Mwigulu Nchemba: Wahitimu vyuo vikuu rudisheni mikopo

Ni hatari Sana kumkopesha Mtu ambaye hauna uhakika wa ye ye kukulipa
 
Gulu inaonekana hazina na mifumo hazisomani.
 
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wahitimu wa vyuo vikuu kurejesha mikopo waliyopata kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ili wanafunzi wengine wasio na uwezo pia wanufaike.

Hotuba ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo kwa niaba ya Dkt. Mwigulu wakati wa mahafali ya 50 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alisisitiza kuwa mikopo hiyo imetolewa inakusudiwa kuzunguka na kuwanufaisha wengine.

“Naelewa kuwa baadhi yenu mliohitimu leo (Jumamosi) mliweza kufikia hatua hii muhimu baada ya kupata mikopo kutoka HESLB, Hii ndiyo nia ya serikali ya kuwatumikia wananchi wake bila kujali hali zao. Mpango huo ulianzishwa kwa wale wanaohitimu elimu ya juu lakini wanakabiliwa na vikwazo vya kifedha.”

"Niwakumbushe wanufaika wa mikopo ya serikali kuwasaidia wenzao katika kufikia ndoto zao kwa kuanza kurejesha mikopo yao,"

Waziri aliongeza kushindwa kurejesha mikopo hiyo kutaathiri jitihada za serikali za kuwawezesha wananchi wengi kupitia elimu.

Mwigulu .png

Source: East Africa Radio
 
Huyu nae aache ulevi wakati wa kazi! Serikali haiwezi kukusanya madeni ya HESLEB kwenye vijiwe vya bodaboda na mabandà ya chips.
Waajirini muone kama mtaishia kutoa matamko ya kilevi kwa wasio na ajira.
 
Mikopo iwe buree kabisa yaani isiwe mikopo tena bali iwe ni pesa mwanafunzi anapewa bure.

Unajua kabisa nasomea ualimu na unajua huna uhakika wa kuja kuniajiri sasa unanikopesha ili nije nikulipe vipi?

Nisomee ualimu halafu nije nikulipe kupitia uuzaji wa vitumbua!!!??

Serikali haipo makini kwenye suala la mikopo. Mkopeshwaji hana hata dhamana ya mali bali ni dhamana ya mtu, akifa je?? Anadaiwa nan?

Wanufaika wengi ni miaka hawajalipa hata mia, mtawakamata? Hyo ghalama ya kuzunguka nchi nzima na nje ya nchi kutafta wadaiwa mnayo?? Mkiwapata muwaweke jera, wale na kulala kwa kodi za walioko uraiani??

Sameheni madeni yote na muache kukopesha hasa hasa kwa coz ambazo mnajua kabisa ajira zake ni ngumu sana.

Ajira ziwe za mkataba kama ni 15yrs iwe hivyo ili kila mtu apate walau mtaji tu wa kuanzisha biashara ya kumwezesha kulipa hayo mamikopo wakati huo huo akijimudu kimaisha.
 
Ajira za muda mfupi na mikataba znahtajika ili kila mdeni aajiliwe angalau miaka15 huku akirejesha deni..sio mtu kukaa kwenye ajira miaka60...
 
Back
Top Bottom