Mwigulu: Nimekuja, Nitawashikisha adabu wote wasio na Adabu, tuache kushikilia Mali ya Mtu anayedaiwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesema serikali haitavumilia vitendo vya kushikilia mali na vitendea kazi vya wafanyabiashara, akisisitiza kuwa tabia hiyo inakwamisha uzalishaji na ukuaji wa uchumi. Amesema viongozi na watendaji wanapaswa kuacha mazoea ya kukamata mali za watu wanaodaiwa, kwa kuwa hatua hizo huathiri uwezo wao wa kuendelea na shughuli za kiuchumi.

Soma zaidi: Maafisa wa Wilaya ya Ikungi (Singida) wanafunga biashara zetu na kututishia

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma katika eneo la Kambi ya Nyasa Mei 17, 2026, Mwigulu amesema msimamo wa serikali ni kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya kazi katika mazingira yanayowawezesha kuongeza uzalishaji na kulipa kodi bila vikwazo visivyo vya lazima.

"Mapato yameongezeka maana yake wale wanaolipa... wale walio lipa wameongeza uzalishaji. Sasa mtu unayetaka azalishe, huku unaenda unakamata kitendea kazi. Unataka akulipe, huku unaenda unakamata kitendea kazi, analipaje?

Sasa, wanasema wamezoea. Sasa mimi nimekuja, nitawashikisha adabu wote wasio na adabu.

Kuna watu... kuna watu mpaka wanafika serikalini... kuna watu mpaka wanafika serikalini, mpaka wanafika kwenye ofisi, mpaka wanafika kwenye wanashika nafasi, hawajui maisha ya Watanzania. Hawayajui. Hawayajui. Tujifunze maisha ya watu wetu yakoje. Tujifunze."

Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesema serikali haitavumilia vitendo vya kushikilia mali na vitendea kazi vya
Anaweza akawa anafanya haya kwa Nia njema kabisa mwigulu lakini doa la mauaji ya oktoba 29 likawa linaziba Kila kitu chema kisionekane ndio maana tunatamani kuona walioua wanawajibishwa na tukae tufikie maridhiano
 
Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesema serikali haitavumilia vitendo vya kushikilia mali na vitendea kazi vya wafanyabiashara, akisisitiza kuwa tabia hiyo inakwamisha uzalishaji na ukuaji wa uchumi. Amesema viongozi na watendaji wa
Naona Mwigulu anataka kujibrand kama ndio Magufuli ili agombee urais 2030.
 
Kuna watu wa halimashauri, wanataka tukate leseni ya biashara kwa lazima,ukiwa huna leseni wanakufungia duka,wakati huohuo una lipa kodi TRA je mh. Dkt mwigulu nchemba hii ni sahihi?
 
Anaweza akawa anafanya haya kwa Nia njema kabisa mwigulu lakini doa la mauaji ya oktoba 29 likawa linaziba Kila kitu chema kisionekane ndio maana tunatamani kuona walioua wanawajibishwa na tukae tufikie maridhiano
Tunapaswa kuanza na watu waliowachochea watoto wa watu kuingia barabarani
 
kwa hiyo tafsiri yake hakuna haja ya kulipa madeni? na kama hakuna atakayelipa madeni wengine watapata wapi mkopo?

low iq stupid folks …
 
Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesema serikali haitavumilia vitendo vya kushikilia mali na vitendea kazi vya wafanyabiashara, akisisitiza kuwa tabia hiyo inakwamisha uzalishaji na ukuaji wa uchumi. Amesema viongozi na watendaji wanapaswa kuacha mazoea ya kukamata mali za watu wanaodaiwa, kwa kuwa hatua hizo huathiri uwezo wao wa kuendelea na shughuli za kiuchumi.

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma katika eneo la Kambi ya Nyasa Mei 17, 2026, Mwigulu amesema msimamo wa serikali ni kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya kazi katika mazingira yanayowawezesha kuongeza uzalishaji na kulipa kodi bila vikwazo visivyo vya lazima.

