Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, amempongeza Deogratius Ndejembi kwa kuonekana na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa msaidizi wake.
Jana, Jumatano, Agosti 26, 2026, Ndejembi alipendekezwa na vikao vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Makamu wa Rais, kuchukua nafasi ya Dkt. Emmanuel Nchimbi, aliyejiuzulu.
Leo, Alhamisi, Agosti 27, 2026, katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma, Mwigulu ameanza kwa kutoa pongezi kwa Ndejembi, ambaye kabla ya kupendekezwa alikuwa Waziri wa Nishati.
Soma: Deogratius Ndejembi ateuliwa kuwa Makamu wa Rais
Aidha, Mwigulu amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumwona Ndejembi, ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, Mkoa wa Dodoma, kuwa Makamu wa Rais.