawa vyeo ili akupe cheo.
Ukatumia dakika zako chache bungeni kuponda sauti yenye hekima na ukweli ya namna ya kuliponya Taifa hili, ukaamua kuside na watu wanaosema "Korona ni ugonjwa mdogo", Ukaamua kuulinda unafiki wa mtu ambaye yeye binafsi kakimbia ofisi na kujipa "work from home" na "social distancing" ili yeye asipate Korona huku yeye akiwaambia wengine kuwa hali ya Korona siyo mbaya kihivyo wachape kazi wakati yeye kakimbia ofisi, Mtu ambaye anawaza kufungulia ligi ya mpira huku yeye kajifungia ndani na kuigeuza nyumba yake binafsi aliyoijenga kwa jasho lake na mkewe kuwa ndo ofisi ya kufanyia kazi za wananchi. Wakati unatetea hayo, watu wanakufa wengine wanazikwa usiku, wananchi wanahaha kuhusu hali yao, hukutaka kusimama nao Ukaamua kusimama na wagawa vyeo, ili upate vyeo!.
Na yeye anayegawa vyeo ni mjanja pia, akaamua akupe ili atume message fulanifulani kwa wenzako ndani ya chama kwamba kuna "Carrots" kadhaa unaweza kupata ukisimama na miye kwenye ishu hii ya korona. Ni kama Bashe tu alivyopewa cheo ili kutuma coded message kwa watu wa chama chako kuwa kama ukisimama na mimi dhidi ya makatibu wakuu wastaafu na waraka wao basi kuna "Tonge" zuri tu unaweza kumegewa, na iliwork, ila this time hii ya Korona haitawork kwa sababu Korona haichagui wapinzani wala CCM. Ikitandika itatandika kote, na sauti za resistance zitatokea pande zote, ndani ya CCM. na nje, na hakuna vyeo wala pesa za kuwanyamazisha wote hawa, wala vyombo vya dola havitaweza kuzima sauti hizi!.
Mwigulu kwa kutafuta cheo kwa nguvu unataka serikali isitangaze takwimu za maambukizi mapya na vifo vya korona kwa uharaka na uwazi, ili umfuruhishe mgawa vyeo anayeonekana kukubaliana na wewe katika hili, Mheshimiwa hivi hujui kuwa sisi ni wanachama wa WHO wanaolazimika kutoa taarifa mara kwa mara za maambukizi, vifo na kupona ili dunia iweze kupata picha ya hali halisi ya mapambano ya janga la ulimwengu mzima?. Cheo kisikufanye usione mambo haya
Mwigulu,
Kuna namna unavyoweza kufanya siasa na kupanda vyeo bila kuwatupa chini ya basi watu wananchi/watu na maisha yao. Jifunze basi uungwana wa mzee Mwinyi, Mzee Mwinyi yeye alichapa kazi wakati wa ujana wake, hakuwa na sababu za kutetea yasiyoteeteka ili apande vyeo na ndiyo maana alijiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani na Eventually akawa rais serikali zote mbili, ya Zanzibar na JMT. Mungu atakunyanyua tu ukiwa Muungwana na mchapakazi, huna haja ya kuwa tayari kuunga mkono siasa hata kama ni za kuzimu ili wewe upande vyeo
Kwa kuhitimisha:
Kuna namna unavyofanya siasa sometimes ni njia sahihi, huwa ninapenda unavyokwenda man to man na Zitto mtandaoni, hiyo ni sahihi, allegation lazima ijibiwe, lazima uchokonoe hoja ya mwingine ili kuitia matobo, Lakini katika mambo ya msingi yanayohusu haki za Wananchi haswa haki ya uhuru na kuishi na haki nyingine za kikatiba za wananchi vinapokuwa at stake brother hebu rudisha roho nyuma kidogo.
Nadhani kipindi ulipokuwa benchi utakuwa umejifunza kitu kuwa Vyeo hivi vinapita, muda wowote unaweza kurudi benchi. Sasa kama ulipanda maua yataendelea kukunukia harufu nzuri hata ukiwa mbali, Ila na wewe ukiamua kuchimba Shimo ili watu watumbukie ili ulinde cheo, basi ipo siku na wewe utatumbukia humo au kama siyo wewe watoto wako
Mheshimiwa Akili unazo basi zitumie kwa wema na si uovu.
Missile of the Nation(Kombora hatari kabisa la Ulinzi wa Taifa)