"Mapato yameongezeka maana yake wale wanaolipa... wale walio lipa wameongeza uzalishaji. Sasa mtu unayetaka azalishe, huku unaenda unakamata kitendea kazi. Unataka akulipe, huku unaenda unakamata kitendea kazi, analipaje?

Sasa, wanasema wamezoea. Sasa mimi nimekuja, nitawashikisha adabu wote wasio na adabu.

Kuna watu... kuna watu mpaka wanafika serikalini... kuna watu mpaka wanafika serikalini, mpaka wanafika kwenye ofisi, mpaka wanafika kwenye wanashika nafasi, hawajui maisha ya Watanzania. Hawayajui. Hawayajui. Tujifunze maisha ya watu wetu yakoje. Tujifunze."

Sokoine wa pili is real aise,

well done Dr Mwigulu Nchemba, the PM of Tanzania
 
Wafanyakazi wengi wa serikali wanafanya hivyo sababu ya rushwa, ni wapuuzi sana. Yaani Tanzania ni kugumu mno kama unafanya shughuli za biashara na hasa pale ambapo unafanya biashara na una mkwamo wa kuilipa serikali.

kwa kawaida ukishindwa kulipa deni unafirisiwa na mali zako kukamatwa, hiyo ni kawaida dunia nzima deni ni lazima lilipwe, haiwezekani unadaiwa halafu unaendelea kufanya biashara, kwa nini usilipe deni kama unaingiza kipato? kama kila mtu anayedaiwa asipolipa mikopo kwa wengine itatokea wapi? …
 
Huyu mwigulu haoni kama anaingilia utaratibu ulio ndani ya sheria?
Ukikopa sharti urejeshe, kinyume na hapo utaratibu kulingana na makubaliano ya mkataba lazima ufuatwe.
 
kwa kawaida ukishindwa kulipa deni unafirisiwa na mali zako kukamatwa, hiyo ni kawaida dunia nzima deni ni lazima lilipwe, haiwezekani unadaiwa halafu unaendelea kufanya biashara, kwa nini usilipe deni kama unaingiza kipato? kama kila mtu anayedaiwa asipolipa mikopo kwa wengine itatokea wapi? …
That's a cheap argument.
Kukamata mali za unayemdai lazima ifuate mkondo wa kisheria,
 
sidhani kama wanakuja tu kukamata kwa kuwa unadaiwa, mara nyingi na kwa kawaida wanaokamatiwa mali ni wadaiwa sugu, na nielewavyo kukamata mali huwa ni hatua ya mwisho kabisa baada ya efforts zote za kumtaka mdaiwa alipie deni lake kugonga mwamba …
 
Wafanyakazi wengi wa serikali wanafanya hivyo sababu ya rushwa, ni wapuuzi sana. Yaani Tanzania ni kugumu mno kama unafanya shughuli za biashara na hasa pale ambapo unafanya biashara na una mkwamo wa kuilipa serikali.
Tunaofanya kazi na serikali tunajua sema Mwigulu ni mwanasiasa analafu mtu wa propaganda anajua wananchi wanataka maneno gani njoo kwenye utekelezaji je ayo
Kayasema jukwaani yaiataishia jukwaani
 
sidhani kama wanakuja tu kukamata kwa kuwa unadaiwa, mara nyingi na kwa kawaida wanaokamatiwa mali ni wadaiwa sugu, na nielewavyo kukamata mali huwa ni hatua ya mwisho kabisa baada ya efforts zote za kumtaka mdaiwa alipie deni lake kugonga mwamba …
Bado deni lazima lithibitike kisheria.
 
Bado deni lazima lithibitike kisheria.

ofcourse sidhani kama kuna mamlaka za kiserikali au zozote zile zilizoko kisheria zinaweza "kuruhisiwa" kufunga/kutaifisha mali zako bila ya kufwata sheria inayowaruhusu kufanya hivyo, wanaofanya hivyo ni lazima sheria inawaruhusu vinginevyo wasingekuwa na uhalali wa kutaifisha mali na unaweza kuwashitaki, kwani kama sheria haiwaruhusu inakuwa ni uporaji ambalo ni kosa kisheria ...
 
Back
Top Bottom