PostGE2025 Mwigulu: Polisi waache kumtafuta Askofu Gwajima, Muacheni aendelee na ibada zake tujenge umoja wa kitaifa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameliagiza Jeshi la Polisi liache kumtafuta Askofu Dkt. Josephat Gwajima kama walivyokuwa wametangaza awali ili aweze kuendelea shughuli zake.

Amesema baada ya kutoa msamaha kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, waumini wanahitaji wamuone kiongozi wao, hivyo anatakiwa ajitokeze hadharani aendelee na kazi yake. “Mwacheni ajitokekeze tujenge umoja wa kitaifa, tushikamane kurudisha umoja wa kitaifa. Tumekutana na TEC, viongozi wa dini, wa mila na viongozi mbalimbali; twendeni sote kwenye jambo hili, tujitokeze tuhamasishe Tanzania yenye amani, huu ndio wito wa kiongozi wetu wa nchi”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Novemba 30, 2025) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Arumeru katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Magufuli Leganga, kata ya Usa River, wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Waziri Mkuu amewataka Watanzania wakatae kushawishiwa na wanaharakati wanaochochea vurugu kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi. "Nimekuja kuwapa pole wananchi wenzangu, kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Anatambua mambo yanayoendelea. Anatambua kazi kubwa ya kujenga Taifa mnayoifanya," amesema.

Kabla ya mkutano huo, Waziri Mkuu alikagua uharibifu uliofanywa wakati wa vurugu za Oktoba 29, mwaka huu kwenye kituo cha polisi cha Kikatiti (mita 500 kutoka barabara kuu ya Arusha - Moshi); Mahakama ya Mwanzo ya Maji ya Chai (km. 3 kutoka barabara hiyo kuu); kituo cha mafuta Total Energies kilichopo Maji ya Chai (kipo barabarani) ambavyo vyote vilichomwa moto ikiwemo kuiba mali kwenye supermarket na kubomoa sefu ya kutunzia fedha.

Waziri Mkuu amesema masuala ya maendeleo ya wilaya ya hiyo kama vile maji na barabara yamo kwenye Ilani ya CCM na kwenye ahadi za Mheshimiwa Rais lakini yatafanyika endapo tu nchi itakuwa na amani. “Tukichagua vurugu tutakuwa tumechagua kufukuza maendeleo, tukichagua vurugu tutakuwa tumechagua kuongeza umaskini kwa mtu mmoja mmoja," ameonya.

"Kila Mtanzania akatae haya yaliyotokea juzijuzi. Tumechochewa, tumechonganishwa lakini wao wako nje, wanalipwa ili kutuvuruga tu. Wengi wanaochochea vurugu ni wanaharakati, wako nje ya nchi. Hakuna kiongozi wa chama cha siasa anasema wananchi wafanye vurugu. Au mmemuona?" alihoji.

Amesema baadhi ya vijana walioko nje ya nchi wamebainika kupokea dola za Marekani milioni mbili (sawa na sh. bilioni 4.5) ili wachochee vurugu. “Hawa wanaowalipa, wana maslahi gani na nchi yetu? Wana ajenda gani na nchi yetu? Tunajua watazirudishaje hizo fedha?”

“Hawa watu wanalenga tugombane ili wachukue madini adimu (rare earth minerals). Sasa hivi Tanzania imegundua uranium ambapo inakuwa nchi ya tisa duniani na ya kwanza barani Afrika. Ina tani za ujazo 890,000. Hii ni karibu tani milioni moja."

Waziri Mkuu ameonya dhidi ya mchezo unaotumika kuanzisha chokochoko ili kusambaratisha nchi pindi inapobainika kuwa na rasilimali. Amesema ziko baadhi ya nchi barani Afrika ziliathirika kutoka na chokochoko hizo. “Wanaanzisha chokochoko, wanaacha mnavurugana, rasilmali zikiisha, wao wanaondoka,” amesisitiza.

"Watanzania tuamkeni, tuchukue tahadhari. Kuna kamchezo kanachezwa. Wanajua Tanzania ina gesi asilia nyingi na inakaribia kuanza. Wanajua ikianza miradi hii, Tanzania itakuwa ya kwanza katika Afrika Mashariki na wala hatutahitaji kutoa mikopo ya wanafunzi."

Amewataka Watanzania waamke na kukataa kurudishwa tena kwenye hali ya vurugu. "Watanzania tuamke, tukatae kurejeshwa kule nyuma. Umaskini utaondolewa nchi ikiwa kwenye amani. Ajira za vijana zitaweza kupatikana nchi ikiwa kwenye amani."

Amesisitiza kuwa vurugu zikiwepo, hata wakulima wa karoti na nyanya wa Ngarenanyuki hazitauzwa na hivyo kuathiri uchumi wa mtu binafsi.

huyu jamaa ubongo wake umejaa kinyesi si bure
 
Mbona hajesema waliotekwa pia waachiwe
 
Kwani TZ kuna waziri mkuu mwingine nisaidieni
 
Serikali Pumzi imekata na sasa wanataka maridhiano... Hivi wanaridhiana kitu gani bandugu, mwenye kufahamu tafadhari... ni kuhusu mauwaji, kubaka uchaguzi? kuwatesa wapinzani wao au ni nini haswa...? Raisi atoe msamaha wa jumla kwa wafungwa na mahabusi wote wa kisiasa, awaite wapinzani wake kwa style ya kikwete, wanywe juisi, waombane msamahawa wa wazi, wakubali uwajibikaji etc, ndio wananchi wataanza kuwaonea huruma... mpaka sasa wanachofanya ni 0. wafungulieni polepole, mdude Lissu na muwaombe musamaha familia za walio uwawa, muwape kifuta jasho... labda labda ndipo mtaanza kufikiriwa.. mpaka sasa, ni kubwabwaja tu na huyu PM ni kama vile chemical Ali wa Sadam Hussein... anaongea ongea tu. Atachuja mapema sana kwa style hii ya uongeaji huku vitendo sifuri...
 
Usiwe sana kihere kihere Cha kujibu , Waziri wako uchwara ndo alomfuata kitima ofisini kwake kumuomba msamaha

Uchawa Kwa sasa ni laana
Tafuta kazi zingine za kufanya kukuingizia kipato
Ofisi ya waziri mkuu ndiyo ofisi ya kitima?..alimuomba msamaha kwa kosa gani?
 
Msamaha kiaje yaani!! kwani kabisa likikosea Nini??? waache kujipa umuhimu Gwajima kama huko huko utasalisha live YouTube usijitokeze.
 
Leo tumewasamehe, kesho pengine litakuja wazo walipwe fidia ya vinavyodaiwa kupotea kipindi wako chini ya ulinzi.
 
Mmemsamehe kwa makosa yapi? Gwajima alikemea watu kutekwa na kuuwawa, mkalifungja kanisa na kuanza kumsaka, sasa mnasema mmemsamehe kwa kosa gani? je kukemea utekaji ni kosa? Je kuteka na kuuwa watu ni halal? na ni kwa faida ya nani?
 
Back
Top Bottom